Biashara ya Uchawi Tanzania

Biashara ya Uchawi Tanzania

maisha magumu?? kivipi??

mbona sioni uhusiano wa ugumu wa maisha unanvyo link na biashara?

mkuu labda utuambie tu ni ukosefu wa elimu hasa ya biashara ndio huwafanya wafanyabiashara kuingiza ndumba katika business!!

hebu toa mfano kwa watu kama bill gates, reginald mengi, said bakhresa, dangote, mike sonko na eto'o. je hawa wanatumia ushirikina??

je unaweza kunipa listi ya wafanyabiashara Tanzania waliofanikiwa sana sababu ya ushirikina?

huwezi kujua kama wanatumia kwani haya mambo hufanyika sirini,hawatangazi.Mind you ushirikina uko na aina nyingi na level tofauti kutegemeana na mahali ulipo,social status,kipato n.k
 
Naruhusu mchawi yeyote achakachue username yangu anipe jina mimi ni nani na niko wapi.
Sio tunakaa tunakamatana hapa, uchawi upo ila yupo moja ambaye yuko juu ya wote, maana yeye ndiye mwanzilishi wa vyote, na ndiye mwisho. Mchawi atabaki kutumia majini tu kufanya kazi yake ila yule anatazama ulimwengu mzima kwa wakati moja na lolote analolifikiria linakua papo hapo.. Sasa chakachua kwa uchawi wote uniambie mimi ni nani na niko wapi
 
ukitakd uchawi utafanikiwa,ukitmia elim pia utafanikiwa tena mafnikio yakudum sikama ya uchawi yanakoma.Mtegemee mungu
 
Mkuu hizo bado ni hadithi za kusadikika...., Mfano mimi siku nikiona kitu ambacho si cha kawaida takwenda hospitali wakanipime akili, labda nineanza kuchanganyikiwa na ninaona vitu ambavyo havipo unless jambo moja tuone wengi kwa wakati mmoja, na hapo tasema tumepigwa changa la macho.

Sasa since hapa tunaongelea facts na wewe upo hapa.., naomba tuanze kuongelea hili suala la kupaa kwa ungo..., je ni force gani inayofanya mtu apae na ungo au ni michanganuo ipi unafanya ili upae...., sababu ndugu yangu bila kuleta facts hapa kutakua hakuna tofauti na hadithi za alfu lela olela

Wewe na wenzio mnaopinga dhana ya uchawi, yawezekana mnapinga ili kuonekana mnapinga au basi kuna jambo jingine mnatafuta.

Mimi dini yangu imeandika kwa kuutambua uchawi tangia enzi hizo za wana wa Israel kutolewa misri, tunajulishw kwamba farao alikuwa kaidi asiyetaka kuwaachia wana wa Israel na kwamba katika kushinda na Musa (aliwaita wachawi wake )ili watengeneze fimbo za kugeuka nyoka kama alivyokuwa amefanya Musa kwa uweza wa Mungu.

Kwa imani hii uchawi upo na wazungu ndio wako mstari wa mbele kuu practice, anayesema wasomi hawaamini uchawi ni muongo na kweli haimo ndani yake kabisa!
 
The only principle of real success is 1. Working-hard, 2.Proper time management, and 3. Strong faith to GOD. If u want artificial success through Satanic ways u will get it, but it doesn't exist for a long time and it is accompanied by very difficult terms & conditions like sacrification of human beings and likes.{Shida tunataka mafanikio yasiyo na calculations huo ndo udhaifu wetu japo hatutakiwi kuukubali, mbona ukiwa na imani kuu kwa MUNGU aliye hai utapata kila utakachoitaji...!!}. Watanzania walio wengi hawapendi complications cjui nani aliwadanganya kuwa mafanikio yanakuja kiurahisi kiivo...! wakati hata bibilia iko wazi kuwa "Tangu enzi za Yohana mbatizaji hadi sasa ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu nao wenye nguvu wauteka, (Ref: Mathayo 11:12...)" sasa wewe unataka ufanikiwe kiurahisi rahisi tu uku hautaki kuchakalika....? Hii mbinu ya kuamini kuwa hakuna mafanikio pasipo shortcuts inalimaliza taifa letu, Real! fuatilia kila anayeingia kwenye mchakato wa utafutaji utakuta mchawi, fisadi au antoa rushwa ya ngono kwa wanawake yaani hadi vyuoni watu wanahonga apewe GPA kubwa huyu mtu asiyependa kujishughulisha ila anapenda kupokea unafikiri akipewa wazifa atafanya nini kama sio ufisadi au kupiga lamli.....! Tujitahidi kuelimishana tu maana mafanikio ya kichawi hayadumu utakula ww peke yako wanao, wajukuu zako watakuwa maskini km kawa labda nao wawe wachawi pia na wote mtaishia kwenda kuzimu....!! TAKE CARE, MTANYWEKA..!!
 
teh....wakina mama wa nyumbani....hapo ndo penye...ukitoka tuu ,,, nao kiguu na njia.
 
