Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri


Ahsante mkuu saiv nina 4m nadunduliza ninunue.
 

Nice advice mkuu. Big up
 

Mimi nafanya hiyo biashara..na mpk sasa ninazo mbili! inalipa sana hapa town ila kwa njia ya mkataba otherwise itakutesa kama huyo mkuu hapo aliyekua anachukua 15 kwa siku!

Ni hiv mkataba huwa ni miez kumi na 8 (mwaka na nusu) na kwa siku kipande ni elfu 20 na anakupa kwa wik = laki na 40/- kwa mwez ( x 4 = 560,000/-) kwa mwaka na nusu itakua 560,000 x 18 = tshs 10080000/-

Kuhusu matengenezo huduma zote za kawaida anafanya dereva icpokua huduma kubwa kubwa tu ndo utahusika tena kwa kushea gharama na dereva!

Kuhusu ipi ni bora' kwa mkataba bora piagio siyo TVS

Kwann piagio? Kwasababu inanafas kubwa ya abiria kukaa na mizigo pia ukilinganisha na TVS
Tvs ni nzuri kwa mtu anaefanya biashara bila mkataba kwasababu ikimrudishia hela ni rahis kuiuza (inauzika kirahis/inasoko kubwa) na hii ni kwasababu ziliwah kuingia hapa bongo kabla ya piagio)

Uimara wa chombo uko mikonon mwa dereva! ila piagio sina shaka nazo kwenye uimara!

Nin faida ya kuingia mkataba?

1/ Bajaj haihitaj uangaliz mkubwa kwasabab dereva anajua baada ya miez kumi na 8 bajaj ni yake! ( hawez kuitumia roughLy)

2/ Ni win-win project yaan wote wanufaika dereva na boss pia hivyo bas haitakua kaz ngumu kumpata dereva

3/ Huduma za mara kwa mara hazitakuepo mana anakua anaiendesha kwa uangalifu mfano, hata *dei waka huwa hawatoi hawa madereva wa mikataba na kama ikitokea service anamaliza mwenyewe unLess iwe kubwa na pia mtashea gharama!

4/ Payback period ni kubwa kwa muda mfupi..

ANGALIZO>> usisahau kukatia BIMA bajaj yako tena BIMA kubwa! ili uondokane na stress inapokua barabarani!
 
Mkuu hii bima kubwa ya comprehensive ni kama bei gani?
 
Na mkiingia mkataba wa hiyo 20,000 kwa siku ina maana yeye dereva analipwa kiasi gani hasaaa au ndio humlipi hela yoyote ile? Naomba kufahamu hapo na hizo bajaji zina range kwenye kiasi gani? Na wapi naweza kupata nzuri? Na bima ipi nzuri ambayo naweza kuchukua na bima ni kiasi gani kwa mwaka?
 
Nakushauri ufanye hiyo biashara kwa kuwa ni profitable. Mimi pia ninafanya hiyo biashara na mpaka sasa ninazo mbili. Three-wheeler nzuri ni TVS King maana inadumu kwa muda mrefu na pia ni rahisi kupata spare zake na bei nafuu ukilinganisha na aina nyingine za Three-wheelers.

Mimi 'Bajaj' zangu kwa siku hesabu ni sh 20,000 each so kwa mwezi inanipa sh 600,000 kwa kila moja (hapo excluding services). Bajaj kwa mwezi zinafanya service mara mbili ili ziendelee kuwa na hali nzuri na esttimation ya service ni sh 22,000 so kwa mwezi gharama inakuwa sh 44,000-45,000.

Hakikisha unakuwa na kijana anayeeleweka maana huyu ndio a 'secret' ya mafanikio yako, chukua kijana mwenye 'commitment' hapo hutapata usumbufu sana. Pia hakikisha Bajaj yako ina vibali vyote ili usiwe unapoteza hesabu yako kwa kudanganya kuwa amekamatwa na traffic imebidi ampe hesabu yako, vibali ni SUMATRA, Insurance na Road licence (Road licence unalipia once tu maana serikali imetoa msamaha kwa Bajaj na pikipiki kwenye hili). I hope nimeweza kukusaidia kwa kiasi chake.

P.S Sehemu nyingine, mfano Africana njia ya chini hesabu ni sh 25,000 kwa siku so inategemea na location pia mkuu.
 

