Biashara ya Sungura imejaa utapeli wa hali ya juu sana

Mkuu Haaa angalia usije ingizwa Mkenge, Hao unao wafuatilia wangekuwa wanafaidika nao huo mkojo wangefanya kimya kimya. Nani ahangaike na Mkojo wakati kuna Organi fertilizer Madukani tena quality?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huu mkojo hata maduka ya kilimo hai unauzwa sana kwasasa. Wataalamu wangu wa kilimo hai wamenishauri niutumie na umeleta mbadiliko ya haraka sana shambani. Usiwe na hofu fuatilia mtandaoni utaujua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa yangu aliuziwa sungura sita wa mbegu kwa jumla ya shilingi milioni moja na laki nane (1,800,000). Ni kama sungura mmoja ni shilingi laki tatu (300,000).
[emoji33][emoji33][emoji33][emoji33]wakati mda huo sisi kwetu kijijin sungura mdogo, unampata kwa buku jero, na mkubwa kwa buku3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi ni risk taker tuache

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao mende ndio wanyama gani, ama ndio hawa hawa wa chooni???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umefanya utafiti ukagundua siyo dili? Naona hii thread imejaa post zenye negativity na hisia hisia tu. Ni kweli makampuni ya Kenya yalikuja kuamsha ufugaji wa sungura kisha yakapotea. Kwa mtu mwenye "mentality" ya kijasiriamali badala ya kubaki kulia lia kuhusu soko atakomaa alitengeze la kwake.

Naona majukwaa ya ujasiriamali hapa JF siku hizi yametawaliwa na comments kutoka kwa watu ambao ni dhahili kuwa hakuna kitu cha "uzalishaji" wamewahi kamilisha.

Mfano ni hii post ambayo mtumaji anadai mkojo wa sungura siyo dili. Very stupid. Mimi nafanya bustani na hutumia mkojo wa sungura kutoka kwa jirani yangu kama dawa ya kuua wadudu na mbolea simultaneously. Sasa unajiuliza, huyo anayedai siyo dili amefanya jitihada gani kuli-trap soko la wakulima?

Tatizo la mfumo wetu wa kubadilishana maarifa (elimu) haujikiti kwenye masuala (masomo) yanayotuzunguka kama vile ujasiriamali. Badala yake hutumia muda mwingi kukaririshana mambo ambayo yangekuwa ya ziada tu.

Matokeo yake ni waTz wengi kutokuwa na haiba za kijasiriamali kama wenzetu waKenya.
Pia wanawadanganya mkojo wa Sungura deal!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa kiongozi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakwere wana msemo wao kwamba jambo la kuambiwa changanya na za kwako!!
Umeongea maneno ya msingi sana mkuu binafsi nakuunga mkono. Wengi wamejawa na mawazo potof dhid ya sungura. Ndio maana wanaongea visivyo na ushahid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nipe namba yake pm mimi ni mlaji sana wa nyama ya sungura na njiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awale nyama.. mwaka mzima kila siku mboga sungura😂😂
 
Unachanganya vip kiongozi, na je unapiga kwenye mimea baada ya muda gani

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Kwenye maharage.. Kwa wiki Mara moja
2. Kwenye miti ya matunda... Kwa mwezi Mara moja.

Lita 1 ya mkojo kwa Lita 3 mpaka 5 za maji.

Kama ni dawa 1:3 mkojo:maji
Kama mbolea 1:5 mkojo:maji

Inategemea na kipindi.

Kama kipindi cha wadudu wengi ndio 1:3 ili harufu ya mkojo (ammonia) inuke shambani ili wadudu wakimbie.

Ila kwa kua nishapiga sanaa then nimestick na ratio ya 1:5

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee unafuga sungura pori!
 

Watanzania tupimwe kama tu wazima, hao ni wafanya biashara wa:

- sungura wa mengi!
- Mabanda ya sungura
- chakula cha sungura

Kama pangekuwa na Soko la sungura, wana utalaam, wana mbegu na mabanda, Kwa ninj wao wasiwakuze wauze? Kutapeliwa kwingine kwa kweli ni aibu, tuwe na akili eti!
 
haha asantee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…