Biashara ya Samaki vs Maziwa

Biashara ya Samaki vs Maziwa

Kahawa unauza hii ya kwenye kopo au ya vile vikombe vya udongo vidogo
Nipo maahabara natengeneza recipes. Ya hiyo kahawa..ni vyema tukiwa wabunifu kidogo natafta namna tofauti kidogo sitafanya kama wale wa birika
 
Nipo maahabara natengeneza recipes. Ya hiyo kahawa..ni vyema tukiwa wabunifu kidogo natafta namna tofauti kidogo sitafanya kama wale wa birika
Screenshot_20191128-151313.png
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hili andiki lina milalo miwili mikuu. Mmoja ni kujikuza mimi mwenyewe kwa kupata mawazo ya wadau na mlalo mwengine ni kum inspire huyu kijana aliegraduate ama anaefikiria cha kufanya ili tumkomboe..ningependa andiko hili liwe darasa kwani ninaahidi kutoa mrejeshowa kila hatua nayopitia..kwa kufanya hivyo hata walio wengi wanaofanya shughuli hii watajua wamekosea wapi na nini warekebishe
 
Habari wakuu nipo sinza hapa aficasana kwa makjuice. Nimeanza savey kwa madereva tex
 
Location, muhimu ni wapi unauza kirahisi na haraka, kama hapo ulipo mzigo unatembea haraka komaa hapo hapo usifuate majina ya mtaa
Umeona mbali sana mkuu. Kama umeshatengeneza empire yako na kuitelekeza kwenda kutafta nyingine uanze moja ni kupoteza resources...ninaanzia hapa hapa na wateja hawa hawa huku nikipanua mbawa taratibu
 
Habari wanajamvi..miezi kadhaa nilianza biashara kwa mtaji usiozidi laki..ukakua na kuweza kufikua lakinne. Niliomba ushauri juu ya biashara ya samaki au maziwa lakini wadau walipendekeza maziwa...sasha niliendelea na kutembeza maziwa nakufanikiwa kukuza mtaji..sasahivi nimeweza kutengeneza milk point maeneo ya kijichi..natarajia kufika mbali said na kuingia kwenye ushindani na hawa wenye cafe subway.
 
Habari wanajamvi nimerudi tena hustler mkomavu.

Mwanzoni mwa mwaka niliweka nadhiri ya kutembeza biashara kutokana na mtaji kuwa finyu nilianza na mtaji wa 42,000 kwa kuwa baadhi ya vifaa nilikuwa navyo, nilianza kuingia mitaani kuuza samaki kwa miezi miwili mfululizo nikaweza kuanzisha biashara ya maziwa ya mgando nikawa nabeba vyote mpaka leo.

Changamoto ni nyingi na faida pia inapatikana nimeweza kununua freezer na delli mbili chupa za chai nne kubwa meza za plastic mbili viti sita. Ninaomba msaada wa kimawazo juu ya hizi biashara maana naona umefika wakati wa kushikilia moja kwa sasa hasa kuweka kijiwe kabisa ili asubuhi natembeza namuacha binti kwenye kijiwe nikirudi tunaendeleza mpaka jioni.

Tuanzie kwenye samaki, hawa wanatembea mno ila wana gharama sana kwenye kuwaandaa na hata upatikanaji wake.na faida ni robo ya kile ulichowekeza, kwa upande wa maziwa pia pako vizuri na hamna changamoto sana na faida unapata nusu ya uulichowekeza.

Naombeni msaada wenu nikimbizane na ipi kati ya hivyo, na vipi kuhusu location nzuri. Mimi niliopt Kijichi au Tabata.

Naombeni mnipe mwangaza.

View attachment 1271838

View attachment 1271839

View attachment 1271840

View attachment 1271841

Safi sana, mimi nilikuwa na wazo La baishara ya samaki.tafadhali naomba contacts zako inbox tuwasiliane
 
Safi sana, mimi nilikuwa na wazo La baishara ya samaki.tafadhali naomba contacts zako inbox tuwasiliane
Biashara ya samaki ipo fresh sana kinachotakiwa ni kujituma tu
 
Hongera kwa kua jasiri,tulio wengi tunashindwa kufanya biashara hasa za mitaji midogo kwa kuangalia status zetu,
Warren buffet alianza kwa kutembeza magazeti mtaani..ila sasa dunia inamtambua
 

Attachments

  • 20200425_160545.jpg
    20200425_160545.jpg
    99 KB · Views: 35
  • 20200425_160557.jpg
    20200425_160557.jpg
    81.3 KB · Views: 35
  • 20200421_121157.jpg
    20200421_121157.jpg
    169.2 KB · Views: 34
  • 20200421_204213.jpg
    20200421_204213.jpg
    78.5 KB · Views: 35
  • 20200425_162128.jpg
    20200425_162128.jpg
    88.5 KB · Views: 31
  • 20200425_162120.jpg
    20200425_162120.jpg
    121.7 KB · Views: 30
  • 20200415_185625.jpg
    20200415_185625.jpg
    95.6 KB · Views: 31
Back
Top Bottom