October man
JF-Expert Member
- Nov 23, 2017
- 3,635
- 5,012
Nime sabusklabu hapa nipate chochote
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda used ila vifaa vipya nadhani itakuwa ngumu kwa hiyo pesa.Hapana ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa
Hata used hapatiLabda used ila vifaa vipya nadhani itakuwa ngumu kwa hiyo pesa.
🤣🤣 Mangi mwenzangu unamwambia tena hata used hapati, labda ungemshauri atafute Kodi kwanza mengine atayajua yanakaaje?....
Uliuziwa location gani mkuu?Mimi nimeuziwa salon mzima mzima laki 7 jamaa alitumia garama zoote nikalialia had laki 6. Sasa wewe laki 5 jipange mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimeuziwa salon mzima mzima laki 7 jamaa alitumia garama zoote nikalialia had laki 6. Sasa wewe laki 5 jipange mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
😎😎Sasa nitakuorodheshea manunuzi ya vifaa haraka haraka
Mashine lazma uwe nazo mbili moja original ambayo zinakuwa na warranty ya mwaka mmoja so unaweza kupiga kaz miaka miwili hv na hyo mashine wanauza kuanzia 125k-150k unatakiwa uwe na fake ile kwa ajili ya kuchongea na ndevu wanauza 30k kuna apron 20k kiti cha kukalika andaa 200k afu kuna kioo cha ukutani 70k afu kuna feni andaa 65k afu kaframe ka kuwekea vitu wanauza 250k ukichonga mwenyew 150k baada ya hapo weka mengneyo 100k
😎😎Kinyoz kutegemeana na location anakupa 35-50 kwa week zen umeme ni juu yake ww ni kod kila mwisho wa mwez
Haya mambo yakaugiza mpaka mwezi ndio mzigo uje na meli .
Nenda Pale Radium Salon Equipments company limited
Kuna kila kitu
Niliwahi kununua pale kama miaka mitatu iliyopia Full Set ya salon equipments.Yaani ukitoka pale hununui kitu sehem nyingine wana hadi mataulo.
Ukifika pale utapata wazim kwa jinsi walivyosheheni vifaa.
Wapo Town,mitaa ya kueleka Swahili Street
Ukipotea wapigie 0713 608681 watakuelekezo walipo
Nio bora uende pale then ndio utapata tathmini ya Gharama ya Salon kamili.Maana hata mie ndio nilivyofanya
Sio kwamba nawafagilia ila ni Dar nzima hawa ndio jamaa walio sheheni vifaa vyote vya Salon.
We ulikosea ulitakiwa uweke kipande kwa siku kama Bodaboda mkuu.Biashara yake kichaa sana yan..waliowin kwenye hii biashara wachache sana yan..nna experience nzuri sana adi nlijuta nliwekeza M 3 mwaka 2013 ila niliijutia ile ela kuliko kitu kingine chochote..kwanza anafungua ofisi mda anaotaka yy..akiamua anakuja akiamua haji..vinyozi washenzi sana..