Biashara ya ukopeshaji pesa kwa riba

Kwanza hii biashara hutakiwi kuwa na roho ya huruma Nina dada angu anaifanya mwaka wa nane na ndio biashara inayomuweka mjini

Anakopesha kuanzia 10000 mwisho laki tatu. Riba anafanya asilimia 50 ndani ya mwezi mmoja. Anayekopesha lazima aweke kitu na hicho kitu analetewa sio abaki nacho mkopaji , vitu anavyopokea vifaa vya umeme mfano TV, radio , pasi nk.

Vito vya thamani dhahabu , silver , tanzanite nk kabla ya kumpa mteja pesa anaenda kuvipima kujua thamani yake ana sonara yake maalum.

Hapokei kiwanja Wala hati ya nyumba, anayeleta pikipiki au gari anaacha na kadi.

Anavyokopesha mfano mtu akiwa shida na laki , anatakiwa aweke vitu vyenye thamani ya laki na nusu pamoja anajumlishia na thamani ya riba. Anamletea ikifika muda wa malipo asipoliopa anaweza akamletea faida 50000 Deni Lina baki palepale, mkopaji akikaa kimya mfano miezi miwili anampigia simu muhsika kumuuliza vp akiwa Hana jibu anamwambia tumemalizana Basi vitu vyako nauza Mimi na wewe tumemalizana.

Unakuta mtu labda kamuachia flat screen nch 32 kapewa laki moja so hata akiuza laki nanusu yeye faida yake ipo

Kikubwa uwe makini na vitu wanavyoleta wateja ni biashara nzuri ila yahitaji umakini wa Hali ya juu.
 
ana lesen au anafanya locally?

Sent from my SM-J320F using Tapatalk
 
naona yy anafanya vzur kushika mali asee mm pesa yangu ndefu imepotea kwny hii bussness mana wadaiwa wamekausha kama hawana deni vile na huez wapeleka polis coz huna lesen ya kukopesha.

Sent from my SM-J320F using Tapatalk
 
Ana leseni kutoka benki kuu? Kama hana basi atakuwa anafanya biashara haramu na kuna siku itam-cost sana. Kuna watu wameingia kwenye matata kwa sababu ya kufanya hii shuguli bila leseni halali. Na mara nyingi hutokea mkopeshaji atakapokutana na mkopaji jeuri na kuamua kuuza mali yake. Mkopaji akimua kwenda mbele ya sheria basi vinafumuka vitu vingine amabvyo vitabaki vinamshangaza na kumliza mkopeshaji.
 
Huyu anafanana na Zack finance.
Yeye pia hufanya.

Japo yeye riba zake ni 30%
Alinifilisi sana mwaka niliomalizia chuo nilikuwa natafuta pesa ya kwenda kulimia
Nilijikuta kila kitu nimekiweka kwake bond.

Hii njia nzuri lazima vitu vile ufight uvirudishe maana unakuta umeweka flat ya laki 6 na nusu jamaaa anakukopesha laki mbili na nusu.
 
aiseeee
Sent using Jamii Forums mobile app
 
naona yy anafanya vzur kushika mali asee mm pesa yangu ndefu imepotea kwny hii bussness mana wadaiwa wamekausha kama hawana deni vile na huez wapeleka polis coz huna lesen ya kukopesha.

Sent from my SM-J320F using Tapatalk
Mkuu anza kukopesha kwa kina mama ama ama kikundi ambao wanahitaji pesa za kudouble ama kuweka akiba ili wapewe mkopo taasisi flani.

Pale wanapopokea pesa zao na wewe huyo, Unachukua chako.

Na hii unawapa wale ambao wana uhakika ndani ya wiki mmoja pesa watakuwa wamepata.riba (30%)
 
aah kweli sio mchezoo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…