Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Biashara ya upatu, ni uchangishaji fedha unaoweza kuendeshwa na mtu au kampuni kwa ahadi ya kuwapatia faida kubwa baada ya kipindi kifupi.
Baadhi ya makampuni hujificha katika kivuli cha kuuza bidhaa fulani na mara nyingi huwa bidhaa za afya. Mwanachama hutakiwa kutoa kiasi fulani cha fedha kama mtaji ili kujiunga, na baada ya kujiunga hatakiwa kutafuta watu watakao jiunga chini yake katika mfumo ya piramidi.
Baadhi ya nchi huichukulia biashara hii kuwa ni haramu na hivyo makampuni yanayojihusisha na biashara hii kubuni njia mbadala za kuficha uharamu huo, ikiwa ni pamoja na uuzaji wa bidhaa ambapo mwanachama hutozwa kiasi fulani kama ada ya kujiunga na kisha hupewa bidhaa fulani lakini akitakiwa kutafuta mwanachama wakujiunga chini yake ili aweze kupata faida.
Kutokana na kiasi kikubwa cha ada ya kujiunga wanachama wapya hukosa watu wakuwaunganisha na hivyo wanakuwa wamepoteza mitaji yao
Dalili za biashara ya upatu, Ili mtanzania uweze kutambua kuwa unawindwa na biashara hii haramu kuna mambo unayopaswa kuyachunguza na kuwa makini nayo. Kwanza, ahadi ya malipo makubwa yasiyo na kikomo baada ya kujiunga na kumuunganisha mwanachama mwingine. Kwakuwa biashara hii ningumu kuwapata wanachama, hivyo waendeshaji hushawishi kwa kukuahidi malipo makubwa ndani ya muda mfupi sio ajabu kusikia " ukileta watu wawili tayari wewe ni tajiri." Pili, watakusumbua kwa barua pepe, simu na jumbe mbalimbali kukushawishi kuhudhuria mikutano yao, na ukifika watakuwa wakisimulia mafanikio yao pekee. hizo ni baadhi ya dalili za kuwa unawindwa na biashara hii.
Vilevile biashara ya upatu (MLM marketing) inayo madhara mbalimbali kwa vijana na watanzania, kuichumi, kijamii, kisiasa kama ifuatavyo,
Mosi, husababisha umaskini; hii nikutokana na kuwa ipo ada kubwa kwaajili ya kujiunga na biashara hizi, kwaahadi ya kufanikiwa ambapo watu huweza hata kukopa fedha nyingi kwaajili ya kujiunga na mpango huu haramu na hivyo kusabaisha mitaji mingi kutoka katika mizunguko halali ya uzalishaji na kuingia katika mifumo haramu na mwisho mwanachama hataambulia kitu zaidi ya kupoteza muda na fedha, na kwawale waliokopa mikopo huishia kufilisiwa
Pili, Husababisha uhamishaji wa fedha/mitaji kwenda nje ya nchi (capital flight); Kwa kuwa makampuni mengi yanayojihusisha na biashara hii haramu ni yakimataifa husababisha mitaji mingi kutoka katika mzunguko wa nchi na kutoka nje na hivyo kusababisha upungufu mkubwaa wa fedha za kigeni.
Tatu, Uvivu; Baada ya mwanachama kujiunga huahidiwa utajiri ndani ya kipindi kifupi, vilevile atakutana na shuhuda za watu walio acha kazi kwaajili ya utajiri wa biashara hiyo na hivyo kushawishika kutowajibika kwa shughuli za kawaida za kujipatia kipato na kusababisha kuwa mzigo mzito kwa jamii na serikali.
Nne, Husababisha uadui; Mwananchama mpya anapojiunga katika biashara hii watu wakwanza atakaowafikiria kuwaunganisha niwale marafiki zake wakaribu, hivyo huanza kjuwashawishi kujiunga na kuwahidi faida kubwa na mafanikio, na ikiwa marafiki zake watatoa fedha zao na kujiunga na wsipate kile walicho ahidiwa uadui baina yao huibuka na kusababisha kutokuelewana.
Tano, huweza kusababisha uhasama kati ya wananchi na serikali; Siku zote wananchi huamini kuwa serikali ndiyo yenye dhamana ya kuthibiti mambo yasiyofaa kwenye jamii, kama vile utapeli na wizi, inapotokea wananchi wakajiunga na biashara hizi na wakapoteza fedha zao huanza kuilaumu Serikali kwakushindwa kudhibiti jambo hilo, na wakati mwingine wananchi huweza kuiondoa serikali madarakani kwa kushindwa kudhibiti biashara za upatu kama ilivyotokea katika nchi ya Albania.
Sita, husababisha wanachama ambao ni wanafunzi kufeli masomo yao; Walengwa wengi w biashara hizi za upatu ni wanafunzi wa vyuo ambao hujikuta wakipoteza muda mwingi kuhudhuria semina na mikutano kwaajili ya biashra hii haramu na mwisho hawafaidiki chochote zaidi ya kupoteza muda wa vipindi na hivyo kusababisha wao kufeli
Mwisho wananchi hasa vijana wanatakiwa kuwa makini sana ili kujiepusha na biashara hizi.

Upvote
8