Biashara ya uwakala wa simu na benki (M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, fahari huduma na NMB Wakala) unaweza kuanza kwa mtaji wa shilingi ngapi?

Kuna classmate wangu mmoja kigamboni wadogo zake wawili walikula shaba getini kwao kabisa! Wajuba wakabeba million 4
 
Hii biashara nilishasemaga ni ya watu wavivu kufikiri! Kuna mtu alininanga ila nilikuwa nishampa ukweli!

Its useles ku risk million 10 kwa mwezi mzima kwa returns za 1.5M ambayo ni makadirio ya juu sana unaweza pata chini ya hapo! Kuna kupigwa risasi na sahizi Magufuli hayupo maana ujambazi utakuwa nje nje! Kuna chumaulete pia! Its surely a risky bet
 
Kabisa, unless uwe na mtaji mkubwa wa kuifanya kama hizi 'mini bank' ambapo unaweza kuajiri watu wenye taaluma ya fedha (cert/diploma au bachelor) na kudeploy security ambayo itapunguza risk.

Hata hivyo hizi kwa asili ni huduma na si biashara, hata bank hazitegemei hizi transactions kujiendesha ndio maana wana engage mawakala na wao wanajikita zaidi kwenye corporate banking, kwa hiyo bado profit margin ni ndogo ukilinganisha na mtaji huo huo ukiwekeza kwenye biashara zingine.
 
Yah bora kutafta chaka jingine ambalo kwa million 5 waweza pata returns hizo ndani ya week tu au siku 10!
 
Pia nimegundua watu wengi huwa hawafanyi analysis kabla ya kuingia kwenye business, wengi huiga tu kwa kuona fulani anafanya.

Mfano, watu wengi anapotoa pesa kama mteja kwenye let's say M-pesa kiasi cha laki 1 na kukatwa 3,650/= anahisi pesa yote ile inaenda kwa wakala, kisha anaangalia movement ya wateja... anaona jamaa anapiga pesa hatari [emoji23][emoji23]

Ila kiuhalisia katika ile 3,650/= ya kutolea, wakala anabaki na tshs. 460/= na hapo bado haijakatwa kodi 10%. Sasa ndio hizo uzidundulize hadi mwisho wa mwezi uje utoe gharama ya kulipa operator(s), hujalipa kodi ya pango, umeme, ulinzi nk. unabaki na kiasi kidogo sana kwa kweli.
 
Duh! Mbona ni shida sasa
 
Kwa hesabu hizi ni kwamba kwenye transaction ya milioni moja (1,000,000) unapata 4,600 kabla ya hiyo kodi ya asilimia 10, ambapo ukikatwa na yenyewe unapata kama 4,160....so ili uondoke na commission (faida) ya 20k kwa siku ni ufanye miamala ya shilingi milioni tano taslimu (5,000,000)....sijui nipo sahihi
 
Ukifanya muamala mmoja wa milioni moja wa kutoa commission ni kama elfu 2, kuweka ni 1,500/=. In short miamala mikubwa kamisheni inapungua sana, ukipata miamala midogo midogo ndio inalipa zaidi.

Mfano, ukimuwekea mteja mmoja milioni moja kamisheni ni 1,500/= ila ukiwawekea wateja kumi wa laki moja moja utapata kamisheni zaidi ya elfu 4.
 
Kama ni hivi biashara hii ni nzuri kwa sehemu kama sokon inalipa.ila kama ninkweli anayosema huyo wa comment ya juu kwamba muamala wa milion moja unapata 460 basi hii biashara ni taka taka.
 
Ofcoz naelewa hivyo pia ila nilipigia kwa miamala ya kilo kilo ambayo ndo ilikua sample yetu na kwa upande mmoja au mwingine ndio faida ambayo ni maximum kwa wastani wa kawaida
 
Kama ni hivi biashara hii ni nzuri kwa sehemu kama sokon inalipa.ila kama ninkweli anayosema huyo wa comment ya juu kwamba muamala wa milion moja unapata 460 basi hii biashara ni taka taka.
Sio mia nne sitini mkuu ni elfu nne na mia sita tena ni kwa miamala kumi ya laki laki na hapo kabla ya asilimia kumi ya kodi mbapo utabakiwa na elfu nne na mia moja sitini kama faida
 
Kama ni hivi biashara hii ni nzuri kwa sehemu kama sokon inalipa.ila kama ninkweli anayosema huyo wa comment ya juu kwamba muamala wa milion moja unapata 460 basi hii biashara ni taka taka.
Yah, ukiwa kwenye eneo lenye mzunguko mkubwa unapata faida. Problem ni risk zinazo ambatana na biashara hii na pia ukijaribu kufanya comparison ya mtaji huo huo ukiwekeza kwenye aina nyingine ya biashara faida yake itakuwaje.

Otherwise, kama mtu hana option nyingine ama anafanya biashara hii kama nyongeza kwenye biashara yake nyingine pia ni nzuri zaidi sabab gharama mfano za pango, umeme, mlinzi na pengine operator zinakuwa covered na biashara kuu.
 
Ofcoz naelewa hivyo pia ila nilipigia kwa miamala ya kilo kilo ambayo ndo ilikua sample yetu na kwa upande mmoja au mwingine ndio faida ambayo ni maximum kwa wastani wa kawaida
Yah ni sahihi kabisa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…