Biashara ya uwakala wa simu na benki (M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, fahari huduma na NMB Wakala) unaweza kuanza kwa mtaji wa shilingi ngapi?

Biashara ya uwakala wa simu na benki (M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, fahari huduma na NMB Wakala) unaweza kuanza kwa mtaji wa shilingi ngapi?

Nawashukuru sana....mpesa kurudisha lipa kwa mpesa kama ilivyo lipa kwa Tigo pesa.
 
Boss mtaji 20M upate commission ya sh 500k? Kuna tatzo mahali au huenda ndo kwnz umeingia kwenye game. Hyo 500k ilitakiwa ipatikane ktk line mojawapo ya unazofanyia dukan. Kwangu line zinazofanya vbaya ukitoa t-pesa ni halopesa na airtel money, ila nikijumlisha commission ya halopesa +airtel money =500k. Na hapo mtaji wangu haujafika hata nusu ya huo mtaji. Imagine nina uwakala wa crdb, nmb, tpb, nbc, equity, akiba +maendeleo Bank. Narudia mtaji wangu haujafka hata nusu ya 20M.
Mkuu niko kwenye location mbaya. Kwenye hii biashara nimegundua location matters a lot. Hata hivyo nina mpango wa kufungua ofisi nyingine maeneo ya mjini ili compliment each other
 
Jaman nina mtaji wa 4M na plan ya kuingia kwenye hii biz yan nitakuwa na 3M ya floats vip naweza toboa ?
 
Nimeona watu wanajaribu kutoa ufafanuzi kwenye mambo wanayosikia kwa watu, mimi nimemaliza chuo mwaka 2017 hapa jijini wakati nipo chuo nilinunua lain za uwakala kwa wakala mkuu wa mitandao yote. Nilivyomaliza nikapiga kambi rasmi na mwamvuli tu barabarani na mtaji wangu wa laki 8 mpaka sasa nakwambia nimeshajenga nyumba kali na ni well finished kwenye eneo lenye thamani kubwa kigamboni na kumiliki viwanja na mashamba kwa biashara hyo hyo takataka. Kuna watu wanapenda kutoa ufafanuzi wa mambo ambayo hawajawah fanya kama risk hakuna biashara ambayo haina ila kuwa mwangalifu tu na wateja unaowauhudumia sio kila mteja unamtolea hela kubwa au kumuekea hawa ndio wanakua chanzo cha mambo yote na pia usijenge urafiki na wateja kama kashahudumiwa aondoke ofisi yako sio kijiwe. Mwisho kwa uangalifu, kupigwa kupo hata mimi nilipigwa laki tatu kwa kuleta mazoea na mteja pamoja na kutoshikiria kanuni za kazi. Tigo pesa sasa hivi hakuna biashara kama hii ina moto sana watu wanapata namba za ajabu kwa mitaji midogo
 
Hii biashara nilishasemaga ni ya watu wavivu kufikiri! Kuna mtu alininanga ila nilikuwa nishampa ukweli!

Its useles ku risk million 10 kwa mwezi mzima kwa returns za 1.5M ambayo ni makadirio ya juu sana unaweza pata chini ya hapo! Kuna kupigwa risasi na sahizi Magufuli hayupo maana ujambazi utakuwa nje nje! Kuna chumaulete pia! Its surely a risky bet
Inasikitisha kuona watu wamelike kabisa comment yako. Wewe bila shaka sio mfanyabiashara wala huna uelewa wa kutosha wa biashara
 
Mimi nahis napingana na wanao Sema faida ni ndogo kwa sababu Kuna wakala Ana tigo pesa, mpesa na Airtell money ila kwa mwezi anapiga laki 4 vipi wale wenye mpaka branch za bank?

Mimi kuna jamaa yangu kwa mwezi inagonga 2na nusu mpaka Tatu na nusu Milion
Hiyo ndogo sana watu wanagonga million mpaka 8 Nmb/Crdb/Nbc/Tpb huku sumbawanga
 
Mwenye mashine wa Uwakala ya NMB tafadhali tufanye biashara
 
Back
Top Bottom