Biashara ya viatu inaweza kukutajirisha

Biashara ya viatu inaweza kukutajirisha

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,641
Reaction score
4,457
Hello

Natumaini mnaendelea vyema na harakati za kutafuta maisha nimeona leo niwaibie siri jinsi hii biashara ya sandals na viatu inaweza kukutajirisha kwa haraka.

Historia

Mimi kwa majina ya kuzaliwa naitwa Innocent kirumbuyo nimezaliwa Kilimanjaro katika hospital marubeneti miaka mingi iliyopita huko nyuma.

Mwaka 2012 nilimaliza elimu yangu ya sekondari katika shule ya sekondari Siha

Baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari nilingia mtaani kutafuta maisha ndipo nilipo jisogeza paka kwenye jiji la miamba Mwanza alimaarufu rock City

Nilipofika tu Mwanza nilianza na biashara ya kuuza viatu vya kike simple zile bei ndogo nilifanya ile biashara kwa kipindi cha miezi miwili tu.

Nikabadili biashara na kuanza kuuza simu za mkononi nilifanya biashara ya simu kwa mwaka moja tu

Kwa mara nyingine tena nikabadili tena biashara nakuanza kuuza viatu na sandals biashara ya viatu na sandals ndio ninafanya paka muda huu ni biashara nzuri sana ambayo ukiwa nayo makini unaweza kutajirika na kusahau umasikini kabisa

Unajua kwanini nakuambia hivyo hii biashara nimeifanya kwa miaka 7 ni biashara nzuri sana naitambua vizuri

Inachangamoto ila siyo kubwa sana kama za biashara nyingine ambazo nimefanya.

Uzuri hii biashara cha kwanza kuna faida kubwa sana na inamzunguko mkubwa sana

Unaweza kupata paka 60 elfu kwa katoni moja tu ata zaidi na hii katoni moja unaweza kuuza kwa siku au wiki inategemea sana mzunguko wako.

Karibu kwenye biashara ya viatu.

Tunakaribisha maswali maoni nipo hapa kutolea kila kitu ufafanuzi kwa kadiri navyoelewa.

passions100mins_kariakoo_20200828_164815_0.jpg
viatu_jumla_rejarejaa_20200621_151842_0.jpg
viatu_jumla_rejarejaa_20200621_152207_0.jpg
viatu_jumla_rejarejaa_20200725_161326_0.jpg

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
unauza kwenye frem au kuzunguusha mtaani au kupanga barabarani? Ipi itakulipa zaidi? Nawasilisha
Nauza kwenye fremu mimi ila kupanga barabara inalipa sana kwasababu ata ukiuza laki moja auwezi kuwaza kwasababu inakuwa umeepuka cost kubwa sana kama kodi za serikali fremu n.k

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Viatu vinalipa kweli kama una mtaj hata wa m1 baada ya mwaka unaweza kuwa na mtaj mkubwa sana .me nina biashara nyigine lkn baada ya vyuma kukaza. niliweka kimeza nje ya frem nikaanza na mtaji wa elf 70 nafata moshi naleta arusha vya mtumba. kuna kiatu unanunua elfu 5 kikiwa kichafu ukiosha unauza elf 20, kwa sasa mpaka natamani nihachie frem nibaki nje maana sikosi faida elfu 20 mpaka 30 kwa siku.
IMG_20200924_145104_7.jpg
IMG_20200924_145808_0.jpg
IMG_20200924_150142_3.jpg
IMG_20200924_145526_8.jpg
IMG_20200924_150503_4.jpg
IMG_20200924_150633_6.jpg
 
Attachments

  • IMG_20200924_145958_2.jpg
    IMG_20200924_145958_2.jpg
    93.1 KB · Views: 235
viatu vinalipa kweli kama una mtaj hata wa m1 baada ya mwaka unaweza kuwa na mtaj mkubwa sana .me nina biashara nyigine lkn baada ya vyuma kukaza. niliweka kimeza nje ya frem nikaanza na mtaji wa elf 70 nafata moshi naleta arusha vya mtumba. kuna kiatu unanunua elfu 5 kikiwa kichafu ukiosha unauza elf 20, kwa sasa mpaka natamani nihachie frem nibaki nje maana sikosi faida elfu 20 mpaka 30 kwa siku.View attachment 1583207View attachment 1583208View attachment 1583210View attachment 1583211View attachment 1583214View attachment 1583216
Hongera sana boss alafu moshi kuna mtumba mzuri sana tofauti na mikoa mingine usiache frem tafuta eneo jingine weka mtu mwingine mwambie ata kwa siku akupe 5000 au wewe utaona akupe ngapi kulingana na kasi ya biashara

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
viatu vinalipa kweli kama una mtaj hata wa m1 baada ya mwaka unaweza kuwa na mtaj mkubwa sana .me nina biashara nyigine lkn baada ya vyuma kukaza. niliweka kimeza nje ya frem nikaanza na mtaji wa elf 70 nafata moshi naleta arusha vya mtumba. kuna kiatu unanunua elfu 5 kikiwa kichafu ukiosha unauza elf 20, kwa sasa mpaka natamani nihachie frem nibaki nje maana sikosi faida elfu 20 mpaka 30 kwa siku.View attachment 1583207View attachment 1583208View attachment 1583210View attachment 1583211View attachment 1583214View attachment 1583216
Ila boss una viatu vizuri sana

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom