floow
JF-Expert Member
- Mar 20, 2017
- 411
- 855
Huu ni mwezi wa pili tangu nimefungua biashara yangu ya Tigopesa. Niliamua kusimamia mwenyewe kwa muda wa siku 20 ili kuzijua changamoto ndogo ndogo. Hatimaye nimempata mtu wa kusimamia (kumuajiri) na ameanza rasmi kazi tar 04/05. Nimekuwa na desturi ya kumtembelea majira ya usiku anavyofunga ofisi na huwa nafanya naye hesabu na ikiwa sahihi namruhusu aende.
Leo tar 06/5 nikiwa nafanya naye hesabu nimegunduaTsh 127,950/= haionekani. Imekuwa hasara ikiwa mtu niliyemuweka ana siku tatu tu. Naanza kuona pesa yangu itapotea bure.
Niinusuru vipi pesa yangu? Nimeanza kufikiri niuze laini zote na pamoja na banda halafu pesa itakayopatikana niongeze na mtaji uliobaki nikanunue mpunga Mbeya kwani msimu wa mavuno unakaribia.
Vipi mtazamo wenu wakuu? Niendelee kukomaa na hii biashara au niikatae mapema kabla haijanifilisi?
Ikumbukwe siku 20 nilizokaa pale nilisababisha hasara ya Tsh 157,000/= mpaka nikaanza kufikiri Chuma ulete