Biashara ya samaki

Kusema ukweli bado sijahmini kuwa umeweza kufuga sato had anafika kilo 5. Ukiprove hakika soko ninakutaftia tena la uhakika
 
Mkuu uneshaanza, tupe mrejesho in depth.
 
mkuu mbeya upo sehemu gani,,kwa msaada zaidi ukihitaji ngomb'e nenda maeneo ya bonde la usangu siku za minada wanauzaga ng"ombe cheap sana,,

na kuhusu kufungua mashine ya mchele,naomba unielekeze kidogo ghalama za hyo mashine kuinunua,,hata mm nina plani ya kufanya biashara hyo ya mchele,,nina stoo uwa najumua mpunga huko rukwa
 
Habari zenu wakuu,
Ni makusudio yangu kuanzisha biashara ya kusafirisha samaki aina ya sato na sangara kutoka mwanza kwenda dar es salaam. Kwa mwenye uzoefu na ushauri juu ya changamoto na fursa zinazoendana na biashara hiyo ningefurahi kupata mawazo yao. Natanguliza shukrani, karibuni kwa mjadala
 
Wakuu heshima kwenu,

Wakuu naomba kusaidiwa kwa wenye uzoefu au uelewa wa biasha ya bucha za samaki, hasa ningeomba kusaidiwa katika maeneo yafuatayo;-

1) Upatikanaji wa frem za biashara,
2) Leseni ya biashara,
3) Mtaji wa kuanzia,
4) Namna ya usafirishaji wa samaki (Mwanza to Dar)
5) Upatikanaji wa wateja katika eneo husika (Dar),
6) Changamoto za biashara.

Eneo lengwa la biashara ni jijini Dar, natazamia kufanya biashara ya samaki wa maji baridi yaani kusafirisha samaki kutoka Mwanza mpaka Dar, naomba kujuzwa nimaeneo gani haswa hii biashara inalipa.

N.B. Hizi zote ni jitihada za kukubaliana na wito wa serikali yetu wa kutaka vijana tujiajiri japokuwa haiweki malengo ama mikakati ya vipi vijina tunaweza kujiajiri.

Naomba kuwasilisha wakuu, natumaini nitapata msaada.
 
Haya wahusika wa mtoni maeneo ya Migori karibuni biashara ya samaki kambale, perege, mchena na wengineo. Bei ni shiling ngapi toka kwa wachuuzi?
 
mimi nipo mwanza najishughulisha na shughuli za samaki na dagaa wa kukaanga ukihitaji taarifa zaidi 0759292980
 
Habari wadau,

Baada ya kuishi Dar kwa muda, nimeona samaki wengi wanaouzwa mitaani, sokoni na hata mahotelini ni aina ya Kibua na samaki wengine wadogo wadogo wa jamii hiyo...ukitaka pande la samaki mkubwa ni ghali na jamii ya chini haiwezi kumudu. Nataka kuanzisha biashara ya kulangua Sato na Sangara kwa bei nafuu kutoka Mwanza maana ndio nyumbani, hivyo chocho zote za ziwa Victoria nazijua.

Swali ni je, unadhani ntapata soko? tageti yangu ni wale walaji wa chini.
 
Soko lipo, ingawa ni vigumu kumbadilisha mtu wa mwanza kula kibua wakati alishazoea kula sangara nadhani itakuchukua muda kupata wateja cha kukushauri tengeneza posters ambazo zitakurahisishia wewe kupata wateja kiwepesi yaani ukitangaza kwa beni nafuu Zaidi ya zile walizozizoea huko dar.
 
habari wapendwa...naomba kujuzwa..
*mtaji unaoweza kuanzia kwenye biashara ya kuuza samaki(kuwaweka kwenye butcher)
*namna ya kuwatunza katika usafirishaji
*changamoto za hiyo biashara
*uendeshaji mzima wa biashara
*vitu vya kuzingatia wakat unapoaza hiyo biashara..mfano eneo
..soko lilivyo la biashara hiyo..
..na vitu vingne muhimu kama nimesahau kuvitaja..natarijia kufanya hii biashara kuwatoa mkoani ..Nyasa kuwaleta dar!!..
shukran
 
Ukipata hizo habari nitafute nikuunganishe kupata samaki mimi nachukua mwanza napeleka dar
 
Unga wa mifupa ya samaki (mapaki) unatumika kama chakula cha mifugo kuku,nguruwe ...... nchek kwa namba hii 0762655938
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…