Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Raha ya biashara ni kufanya biashara halali,lakini biashara kama ya huyu bwana haina tofauti na ya wamachinga ya kiwizi wizi, kila siku utakuwa unatizama nyuma, nani ananifuata TRA, CITY, BWANA AFYA au Polisi. Watu wanasema kama hutaki kuota usilale - wewe kama ni mtu wa kutopenda matatizo ushauri wa huyo jamaa hautokufaa. Kikubwa mafanikio ya biashara yako ni kupata vifaa vizuri, mpishi mzuri,Packing inayovutia, usafi wa sehemu yako ya kufanya kazi na kuweka uangalizi mzuri maana wengi wenye bakery wanalia na wizi unaofanywa na wafanyanyakazi wa vitu kama Sukari, Unga, Mafuta na mara nyingine hata wanacheza na uzito wa mkate itoke mingi wauze inayozidi pesa wachukue wao.
 
newmzalendo naomba nisaidie namna ya kumpata huyo jamaa.
 
Last edited by a moderator:

NGOJA WAJE watuchambulie nami nidonoe
 
Piga tu kazi mkuu kuna bakery moja mitaa ya ununio jamaa amefungua pale pako very silent lakini anafanya biashara nzuri sana japo yeye mpk chapati vitumbua sambusa keki mikate na kahawa/chai take away anauza kwako wewe jitahidi kwenye products zako ziwe nzuri utapata wateja tu na kwa sinza mzungumko wa watu ni mkubwa ukipata connection ya maduka ya mwenge sinza yenyewe na kijitonyma kabla hujasambaa tandale na manzese. kazana tu kiongozi ila jitahidi kuzingatia uwepo wako uone kile kinachotakiwa upate kuyadhibiti mapungufu, jitahidi pia kuzungumza na wengine walio tayari kwenye hiyo biashara watakusaidia njia sahihi kufanikisha lengo lako.
kila la kheri kwako.
 


Ni move nzuri..ila Fanya research ya Soko. Usiwekeze mtaji ukakosa wateja. Ila jitahidi ku brand bidhaa zako. Zikiwa bora watakufuata tu. All the best
 

Kuhusu mfanyakazi mwenye uzoefu nenda bakery inayofanya vzuri kisha mchukue kwa kupandisha salary. Kimya kimya
 
mkuu short white, hvyo vifaa vimekucost sh ngap?
 
Mkuu Short White salaam,

Vipi waendeleaje na mchakato wa biashara yako ya bakery? Nimesoma thread yako kwa umakini sana na nimefurahishwa na jinsi wachangiaji walivyotoa ushauri wao mzuri sana sana. Hili jambo nami liko kichwani japo sijachukua hatua za kuanza maana majukumu yaningilia mambo.

Hakika ukifanikiwa hutajutia maana nina AUNT yake na rafiki yangu alianzisha bakery mjini hapa 2011 na sasa na supplier mkubwa na anapata vyombo sana. Ila ukiweza (imani yangu ulishaanza maana naona andiko ni la 2011) basi waweza boresha kwa kuongeza viuongo vyenye kutia ladha kama IRIKI na vile vile walau ujitahidi uweke na maziwa. Huo mkate nakuhakikishia walaji watakutafuta. Pale Kunduchi jirani na Chuo cha Kijeshi kuna jamaa kafungua pale nilifurahishwa sana na jinsi alivyojipanga. Ana-make sana yule jamaa.

Tukuombe tu utupe uzoefu na changamoto unazokumbana nazo mkuu.

Aksante
 
Hongera sana mkuu,. Hivyo vifaa vimekugharimu kiasi gani cha pesa. Na kwa gharama kwa jumla mpaka unamaliza umetenga kiasi gani?
 
yaani hakuna biashara inayolipa kama bakery hapa jirani yangu jamaa amefungua bakery na awali magari ya bakery yalikua yanagongana hapa sio chini ya manne yanasupply brands zao, tukasema huyu jamaa atapata hasara sababu hii biashara inaonekana kama ina ushindani sana lakini huwezi amini jamaa anapiga kazi mpaka usiku yaani hakuna mchana wala usiku kwake na bado hawezi kulitosheleza soko.
 
Hapo inabid utoe specification kwamba unataka vofungashio vya namna gan plastic or karatas itakuwa vizur tukianzia hapa
 
Hapa kuna vitu vichache vya kuzingatia ili ujue utatumia vifungashio gani.

Una target wateja wa aina gani na hizo bidhaa bei zako umezipangaje? Nakuuliza hivyo kwa sababu kama unatarget mabosi wao wanaexpect packaging ya kueleweka na mara nyingi hawana tatizo na bei lakini kama una target walalahoi wao wapo very price sensitive hadi haelewi thamani ya packaging. Kama una target walalahoi kuna mifuko ya khaki inauzwa kariakoo inakuwa 50 au 100 not sure, watu wengi wenye bakery wanaitumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…