Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

Kazi kweli
Jamii forum siku hizi watu hadi ushauri wanauza.
Maana Pm kibaoo bila majibu.
Akili kumkichwa

Mkuu huwa nachukia sana mtu anaomba ushauri halafu mtu anakwambia ni pm.na hawa watu wa pm wengi ni matapeli maana chemba mkafanye nini.bajaj nyingi kwa Dar ni 15 elfu hesabu maamuzi yako upewe kwa wiki au baada ya wiki 2 na ninakushauri usinunue iliyotumika nunua mpya ni biashara inayolipa ila uwe makini kuisimamia
 
Bajaji ni laana, pikipiki ni laana.

Utaishia kujuta.

1. Asilimia kubwa anapata dereva anakusanya 50000/= anakupa 20000/=

2. Ni lazima umuachie makusanyo siku mbili tatu ili aifanyie service ya uhakika, ukiwa mbishi itafanywa tambala bovu. Service mara mbili kw mwez, au moja, mbili ni bora zaid

3. Asilimia 90 Hazirejeshi bei ya manunuzi. Buni bisshars tofaut
 
bajaji ni laana, pikipiki ni laana,

utaishia kujuta.

1. Asilimia kubwa anapata dereva anakusanya 50000/= anakupa 20000/=

2. Ni lazima umuachie makusanyo siku mbili tatu ili aifanyie service ya uhakika, ukiwa mbishi itafanywa tambala bovu. Service mara mbili kw mwez, au moja, mbili ni bora zaid

3. Asilimia 90 Hazirejeshi bei ya manunuzi. Buni bisshars tofaut

Ngoja nikujibu

1. Asilimia kubwa anapata dereva anakusanya 50000/= anakupa 20000/=
Kusema kwamba asilimia kubwa anapata Dereva na kumpangia hesabu anayopata yeye wakati yeye yupo njiani na wewe upo nyumbani.

Sasa we kwa akili yako ya kijani unafikiria kwamba anachokipata yeye na kwa juhudi zake kubwa za kufanyakazi katika mazingira magum ndio mgawe sawa?

We si umesign mkataba? na mikataba yote kwa wazoefu wa Biashara na hesabu za Tajiri zinafahamika.
Hii ni sawa na Daladala,huwezi kusema eti wanachopata wafanyakazi kikubwa kuliko chako,wakati wenzio wote ndio wanavyofanya,mbona siku ya hasara hamsemi mgawe hasara pamoja.

Nakuonea huruma sana kwamba kasi ye maendelea ya dunia ya sasa katika biashara na maisha kwa ujumla imekuacha mbali sana.

2. Ni lazima umuachie makusanyo siku mbili tatu ili aifanyie service ya uhakika, ukiwa mbishi itafanywa tambala bovu. Service mara mbili kw mwez, au moja, mbili ni bora zaidi
Huu ndio ukihiyo mwingine na umbulula,we umeona wapi biashara inafanywa hivi.Hesabu inafahamika kwa wiki na kuna siku inaachwa. Na kwa kukushauri tu ni kwamba Services ya Bajaji ni miongoni mwa Services zinazotumia dakika kadhaa tu kumaliza.

3. Asilimia 90 Hazirejeshi bei ya manunuzi. Buni bisshars tofaut
Hapa ndio nimekuona kwamba umezaliwa kwa bahati mbaya na unaishi kwa makusudi. Bajaji, bodaboda zote zinarejesha pesa yake kwa asilimia 100.

Kuna mdada mmoja anazo Bodaboda 26, na alianza na mbili, na ndio ile miaka ya mwanzo zinaanza.
Lei hii akienda bank kuweka pesa ni heshima.Tena Mdada mdogo tu. Na alipohojiwa kwenye Tv anakuambia changamoto za kawaida sana kama ukijitoa.

Mzalendo. Wewe timiza ndoto zako, nunua mpe Driver upate hesabu yako na ndani ya mwaka pesa imerudi.
Na Bajaji unatumia zaidi ya mwaka mmoja. Kuchoka kwa chombo cha moto ni matunzo yako tu.

Inapotokea kasoro basi irekebishe mapema kabla haijawa kubwa.Muhim ni kutafuta sehem ambayo utamuambia Driver wako atakuwa akipeleka kwa ajili ya Service. Maana hivi ni kama Pikipiki tu,s asa baadhi ya Drivers hujifanya kufanya services kivyao na Oil hizi za mitaani zilizokuwa na kiwango duni sana.

Kila la Kheir and Stay blessed
 
Hello wakuu salaam zenu,

Kwa wale wazoefu na biashara ya bajaji naombeni mnipe mchanganuo coz kuna pesa kiasi hapa nataka kwekeza katika biashara hio, na pia ni bajaji gani ni imara kati ya boxer, piaggio, au atul??

Msaada wenu ni muhimu sana katika hili.
 
Mi pia nampango wa kuanza mwezi huu ningepata majibu la hayo maswali yangenisaidia sana.
 
