Hii biashara ni nzuri lakini ina changamoto zake kama zilivyo biashara nyingine. Kwa kifupi nikupa yale machache ambayo ni ya kuzingatia katika hii biashara.
1. Hakikisha chombo kinalala kwako, maana usipofanya hivyo madereva wa bajaj wana kawaida ya kukifanyisha chombo kazi kwa muda wa saa zote 24 za siku kwa utaratibu wa kuwaachia deiwaka. Halafu wewe anakuletea Tsh 15000 tu, wakati unaweza kukuta wametengeneza hadi Tsh 70,000 (Kama siku ikiwa nzuri sana) kwa siku.
2. Hakikisha unasimamia service na uwe na rekodi ya siku unayofanya service maana usipofanya hivyo, kuna uwezekano ukaambiwa kuna service imefanyika ilipe utoe hela wakati hakuna kilichofanyika. Hii inaweza kufanya chombo kikachoka haraka hadi ukashangazwa.
3. Kama huna utaalamu hata kidogo na mambo vyombo vya moto, sikushauri hata kidogo kununua bajaj zilizotumika maana utatumia hela nyingi sana kulipa mafundi na kununua spea. Ni vizuri ununue vyombo vipya na pia usikae navyo sana, fanyia kazi si kwa zaidi ya miaka miwili, uza na ununue vingine.
4. Usiwachekee kabisa hao madereva kwenye masuala ya hesabu maana hawachelewi kukuletea stori za biashara mbaya wakati wakipiga hela hawakuongezi hata sh 100 kwenye hesabu yako. Kama biashara mbaya weka deni, siku zijazo wajazie hiyo hesabu.