Wanafunzi wa la tisa wanafanya nini kwa wachawi? Aka waganga!
 
Walikutana wakiwa wanafunzi kwenye chuo cha uchawi kilichopo Saudi Arabia, Mtanzania alianza kumfundisha jinsi ya kuruka kwa ungo kwa mwendo wa haraka, mazoezi yalikuwa yakianzia Saudia hadi Kigoma. Kwenye mkutano wa wachawi wa dunia uliofanyika kwenye lango la kuzimu la Mustallah Upanga mwaka 1999, Osama alihudhuria, wengine waliokuwepo ni Khomeini wa Iran, Ghadafi, Mfalme Abdullah, Yasser Arafat na viongozi wengi wa nchi za Kiarabu.

Wewe unamjua Arafat? Na huyo wa Kigoma nasikia ni mm ni kweli?
 
Jamani huyu member aitwaye Asa'rile amepatwa na maswahibu gani make last activity yake inaonesha September 2013...

Tumemkosa sana...
 
Last edited by a moderator:
Wafanya biashara wa maduka ya rejareja, akija mama/baba na chupa iliyofungwa, akakupatia umpimie mafuta ya kula, usiifungue hiyo chupa, mrudishie huyo mama/baba aifungue yeye mwenyewe. Ukimrudishia hiyo chupa kama ni salama ataifungua, la sivyo atalalamika sana, mara hoo vijana wa siku hizi heshima hawana, mara hili na lile, ukweli ni kuwa hawezi kabisa kuifungua hiyo chupa, akianza kulalamika atakuwa anaondoka akisema maduka yapo mengi unafikiri ni wewe peke yako tu mwenye duka. Kumbuka siyo aina yoyote ya chupa, lazima iwe chupa ya kioo yenye mfuniko wa kujizungusha kama chupa zinazowekwa pombe kali.

Chupa za plastiki hizo hazina matatizo. Wachawi wa nchi wanatumia uchawi wao kupata pesa kwa njia za wizi, aina hii ya wizi wa kutumia majini huitwa chuma ulete. Majini haya huyatengeneza wao wenyewe, zipo aina ya majani na vitu vingi huchanganya pamoja na damu ya mnyama, huo mchanganyiko ukifikia hali fulani husomwa dua mbalimbali na machangiko huo hupatiwa jina kama Jumatatu, na kila siku mchawi anaita jina hilo mara tatu au nne akiwa karibu na huo mchanganyiko.

Baadaye hutumika aina mbalimbali za ubani na dua na ule mchanganyiko huwa ni pepo kamili, pepo hilo huingizwa ndani ya chupa kama moshi, ambao siyo rahisi kuona. Anapokupa hiyo chupa kuifungua, kawaida unapofungua chupa, unaiweka mbele karibu na uso wako, hivyo ule moshi ulio ndani ya chupa hutoka na kuingia ndani ya mwili wako.

Jumatatu akishaingia ndani ya mwili wako, mchawi akitaka kitu chochote dukani kwako atakichukua kirahisi sana. Anachofanya akifika dukani anaita tu jina la Jumatatu, lile pepo aliloliweka ndani yako huitika na kupanda, pepo likipanda wewe mwenye duka fahamu zinakutoka, analiangiza sasa nipimie mchele kilo 4, sukari kilo 1, unga kilo 5 akishapimiwa huondoka, na wewe mwenye duka huzinduka bila kujua chochote kilichofanyika, mara nyingine anaweza kuja na kuita Jumatatu nipe shilingi alfu ishirini, Jumatatu hupanda na kumpatia hizo pesa.

Hilo pepo linapanda linapoitwa na mchawi aliyelitengeneza peke yake, akija mtu mwingine na kuita Jumatatu pepo hilo halipandi kwani halimtambui.

Mama Porojo. Ahsante kwa taarifa,Swali langu ni dogo tu;Hivi hata madalali/matapeli nao ni wachawi?
 
Back
Top Bottom