Shukurani mkuu kwa kushea maelezo na uzoefu wako katika hii biashara. Kuna issue ya kukata bima ya comprehensive ili bajaji ikipata ajali au ikiibiwa uweze kulipwa, wasiwasi wangu ni kuwa huyu kijana wa kazi akishajua ina bima kubwa anaweza kufanya mchezo wa kuiiba yeye mwenyewe huku akijuwa itakuwa replaced, sijui hii imekaaje wadau.
 

Faida ya kumwambia utamwachia baada ya kipindi fulani ni kwamba atahangaika kuhakikisha kuwa amelipa hilo deni ili na yeye aweze kupata faida fulani.

Lakini ukimwawmbia lete ngapi kwa siku, likitokea tatizo lolote gharama juu yako, at the end of the day unajikuta kile anachokuletea unakitoa kwa matengenezo, insurance, faini za polisi na kadhalika. Faida atapata yeye mwendesha bajaji tu wewe hutaambulia cho chote.

Yamenikuta hayo kwenye gari la mizigo mpaka nikaamua kuliuza.
 

Asante sana tena sana ndugu yangu,Nashukuru sana kaka maana umenifungua vitu vingi sanaa ambavyo nilikuwa sijui kabisaa hapo so hapo africana kupeleka bajaji inakuwaje hasaaa??Na upande wa malipo ya dereva ni yeye ndio anajilipa au inakuwaje hasa??

Me nashukuru sana umenifungua mambo mengi na umekuwa open bila kudanganya kwamba bajaji inalipa maana wengine wanaficha kabisaa hawasemi ukweli kabisaaaa, Na upande wa Insurance ina range kiasi gani kwa mwaka??
 
Unapoikatia bima kubwa huna haja ya kumwambia dereva wako kuhusu hilo na kikubwa unamuwekea muda reasonable wa kulaza 'chombo'. Kama mimi za kwangu huwa zinalala saa tatu kamili, akizidisha hata lisaa limoja ananilipa sh 30,000 so ikitokea bahati mbaya/nzuri amepata mteja wa mbali na muda unakaribia kumalizika huwa anapiga simu nijue kabisa his 'wherebouts'.
 
Papizo, dereva anajilipa mwenyewe hapo, unaweza mpangia masaa ya kazi tokea saa kumi na moja asubuhi mpaka saa mbili usiku. Bima inategemea, third party ni 120,000 i guess and comprehensive ita depend umei value kiasi gani...ila hesabu ya comprehensive i guess ni 3.5% ya value ya Bajaj yako, you can do the Math there. Hope nimekujibu mkuu
 
Last edited by a moderator:

Asante mkuu nilidhani ile insurance paper/ copy inabandikwa kwenye chombo kwa hiyo lazima atajua ni kubwa au yakawaida.
 
LugovoyHapana bro, ukikata third party/comprehensive zote sticker ni ile ilele cover note ndio inasema kama third party ama comprehensive. Karibu.
 
Last edited by a moderator:

Asante sanaa mkuu nashukuru sana maana atleast umenifungua mengi hapo na nashukuru sana kwa maelezo yako maan nikajuwa unamlipa, asante sana kama ni hivyo basi vizuri kabisaaaa, nitakucheck mkuu unisaidie mambo fulani.
 
Last edited by a moderator:
Shukurani Zinja88 nimekupata vizuri, naplan kuinvest kwenye bajaji, mwanzoni nilifikiria bodaboda 2 za mkataba lakini muda wa mkataba mara nyingi ni miezi 12 tu na faida inakuwa kidogo sana ukilinganisha na bajaji kwa miezi 18.
 
Mkuu hata bajaj aina ya Piaggio ziko poa sana ndo maana zinazidi kuongezeka mjini. Nina uzoefu nazo kwani ninazo zaidi ya nne. Ukihitaji pia uzidi ambayo ina rudisha hela ndani ya miezi 3 kisha unaanza kula faida
 
Aise nimepata kitu humu, je mnaweza kutapa ufafanuzi juu ya kirikuu? Ni ipi bora kati ya kirikuu na bajaji? na bei ya bajaji kwa sasa ni sh ngapi? Min and maximum price
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…