Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 42,023
- 12,811
Uchawi ni kazi inayofanyika kwa usiri mkubwa sana, endapo mchawi atatoa siri za wachawi wenzake adhabu yake huwa ni kifo. Ni vigumu sana kumtambua mchawi, licha ya baadhi ya makabila kuwashuku akina mama wazee wenye macho mekundu kuwa ndio wachawi, lakini ukweli siyo wachawi. Madhalani mkeo/mumeo anaweza akawa mchawi wa kutupwa lakini usiweze kumtambua kabisa.
Kawaida matayarisho ya kwenda kuwanga huanza jioni ya saa kumi na mbili hadi saa mbili usiku, kwa kuchoma ubani na kuomba dua, wachawi wanayo roho ya uchawi ndani yao, ambayo ikifika saa sita usiku, hiyo roho ya uchawi iliyo ndani yake humwamsha. Wachawi wanakuwa na madhabahu zao za kukutanikia usiku, kwa mfano wachawi wa Kariakoo wanayo madhabahu yao, wachawi wa Masaki wanayo madhabahu yao, Wachawi wa Mwananyamala madhabahu yao iko ndani ya hospitali ya Mwananyamala, ndiyo maana vitimbi ndani ya hospitali hiyo haviwezi kwisha bila ya kuivunja na kuisambaratisha hiyo madhabahu.
Mchawi anapoamka usiku wa manane huenda kwenye madhabahu yao, na kila madhabahu ina mwenyekiti na katibu wa kuandika taarifa za kikao. Kazi ya kikao ni kupokea mashitaka kutoka kwa wajumbe, kuyajadili na kuyafanyia maamuzi. Kwa mfano, mchawi anaweza kuleta shitaka kuwa jirani yake XYZ kila siku wanakaanga nyama na samaki, watoto wake wanasoma shule nzuri, na wanaringa sana. Hilo ni shitaka tosha la kujadiliwa kwenye madhabahu za wachawi.
Wachawi wakimaliza kumjadili ndungu XYZ, wanapanga adhabu ya kumwadabisha, adhabu inaweza kuwa, wamtupie mume jini afukuzwe kazi, au wampindishe mama miguu asiweze kutembea. Wakishachagua adhabu, huteua kamati ya utekelezaji ambayo, itahakikisha familia hiyo inaadhibiwa haraka iwezekanavyo. Idadi ya wajumbe inategemea ukubwa wa kazi, lakini mara nyingi huwa ni wachawi kati ya watatu hadi sita.
Wachawi huanza kazi ya ulozi nyumbani kwako, kwa kawaida muda wa kufanya ulozi ni kuanzia saa sita usiku hadi saa tisa usiku, kama siku hiyo hawakufanikiwa kuingia hadi saa tisa usiku, shughuli huairishwa hadi siku inayofuata, roho ya uchawi waliyo nayo huwafanya wachawi kupenya kwenye ukuta, kwa kupitia kwenye kona ya chumba. Wachawi wakikuta mtuhumiwa ni mcha Mungu mzuri huwa wanashindwa kumkaribia kwani mwili wake huwa unawaka moto, wakikuta familia yote haishikiki, basi kikao hungeuza adhabu kwenda kwa mfanyakazi wa ndani, biashara yako, au kwa ndungu zako wa karibu.
Wachawi wakikuta familia iko tupu, kazi ya ulozi huwa ni nyepesi sana, na matokeo yake huonekana mapema.
Kumbe ndio huwa wanaturoga namna hiyo.......kweli inabidi kumrudia Mungu.