Dahh biashara bomba sana kama utaendesha mwenyewe but kama ya kumkabidhi mtuu dahh majanga sana. Mi nilikiwa na yangu kipande 15 kwa siku, but dereva alikiwa anaingiza total 55000 kwa siku akitoa wese 12000, ya bosi 15 kinachobaki chake but ikizingua chochote ni lako wewe mwenyebajaji. Yako ikiwa mbovu anachakupoteza anapiga dayworker, nilikuwa na komaa mwenyewe ahhh mbona safi tu.
 
Fanya hivi ingia na mtu mkataba wa mwaka mmoja. baada ya mwaka unamwachia. Terms ni kwamba kila siku lazima alete pesa endapo ikifika week hajaleta mnamnyang'anya. Matengenezo yoyote juu yake. Kila siku anakuletea 30k. 30,000*30*12=10,800,000
 
Fanya hivi ingia na mtu mkataba wa mwaka mmoja. Baada ya mwaka unamwachia. Terms ni kwamba kila siku lazima alete pesa endapo ikifika week hajaleta mnamnyang'anya. Matengenezo yoyote juu yake. Kila siku anakuletea 30k. 30,000*30*12=10,800,000

- Itaharibika mara ngapi mwaka mzima?
- Haitafanya kazi mara ngapi kwa sababu ya dereva mgonjwa au safari binafsi(lets say matatizo)
- Utatumia wewe kwa matumizi yako binafsi mara ngapi?
- Itakamatwa na polisi mara ngapi (kutoa rushwa)
- etc..

Baada ya mwaka unasema unamwachia,bajaji umenunua mil 5 mwisho wa mwaka umepata mil 10 na bajaji umemwachia mtu huoni faida inakuwa ni chini ya mil 5 mwaka mzima? Na umempa mtu mil 5 hivi hivi? Halafu utanunua mpya au?
 
Inategemea dereva wako kama anaitunza Bajaji, pia kila baada ya wiki tatu ufanye service. Lazima uwe na daftari la taarifa za mapato, matumizi na service. Kama unaendesha mwenyewe ni bora zaidi na inalipa
 
Bajaji nzuri ni TVS. Hesabu kwa sasa ni 20,000 kwa siku. Ikatie bima kubwa/ comprehensive insurance ili hata ikiibiwa or kupata ajali uweze kulipwa na bima. Ili idumu ni vizuri uachie siku moja ya week ufanyie service, hata kama dereva ndo anaifanyia services, jitahid walau Mara 1 Kwa mwezi uwepo wakati wa service. Na pia ili Bajaji isiwe over worked, mpe dereva limit ya mda wa kurudisha Bajaji jioni na ilale na wewe kuavoid cases za Wizi na pia kufanya Kazi masaa 24.
 
Una kifua ? Unamaana gani mkuu?

Biashara pasua kichwa hyo. Ndio nlicho maanisha. Kupata kijana mstaarab na mwaminifu ni bahati sanaa. Wapo vijana ukimpa bajaj yako hutakaa usikie ikiharibika ovyo (nidham ya matumizi/uendeshaji)...ila wengine kila siku utafanya kutafuta spare kkoo/ilala alaf returns za kipuuzi.

Kama mtu ana kimtaji chake anataka kukaza kivyake hapo sawa itamtoa big tym (wapo watu wamejenga from bajaj)....hata uendeshaji wako utakua wa adabu.
 
Biashara pasua kichwa hyo. Ndio nlicho maanisha. Kupata kijana mstaarab na mwaminifu ni bahati sanaa. Wapo vijana ukimpa bajaj yako hutakaa usikie ikiharibika ovyo (nidham ya matumizi/uendeshaji)...ila wengine kila siku utafanya kutafuta spare kkoo/ilala alaf returns za kipuuzi.

Kama mtu ana kimtaji chake anataka kukaza kivyake hapo sawa itamtoa big tym (wapo watu wamejenga from bajaj)....hata uendeshaji wako utakua wa adabu.

Mkuu hamna biashara inayokosa changamoto so ni kumpa moyo na kumpa ushauri mzuri mkuu...karibu Sana Event 9 limited tukusaidie kuhusu biashara hii
 
- itaharibika mara ngapi mwaka mzima?
- haitafanya kazi mara ngapi kwa sababu ya dereva mgonjwa au safari binafsi(lets say matatizo)
-utatumia wewe kwa matumizi yako binafsi mara ngapi.?
-itakamatwa na polisi mara ngapi(kutoa rushwa)
- etc..
Baada ya mwaka unasema unamwachia,bajaji umenunua mil 5 mwisho wa mwaka umepata mil 10 na bajaji umemwachia mtu huoni faida inakuwa ni chini ya mil 5 mwaka mzima? Na umempa mtu mil 5 hivi hivi? Halafu utanunua mpya au??????

Kutofanya Kazi na kuharibika vinakua nje ya hiyo hesabu kwasababu service zote zinakua juu ya Dereva ambae anategemea kuichukua hiyo Bajaji baada ya kumaliza mkataba wenu.hii humfanya Dereva aitunze Sana kwasababu anajua inakuja kuwa yake...hivyo atakapofikisha hela hiyo wewe inakua unauwezo wa kununua Bajaji zingine Mbili Mpya hivyo Bajaj 1 inakua imezaa Bajaji Mbili kwa Mwaka.
 
Back
Top Bottom