Biashara ya uwakala wa simu na benki (M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, fahari huduma na NMB Wakala) unaweza kuanza kwa mtaji wa shilingi ngapi?

Biashara ya uwakala wa simu na benki (M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, fahari huduma na NMB Wakala) unaweza kuanza kwa mtaji wa shilingi ngapi?

Hello great thinkers! Leo nimeanza rasmi biashara ya Vinywaji~rejareja pamoja na uwakala wa mitandao yote. Eneo ni changamfu na kuna watu tunaofahamiana(wateja wa uhakika hawa).

Naomba kufahamishwa mazuri na changamoto za biashara husika, fursa zaidi zilizopo na jambo lolote lenye kujenga/tija.

Nimefanya maboresho kwa kuweka muonekano mzuri wa frem na mazingira ya Ofisi, lengo ni kuwapata wateja wote, wa chini kati na juu!
Asanteni.
Punguza kujielezea sana, wewe fanya biashara.
 
Working capital kama wakati unafunga hesabu zako jioni itakuwa in form of float basi ni rahisi zaidi, lakini kama utakuwa na hard cash nyingi nadhani utaangalia usalama wa ofisi yako kama unaweza kutunza ndani ama vinginevyo itabidi uzibebe pamoja na POS zako.

Kama uko jirani na branch ambayo inafanya kazi 24hrs (kwa maeneo ya mjini) basi ni vema uka-deposit ukishafunga ofisi kuhakikisha usalama lakini pia itakurahisishia kesho kuanza kazi ukiwa na float asubuhi maana nature ya transaction nyingi ni za kuweka zaidi.

Angalizo:
Pia inabidi kuwa makini sana na wateja wanaokuja mida ya mwisho mwisho kabla ya kufunga, baadhi wanaweza kuwa wezi wanakuvizia kwa hiyo anakuja na cash nyingi then anaweka M-pesa kama haijatosha ataweka na NMB, tigo na airtel ili ahakikishe amekuacha na cash ili wakikuvamia wachukue cash zao bila tabu.
Madini haya
 
Aisee mtaji usikupe shida, waza ni eneo gani tu. Kama ni mjini utahitaji mtaji mkubwa kiasi kweli angalau 10 mil ili uwe comfortable. Vinginevyo anza na iliyopo ili ujue kama unahitaji kuongeza au vipi. Changamoto zingine zimesha ongelewa.
Lain ya till ya tigo naipataje, npo iringa mufindi
 
Lain ya till ya tigo naipataje, npo iringa mufindi
Nenda Tigo shop yoyote hapo Mafinga, watakupa mwongozo. Au unataka line ya kumvua mtu? Ukishindwa kabisa nenda Iringa mjini. Tigo shop iko mkabala na ile stendi ya zamani.
 
Hata mimi jengo lipo hatua za mwisho. Sidhani kama nitabadilisha matumizi. Nitajitahidi tu kuchukua tahadharu dhidi yaa matapeli na hayo majambazi. No way out.
Endelea kusubiria maoni y watu wakati watu wanapiga pesa. Hakuna bznes isiyo n risk mdau. Kinacho takiwa ni kuangalia jinsi gani y kupunguza tu.
The 4
 
Mkuu nakushukuru sana.

Kuna watu wanaponda hii biashara lakini ukisoma alichokiandika unagundua kuwa hajawahi kufanya biashara hii bali anazo story tu za vijiweni.

Kwangu mimi mtaji sio shida sanaaa,ila maelewano na wafanya biashara wenzangu wanaonizunguka (Mawakala) ndo kitu kinaniweka town , Nina uwezo wa kumuhudumia mteja aliyekuja kutoa laki 8 wakati mimi nina cash ya laki 5 tu.

Endeleeni kuponda ,muhimu tu mje tuwahudumie .

Wanangu pesa ipo.
Saw poll94ezzteeztee
 
Part kubwa ya huu uzi ulijibiwa na watu ambao hawapo kwenye game, mtaji wa million 10 kwa uwakala wa mpesa, tigo pesa na hizo bank ni kukurupuka, biashara hii unashauriwa kuanza kidogo ukipma upepo then unatanua misuli mbele baada ya kuelewa mzunguko.
 
Part kubwa ya huu uzi ulijibiwa na watu ambao hawapo kwenye game, mtaji wa million 10 kwa uwakala wa mpesa, tigo pesa na hizo bank ni kukurupuka, biashara hii unashauriwa kuanza kidogo ukipma upepo then unatanua misuli mbele baada ya kuelewa mzunguko.
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
TANGAZO

Kwa wahitaji wa laini za uwakala zenye majina yao natengengeza hizo kwa muda muchache inakamilika ndani ya masaa 24.

