Biashara ya fedha ni ngumu kiasi hasa mwanzoni lakini baada ya muda ukitulia vizuri hupotezi fedha kirahisi na utaifurahia mno tatizo ni pale utakapokuwa umekosa umakini kwa mfano
1 wanakuja wateja wengi kwa wakati mmoja unajidai kuwahudumia wote kwa pupa lazima upoteze hela tu kama ukikuta wengine ni wajanja na wana tabia ya kuiba maana watakuchanganya na lazima uingie mkenge kwa hivyo epuka kukimbizwa na wateja wako yaani fuata taratibu za kifedha yaani utulivu ili umhudumie kila mtu kwa utaratibu unaofaa nawe hutoiona hasara labda upate hasara ya sh 1,10 na ikizidi 500 kwa mwezi.
2 Epuka sana kuwapatia watu wengine biashara hii hadi uwe na uhakika kuwa no way watakuangusha, lakini mara nyingi hakikisha ni mkeo au wewe mwenyewe hapo mtafanikiwa kwa kuwa biashara ya fedha ina ushawishi mkubwa mno wa mtu kudokoa, imagine mtu anaishi mtaani anafukuzwa kodi unadhani atakubali kufukuzwa kizembe si heri alipe then anakwambia imepotea na kwa kuwa nawe ulipoteza si utaunga mkono tu? Ndiyo maana unashauriwa uwe wewe mwenyewe au la mkeo au ndugu yako wa karibu mno.
3 Mtu yeyote haruhusiwi kuingia katika jengo la biashara hii yaani usijaribu kumwamini mtu katika biashara hii cos mahesabu yake mara nyingi ni jioni sasa ukijisahau mtu yeyote anaweza kuchukua pesa afu ukipiga hesabu jioni huzioni na ukikumbuka unajikuta huamini kama rafiki yako ndiye aweza kukuibia kumbe ndiye. So usiruhusu kabisa mwongiliano wa kimaeneo eneo la kazi na usikubali mtu wa nje kujua taarifa zako za siri za Tigo Pesa, au M pesa na Airtel money.
4 FANYA KAZI KWA MKATABA
Vijana wengi unawaajiri lakini hawapo makini na kazi na matokeo yake ni loss kama hizo lakini ukimpa mkataba akaweka wadhamini wake wa kuaminika nakuambia kabisa hutapata loss za hivyo na hata akipata loss itakuwa ni juu yake wala si kwako. Maana loss huja kutokana na uzembe wala si chuma ulete. Kwa hivyo chini ya mkataba mtu atajua hii ni kazi na lazima niifanye kwa moyo wote maana anajua jela i mlangoni akileta mchezo na au atawatia matatani wadhamini wake.Hivyo hata awe ndugu kama humwelewi mwelewi mpige mkataba kama hataki achana nae maana mtu anayekubali mkataba maana yake atafanya kazi kwa mujibu wa mkataba wake na hivyo anakuwa amekubali kuwajibika inapotokea hasara kama hizo. Bila mkataba utaondoka barabarani labda pona yako uwapate waaminifu by nature ndo utapona.
Baada ya hayo nikushauri hivi
Watu wote wanaofanya biashara hii wamewahi kupata loss lakini walio makini loss yao haifiki hata 2/10 ya faida wanayoipata kwa mwezi, kwa mfano mtu kapata loss ya sh 500 kwa mwezi au 1000 afu kaingiza 500000 ataachaje biashara hii? Au labda umepata loss ya sh 20 elfu ila umepata faida laki 5 kazi ni kuboresha umakini ili ile ishirini irudi yenyewe na kuingia kwenye faida yako kuliko iwe loss once more kwa hivyo nakushauri usikate tamaa kabisa ongeza umakini tu nawe utafanikiwa.
Lakini kwa ushauri zaidi nitafute kwa namba 0625911797 endapo una halotel weka namba yako nikupigie nikushauri zaidi