Usafiri wa ungo upo wa aina nyingi, upo usafiri wa ungo unaotumia wanyama, upo usafiri wa kutumia fagio, upo usafiri wa kutumia fimbo, upo usafiri wa kutumia ungo.
Wachawi wote wana roho ya uchawi, roho ya uchawi ni roho inayokufanya uweze kupita eneo ngumu na kutokeza upande wa pili, kwa mfano wachawi wanapowanga usiku roho hizi huwafanya kuingia katika nyumba yoyote na kuwafanyia uchawi usiku watu waliolala ndani ya nyumba hizo bila ya kuonekana. Isipokuwa nyumba za walokole haziingiliki kabisa.
Roho za uchawi zinawawezesha wachawi kujibadilisha maumbo yao, kutoka maumbo ya kibinadamu na kugeuka kuwa paka, panya, kunguru n.k.
Wanapotaka kusafiri anakuwa na vifaa vyake vya kichawi, kisha huomba dua akinuizia majini yampeleke sehemu fulani, roho yake ya uchawi na majini humuinua juu angani kwa kasi hadi eneo alilokusudia. Usafiri wa aina hii ni hatari kwani unaweza kutunguliwa kirahizi ukiwa angani.
Usafiri wa kutumia wanyama kama fisi, hutumika kwa nchi kavu tu, hawawezi kuvuka bahari kwenda visiwani au nchi za mbali.
Usafiri wa kasi sana ni wa kutumia fimbo, kabla ya kuanza safari, unaomba dua ya manuizo na kukanyanga incha moja ya fimbo, roho ya uchawi na majini hukuinua juu angani, kama unataka kwenda Nigeria kutoka Dar, utaonyeshwa njia yote ilivyo, kama kuna hatari yoyote huonekana, na inabidi uhairishe safari, kama njia ni nyeupe, unatakiwa ukanyage incha ya pili ya fimbo, na safari huanza kwa kasi ya sauti. Kwa sababu safari ni ya kasi sana na upepo ni mkali sana, kiasi kuwa huwezi kufika ukiwa hai, majini huchomoa roho yako ndani ya mwili wako na roho kukutangulia mbele, mwili wako huikimbiza roho yako ukiwa katika hali ya umauti, unaweza kutumia sekunde 10 kufika Nigeria, lakini ni usafiri wa hatari kuliko zingine, usafiri huu hujulikana kama usafiri wa kujichinja.
Wachawi wa Marekani na bara Ulaya wao hutumia sana usafiri wa fagio.