Laini zinatengenezwa ni kama zifuatazo:

NB malipo ni baada ya kazi[emoji736][emoji736]
Inahitajika kiasi Gani Cha pesa kwa Kila laini moja
 
Mkuu tunakupataje Kwa laini za uwakala wa tigopesa na HALOPESA hizo ndiyo Bado cjapata mkuu
 
Hii biashara nilwahi kufanya, baada ya Covid kuingia mambo yakibadilika kiasi fulani, na baada ya tozo za miamala kuongezwa ndio kabisaa, binafsi nashauri kama unafanya hiyo biashara uwe na biashara ingne hapo hapo
Unaweza kuweka biashara gani nyingine kwenye fremu kama hiyo inayoshughulika na miamala ya simu na benki na usisumbuliwe kuhusu leseni ya hizo bidhaa nyingine?
 
Ndugu zangu je uwakala wa pesa kwa njia ya simu na bank unalipa?
Je malipo yakoje?
Faida ikoje?
Hasara nayo vipi?
Zipi changamoto zake?
Kumekuwa na idadi kubwa sana ya wanachi kujiingiza katika biashara ya wakala wa pesa kwa njia ya simu na bank, je faida inayopatikana ndiyo inayoshawishi wananchi kuwa wakala ama ni ugumu wa maisha unapelekea wanachi kufanya biasha yeyote pasipokujali maslahi?
Hivi kwa nini makampuni ya simu yanawasajili mawakala ambao ufanya biashara ya miamala popote pale pasipo hata kuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo kutoka kwenye mamlaka husika? Nionavyo kwa kufanya hivyo kunadhoofisha biashara ya wale wafanya biashara wengine waliolipia leseni za biashara hiyo huku wakiingia gharama nyingine za kukodi eneo la biashara, n.k.
 
Maana pia ni Wakala Mkuu wa CRDB yupo kariakoo
HIvi kuwa wakala mkuu wa mtandao mfano Tigo ni hadi uwe na mtaji kiasi? Na pia kuwa wakala mkuu wa NMB au CRDB ni hadi uwe na mtaji wa kiasi gani?
 
Part kubwa ya huu uzi ulijibiwa na watu ambao hawapo kwenye game, mtaji wa million 10 kwa uwakala wa mpesa, tigo pesa na hizo bank ni kukurupuka, biashara hii unashauriwa kuanza kidogo ukipma upepo then unatanua misuli mbele baada ya kuelewa mzunguko.
Wewe uonavyo hicho kiasi kidogo cha kuanza nacho kinatakiwa kuwa kiasi gani?
 
Hii biashara nilishasemaga ni ya watu wavivu kufikiri! Kuna mtu alininanga ila nilikuwa nishampa ukweli!

Its useles ku risk million 10 kwa mwezi mzima kwa returns za 1.5M ambayo ni makadirio ya juu sana unaweza pata chini ya hapo! Kuna kupigwa risasi na sahizi Magufuli hayupo maana ujambazi utakuwa nje nje! Kuna chumaulete pia! Its surely a risky bet
Naomba wazo lingine ukiachana na hii ya uwakala Mzee
 
Nmegundua kwamba watu wengi wapo ili kukatisha wengne tamaa.

Sio kila biashara ulioshndwa ww kwmb haina faida. Na wengi wetu tunapenda kuponda biashara wakati hatujawahi kuifanya.

Kila biashara ina changamoto zake kwahyo biashara ya wakala ina changamoto km biashara nyngne.

Kuna watu biashara hii ya uwakala wamejenga alafu leo unasema ni biashara kichaa?

Ktk kila biashara kila mtu ana malengo yake kwahyo tusipende kukatishana tamaa.

Biashara hii ili uone faida yake lazma uchague location nzuri na uwe na mtaji. Km mtaji wako ni mdogo basi uwe mjanja sana. Ujanja sio kuibia watu bali uwezo wako wa kuwahudumia watu na kuhakikisha kila anayefka kwako anapata huduma kwa wakati bila shda.

Hapo juu kuna mtu amesema faida zake haziongezi wala huwez kupata wateja wateja wapya. Hii sio kweli.

Mm nafanya biashara hii na huniambii kitu
NI kwel hata mm nlshaifanya , mm nlchojfunza hapa NI tahadhar , location na mtaji
 
Back
Top Bottom