Biashara ya viazi mviringo

hizo bei za dawa zipo sawa, lakini kumbuka Mastakinga kilo moja utapiga wiki mbili au tatu itakua imeisha, kwa eka moja unahitaji walau kilo nne na nusu. Viazi vinaenda hadi miezi 4
 
Hujaweka mbolea ya kukuzia Mkuu,! Alafu hyo DAP kilo ulizoweka hazitoshi kulima ekari 1
 
Habari, Naombeni kujua mwenye kujua viazi mviringo kwa kipindi hichi vinauzwa bei zipi mikoa njombe na mbeya mzigo kwenda Dar!
 
Habari, Naombeni kujua mwenye kujua viazi mviringo kwa kipindi hichi vinauzwa bei zipi mikoa njombe na mbeya mzigo kwenda Dar!
UMALILA MBEYA Kwa bei ya shambani kwasasa wachuuzi wananunua 25,000/= kwakipeto cha debe 5 sawa na 5,000/= kwa debe moja.
Wakulima wanalalamika kuwa bei hiyo ipo chini wengi wameamua kuviacha kwa muda humo humo shambani kusikiliziia bei kama itapanda panda,kama itaendelea kubaki hapo hapo bora waviache waje wauze mbegu..
kwahiyo kama unataka uje ujaze mzigo chapu nakusepa njoo na ofa japo ya elf 30 kwakipeto cha debe 5 sawa na elf 6 kwa debe
 
Naombeni kujua bei ya viazi kwa sasa wapendwa, na viazi pendwa kwa wana dar es salaam ni kutoka mkoa gani?
 
habari mkuu
mimi pia nahitaji kuanza hii biashara lkn niliplan kutoa mbeya kuleta Mwanza naomba kujua yafuatayo

umesema usafiri unalipa advance ( na kwa Dar unaanza na laki 3 probably kwa kuwa malori yanakuwa yanarudi bila mzigo) vipi bei kamili ya usafiri ni ngapi? na kama una fahamu bei ya usafiri kuja Mwanza

na kama unashare na mzoefu ni zipi ni Changamoto za kutegemea

naomba kama unalolote la Kushare naomba unisaidie
 

Biashara Kuoza au Mali Kuoza. Kuna kipindi iliniangusha sana biashara ya viazi.​

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…