Biashara ya Samaki vs Maziwa

Biashara ya Samaki vs Maziwa

Cleverman324

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2018
Posts
389
Reaction score
631
Habari wanajamvi nimerudi tena hustler mkomavu.

Mwanzoni mwa mwaka niliweka nadhiri ya kutembeza biashara kutokana na mtaji kuwa finyu nilianza na mtaji wa 42,000 kwa kuwa baadhi ya vifaa nilikuwa navyo, nilianza kuingia mitaani kuuza samaki kwa miezi miwili mfululizo nikaweza kuanzisha biashara ya maziwa ya mgando nikawa nabeba vyote mpaka leo.

Changamoto ni nyingi na faida pia inapatikana nimeweza kununua freezer na delli mbili chupa za chai nne kubwa meza za plastic mbili viti sita. Ninaomba msaada wa kimawazo juu ya hizi biashara maana naona umefika wakati wa kushikilia moja kwa sasa hasa kuweka kijiwe kabisa ili asubuhi natembeza namuacha binti kwenye kijiwe nikirudi tunaendeleza mpaka jioni.

Tuanzie kwenye samaki, hawa wanatembea mno ila wana gharama sana kwenye kuwaandaa na hata upatikanaji wake.na faida ni robo ya kile ulichowekeza, kwa upande wa maziwa pia pako vizuri na hamna changamoto sana na faida unapata nusu ya uulichowekeza.

Naombeni msaada wenu nikimbizane na ipi kati ya hivyo, na vipi kuhusu location nzuri. Mimi niliopt Kijichi au Tabata.

Naombeni mnipe mwangaza.

20191008_092414.jpg


20191115_174531.jpg


20191115_174446.jpg


20191115_174442.jpg
 
Hongera sana hAssler.Ni bahat mbaya kuwa nyuzi zenye madini kama hizi hazipari wachangiaji wa kutosha.
 
Mwamba usife moyo zidi kukaza.Customer care izidi kuwa vizuri kwenye huduma zako zote na uaminifu.
 
Ahsanteni sana wakuu kwa kunipi sapoti..nimeopt kutambaa na mtindi maziwa fresh na kahawa..ila kwenye bite kuna changamoto ya sambusa au chapati kupoa...
 
Mbona umeficha sura sasa? Hahaa unacho hofia ni nini?

By the way Biashara ya Maziwa ni nzuri kama source ya maziwa ni Ng'ombe wako na kama sio wako basi labda ununue na ku add value kabla ya kuuza tena. Ila kama source ni wewe basi hata ukiuza Raw bado ni Ok tu
 
Uza Alkasus mkuu kwa sasa ina wanywaji wengi sana.
 
Back
Top Bottom