Working capital kama wakati unafunga hesabu zako jioni itakuwa in form of float basi ni rahisi zaidi, lakini kama utakuwa na hard cash nyingi nadhani utaangalia usalama wa ofisi yako kama unaweza kutunza ndani ama vinginevyo itabidi uzibebe pamoja na POS zako.
Kama uko jirani na branch ambayo inafanya kazi 24hrs (kwa maeneo ya mjini) basi ni vema uka-deposit ukishafunga ofisi kuhakikisha usalama lakini pia itakurahisishia kesho kuanza kazi ukiwa na float asubuhi maana nature ya transaction nyingi ni za kuweka zaidi.
Angalizo:
Pia inabidi kuwa makini sana na wateja wanaokuja mida ya mwisho mwisho kabla ya kufunga, baadhi wanaweza kuwa wezi wanakuvizia kwa hiyo anakuja na cash nyingi then anaweka M-pesa kama haijatosha ataweka na NMB, tigo na airtel ili ahakikishe amekuacha na cash ili wakikuvamia wachukue cash zao bila tabu.