Biashara ya stationery ya mtaji mdogo iliyoongezewa thamani

Biashara ya stationery ya mtaji mdogo iliyoongezewa thamani

Wakuu naomba mawazo yenu.

Nina mpango wa kuanzisha stationery ya mtaji mdogo around mil 5 yani umo kila kitu mpaka fremu.

Naomba ushauri zaidi ya kuprint na kutoa copy pamoja na vifaa kama bahasha, rimu, kalamu, etc

Naweza vipi kuongeza thamani kwenye stationery kwa gharama ndogo lakini niwe na vitu vinavyoingiza buku buku kila siku?

Mie nimewaza huduma kama kutafutia watu TIN, kusaidia mifumo kama nest, heslb, loss report, kuomba vyuo na scholarship, kupiga passport size,

Vipi unaweza nishauri vitu vya ziads navyoweza kufanya bila gharama kubwa ila nikaongeza thamani?

Pia mimi nipo Dar mbezi ya kimara, ni location gani nzuri kwa hii biashara maeneo ya huku au ata Dar sehemu nyingine naweza kufika na kufanya research yangu.

Asanteni
Ilove this business
 
Weka huduma ya internet (WiFi). Ambapo mwenye uhitaji anakja na kifaa chake anakulipa, iwe ni simu au pc, unamunga.
  • Buku kwa saa moja.
  • Itakulipa sana
Anakuja mwanaccm mmoja na litisheti lake kupakua video za pilau, hilo bundle la buku kwa saa itamlipa kweli ?
 
Mpango wako wa kuanzisha stationery unaonekana kuwa mzuri na umejumuisha huduma muhimu ambazo zinaweza kuvutia wateja. Ili kuongeza thamani kwa gharama ndogo, unaweza kuzingatia mambo yafuatayo:
  1. Huduma za Kucharaza Barua na CV: Toa huduma ya kuandika na kuchapisha barua za kikazi, CV, na wasifu wa kitaalamu (resume) kwa watu wanaotafuta kazi au fursa za masomo.
  2. Huduma za Kutoa Viapolo/Notarization: Kwa gharama ya chini, unaweza kuingia kwenye ushirikiano na wakili au mthibitishaji ili wateja wawezeshwe kuthibitisha nyaraka zao kwenye stationery yako.
  3. Kuweka Kioski cha Intaneti: Weka kompyuta chache kwa ajili ya wateja kutumia intaneti kwa shughuli kama kuomba kazi, vyuo, au kufanya utafiti mdogo. au pia weka router watu wa karibu na stationary yako wanaweza kutuma kwa gharama ndogo ya buku kwa siku.
  4. Kubuni na Kuchapisha Kadi za Biashara au Mabango: Toa huduma za kubuni na kuchapisha kadi za biashara, mabango madogo (brochures), na vyeti.
  5. Photocopy ya Kitabu Kikubwa (Binding Services): Ongeza huduma ya kufunga nyaraka na vitabu vikubwa vya taarifa au ripoti.
  6. Stationery ya Ubunifu: Nunua bidhaa za ubunifu kama vibandiko vya kiofisi, karatasi za rangi tofauti, na vifaa vingine vya kazi za mikono, ambavyo vinahitajika sana na wanafunzi na walimu.
Kuhusu location, unaweza kufanya utafiti maeneo yenye taasisi za elimu kama vyuo, shule, au karibu na ofisi za serikali kwani kuna watu wengi wanaohitaji huduma za stationery. Mbezi Kimara ni eneo zuri, lakini pia unaweza kuangalia maeneo yenye msongamano wa watu kama Kariakoo au Sinza.
Ukifanikisha kuongeza huduma hizi, unaweza kuvutia wateja wengi zaidi na kuongeza mapato kila siku.
aongezee na kufanyiwa wavyuo research reports zao, awe vizuri kwenye internet surfing na kutumia mifumo mbali ya internet.
 
hilo bundle la buku kwa saa itamlipa kweli ?
Kimsingi wanao fanya download za movie ndio walengwa hasa.

Kwa sasa ISP karibia wote wana Unlimited internet package amabapo unalipia speed, yaweza kuwa 10mbps, 20mps na zaidi, na utafanya download kwa kadri ya uhitaji wako. malipo ni fixed kwa mwezi.

Hivyo mteja hata kama atahitaji afanye downoad ya 100GB ni yeye tu na muda wake, haimuthiri mtoa huduma.
 
All the best...La muhimu lingine unakuwa unapitia stationary za wengine unajionea baadhi ya mambo na unajifunza
 
Kimsingi wanao fanya download za movie ndio walengwa hasa.

Kwa sasa ISP karibia wote wana Unlimited internet package amabapo unalipia speed, yaweza kuwa 10mbps, 20mps na zaidi, na utafanya download kwa kadri ya uhitaji wako. malipo ni fixed kwa mwezi.

Hivyo mteja hata kama atahitaji afanye downoad ya 100GB ni yeye tu na muda wake, haimuthiri mtoa huduma.
Hapo sawa.
 
Weka huduma ya internet (WiFi). Ambapo mwenye uhitaji anakja na kifaa chake anakulipa, iwe ni simu au pc, unamunga.
  • Buku kwa saa moja.
  • Itakulipa sana
Mkuu unaweza kunipa Mwanga jinsi inavyofanyika.
 
Ooh kumbe sikuwa nafahamu ili

Usisahau na huduma hiz hapa

1. mpesa, airtel na Yas.. hata ukianza na mtaji wa laki 5 sio Mbaya

2. Ka fridge kadogo ka kuuza maji na soda, ila hii utaangalia na mazingira ya eneo kama Hayajabana sana

3. Huduma za passport size. Siku hiz kuna vi dijital printer bei rahs tu .. weka vitambaa vyako (cha blue na cheupe)
Camera yako Na printer basi inatosha
 
Hii ndio biashara nayoiwaza kwa sasa insha'Allah nitaifanya na I will be successful through this business.
 
Usisahau na huduma hiz hapa

1. mpesa, airtel na Yas.. hata ukianza na mtaji wa laki 5 sio Mbaya

2. Ka fridge kadogo ka kuuza maji na soda, ila hii utaangalia na mazingira ya eneo kama Hayajabana sana

3. Huduma za passport size. Siku hiz kuna vi dijital printer bei rahs tu .. weka vitambaa vyako (cha blue na cheupe)
Camera yako Na printer basi inatosha
Hiyo 3 camera ya passport size inauzwa sh ngapi na wapi zapatikana?
 
Back
Top Bottom