Biashara ya Tigopesa inanifilisi

Biashara ya Tigopesa inanifilisi

floow

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Posts
411
Reaction score
855
Huu ni mwezi wa pili tangu nimefungua biashara yangu ya Tigopesa. Niliamua kusimamia mwenyewe kwa muda wa siku 20 ili kuzijua changamoto ndogo ndogo. Hatimaye nimempata mtu wa kusimamia (kumuajiri) na ameanza rasmi kazi tar 04/05. Nimekuwa na desturi ya kumtembelea majira ya usiku anavyofunga ofisi na huwa nafanya naye hesabu na ikiwa sahihi namruhusu aende.

Leo tar 06/5 nikiwa nafanya naye hesabu nimegunduaTsh 127,950/= haionekani. Imekuwa hasara ikiwa mtu niliyemuweka ana siku tatu tu. Naanza kuona pesa yangu itapotea bure.

Niinusuru vipi pesa yangu? Nimeanza kufikiri niuze laini zote na pamoja na banda halafu pesa itakayopatikana niongeze na mtaji uliobaki nikanunue mpunga Mbeya kwani msimu wa mavuno unakaribia.

Vipi mtazamo wenu wakuu? Niendelee kukomaa na hii biashara au niikatae mapema kabla haijanifilisi?

Ikumbukwe siku 20 nilizokaa pale nilisababisha hasara ya Tsh 157,000/= mpaka nikaanza kufikiri Chuma ulete
 
Haujahisi sehemu yoyote inayopelekea hiyo hasara?
 
Pole sana! Hapo tatizo unaweza kuwa ni wewe mwenyewe huenda unafanya hiyo biashara, lakini huna ujuzi nayo yani ndio kwanza unaanza kujifunza na changamoto zake zinakupiga chenga kama za Lionel Messi kwa maana hujui faida na hasara kwenye biashara hiyo zinatokea kwa sababu gani. Wakati mwingine tatizo linaweza kuwa kwa mtu unayemuajiri, au eneo unalofanyia biashara huenda kuna michezo hatari ya kishirikina japo wengi hatuamini katika ushirikina, lakini haya mambo yapo na wapo yanaowakuta. Nakushauri hama hilo eneo unalofanyia biashara, tafuta eneo lingine, tafuta mtu makini na muaminifu halafu ujaribu kuona kama utapata tena hasara - ikitokea umepata hasara kama unayoipata sasa hivi basi achana na hiyo biashara.
 
Asanta mkuu
 
Dawa siyo kukimbia tatizo, jifunze kukabiliana
 
Wengi tunaamini kuna ushirikina lakini hatutegemei waganga. Tukifungua biashara asubuhi tunaanza kumkaribisha Roho Mtakatifu na tukifunga tunamshukuru Mungu baba kwa rizki aliyoileta.
 
Huu ni mwezi wa pili tangu nimefungua biashara yangu ya Tigopesa. Niliamua kusimamia mwenyewe kwa muda wa siku 20 ili kuzijua changamoto ndogo ndogo. Hatimaye nimempata mtu wa kusimamia (kumuajiri) na ameanza rasmi kazi tar 04/05. Nimekuwa na desturi ya kumtembelea majira ya usiku anavyofunga ofisi na huwa nafanya naye hesabu na ikiwa sahihi namruhusu aende.

Leo tar 06/5 nikiwa nafanya naye hesabu nimegunduaTsh 127,950/= haionekani. Imekuwa hasara ikiwa mtu niliyemuweka ana siku tatu tu. Naanza kuona pesa yangu itapotea bure.

Niinusuru vipi pesa yangu? Nimeanza kufikiri niuze laini zote na pamoja na banda halafu pesa itakayopatikana niongeze na mtaji uliobaki nikanunue mpunga Mbeya kwani msimu wa mavuno unakaribia.

Vipi mtazamo wenu wakuu? Niendelee kukomaa na hii biashara au niikatae mapema kabla haijanifilisi?

Ikumbukwe siku 20 nilizokaa pale nilisababisha hasara ya Tsh 157,000/= mpaka nikaanza kufikiri Chuma ulete
Mkuu hiyo biashara inahitaji umakinii mkubwa. Wewe uliumizwa sababu hukuwa na uzoefu nayo. Na huyo uliye muweka naye hana uzoefu nayo. Cha muhimu ni kumwambia aongeze umakini zaidi. Kumbuka kwenye hii biashara ukikosea ukatuma 20000/= badala ya 2000/= ni hasara tayari. Sasa akikosea miamala kama hiyo mitatu kwa siku ? Kikubwa ni umakini Mkuu. Na kwa kuwa ni mgeni kama umeweka hela nyingi ipunguze kwanza mpaka atakapo pata uzoefu kidogo ndio uongezee. Ni ushauri tu lakini.
 
Upo mkoa gani, nahitaji laini ya tigo na voda pesa. Mimi nipo Arusha
 
Mkuu hiyo biashara inahitaji umakinii mkubwa. Wewe uliumizwa sababu hukuwa na uzoefu nayo. Na huyo uliye muweka naye hana uzoefu nayo. Cha muhimu ni kumwambia aongeze umakini zaidi. Kumbuka kwenye hii biashara ukikosea ukatuma 20000/= badala ya 2000/= ni hasara tayari. Sasa akikosea miamala kama hiyo mitatu kwa siku ? Kikubwa ni umakini Mkuu. Na kwa kuwa ni mgeni kama umeweka hela nyingi ipunguze kwanza mpaka atakapo pata uzoefu kidogo ndio uongezee. Ni ushauri tu lakini.
Shukrani mkuu
 
Mkuu nimeambiwa nisikate tamaa
[emoji1] [emoji1] ok,, vizuri. Ongeza umakini tu hiyo biashara ni nzuri, ukijitanua soko lake ni uhakika, haina msimu wala stress kama biashara zingine.
 
Back
Top Bottom