Salaam kwenu nyote!
Kwa mwana JF yoyote anaefanya biashara ya Bajaji nina shida kidogo..kuna kautafiti kadogo nataka kufanya.
Nimekuwa nafanya biashara za bajaji kwa takribani miaka mitatu sasa.
Kwa sasa naona kama gharama za uendeshaji wa Biashara hii zinapanda kila kukicha, awali ulitakiwa kulipia road licence, kodi ya mapato na bima ili uweze kufanya biashara hii. But hivi sasa SUMATRA wamekuja kwa kasi ya ajabu wanatoa na wao leseni na wana taratibu ambazo ziko a bit complicated.
Nilitamani kujua wamiliki wengine wa Bajaji wanatoza hesabu ya Tsh ngapi kwa siku, (binafsi toka nimeanza natoza 15,000). Pia ni namna gani ya kukabiliana na changamooto hizi, ukiachia mbali fikra zangu zakuongeza hesabu ya siku.