ZAZUNI Lango la kuzimu la Bagamoyo
Mji wa Bagamoyo ni mji wa kizamani uliokaliwa na Waarabu, na maendeleo yake yalikuwa duni sana hadi siku za hivi karibuni, wageni walipoanza kuingia na kuwekeza katika mji huo.
Lango la kuzimu la Zazuni liko ufukweni mwa bahari ya Hindi, likihudumiwa na majini kumi na mawili.
1. Ruyat ni jini linalosimamia ndoto mbaya
2. Al-Rahab ni jini linalosimamia shoti ya umeme na majanga ya moto, mfano wa majanga ya moto yaliyotokea katika mabweni ya kulala wanafunzi katika shule nyingi, jini hili lilihusika na kuwachukua watoto kuwapeleka msukuleni. Watoto hawa wote wapo hai, tangu vita hivi vya shetani vilipoanza mkoani Kilimanjaro katika shule ya wasichana ya Shauri Tanga, watoto hawa wanaishi katika mateso makubwa makubwa ajabu.
3. Hadarash ni jini katili sana linaloua kwa kukata shingo na kunyonya damu ya mtu
4. Anazihad ni jini linalokamata roho ya mtu, kisha mtu anaonekana amekufa, baada ya mazishi, wachawi huja na kusoma dua kaburi funguka na jini huiachia roho ya marehemu, ufahamu unapomrudia, wachawi huondoka naye.
5. Zuzuk ni jini la maafa. Jini hili likiingia mtaani au kijijini, hutokea vifo vingi sana, kila siku watu wanazika.
6. Munkar ni jini la makaburini. Jini hili linakutokea kwenye ndoto kama babu, bibi au mzazi wako waliokufa zamani, likiwataka mfanye jambo fulani au familia itaangamia. Kimsingi unapotekeleza maelekezo ya jini, mtakuwa mumejifunga wenyewe kwa kamba ya kifo toka kuzimu, na matatizo makubwa ya magonjwa na vifo huanza kwa familia.
7. Tatazu ni jini la uasherati, unafanya tendo la ndoa bila kujali magonjwa au uko kwenye kipindi cha hedhi.
8. Rabdi ni jini linalotumwa kwa Waislamu peke yake, kwa ajili ya kufanya fujo.
9. Balshebe ni jini linalosimamia magonjwa na madhaifu ya mwili
10. Sajidur ni jini linalosimamia pesa. Likitumwa kwako mshahara wako unapotea katika matumizi ya ajabu ajabu.
11. Subrah ni jini linalosimamia mafarakano, na kutokuelewana kwa viongozi wa Makanisa.
12. Lair Labi ni jini linalosimamia hofu na kukata tamaa.