Biashara ya viazi mviringo

Biashara ya viazi mviringo

Jf sikuhizi imekua kama uwanja wa wivu wa kimaendeleo.
 
Salamu kwenu wadau,

Naomba kujulishwa kiundani juu ya biashara ya Viazi mviringo/ulaya kutoka Tarime kupeleka Mwanza. Moja ya Mambo muhimu ninayoomba kueleweshwa ni haya:-
-Misimu ya Viazi hivi ni miezi ipi?
-Gunia shambani ni sh. Ngapi?
-kusafirisha ni sh ngapi?
-ushuru tra ni sh ngapi?
-usafirishaji ni Wa namna gani?
-zipi changamoto hasa?
-kwa kila gunia ukiondoa kila gharama kuanzia kutoa shambani hadi Mwanza sokoni likiuzwa unaweza pata faida kiasi gani?
-mzigo unaweza isha baada ya muda gani ukishafika sokoni? Niishie hapa kwanza

Natumai nitapewa msaada na wazoefu Wa biashara hii,mana maisha magumu nataka nitumbukie na kwenye biashara hii kama ikiwezekana. Natanguliza shukurani ndugu zangu!
Mkuu huku Tarime labda uchukue ndizi ndo nyingi shambani mkungu Buku tatu mpaka tano

Viazi vipi lakini sio vingi sana ila bei yake cjajua ni ngapi kwa Gunia
 
Vile viazi havitoki Tarime, ni vya Kenya, sasa ukitaka ufanikiwe kwenye biashara hii fanya utafiti kwanza huko Mwanza bei viazi ipoje, wateja wakubwa lenga wauza chips ndio uende kule sirari upande wa Kenya kuchukua mzigo.
 
Ndugu wana JF habari ya majukum...?,Nianze na samahani kwa wale ambao watanielewa tofauti,
Mimi natamani kujihusisha na biashara ya viazi mvingo/nyanya maji kwa maana ya kununua aidha mbeya/njombe kisha niuze dar es salaam, Lakin ndugu wana JF bado sijafahamu wapi nianzie hivyo naomba ushauri juu ya biashara hii katika mambo yafuatayo
  • Je ni mtaji kiasi gani walau kwa kuanzia inaweza kutosha kwa maan ya kununua mzigo ,usafiri na ushuru mfano viazi mviringo niaze na gunia 50 /nyanya maji nianze na sanduku 50
  • Pia bei ya viazi mviringo kwa gunia ni kiasi gani au bei ya nyanya maji ni kiasi gani pia
  • Najuaje ikiwa nahitaji viazi mviringo/nyanya maji ambazo ni nzuri kwa mahitaji ya soko ukilinganisha zipo aina nyingi nyingi
  • je hapa dar es salaam napataje masoko kwa maana ni wapi ambapo soko lake limekaa vizuri hapa dar au zanzibar na vipi naweza kupata wateja?
  • Pia changa moto ya hii biashara yaani ni mambo yepi yapasa kujiepusha na yepi yapasa kuyazingatia
  • pia nakama yupo mtu mzoefu na biashara hizo naomba anitumie namba ili nizungumze naye kwa kina
  • Hivo ndugu wana JF naomba ushauri wenu ipi ni biashara nzuri katika viazi mvingo au nyanya maji na mambo niliyo tanguliza hapo juu
Mkuu je ulifanikiwa kulifanyia kazi hili wazo lako ?
 
Viazi safi kwa chakula kutoka Tukuyu vinauzwa, pia tunasafirisha Tanzania nzima.
Bei ya kiazi bila usafiri ni elfu arobaini kwa kipeto, safari inaanzia Mbeya wewe utalipia usafiri kutoka Mbeya jijini.
Bei ya usafirishaji inaanzia elfu 10 kipeto kwa safari za dar es Salaam.
Bei 40000 bila usafiri.
Karibuni PM na 0756254925
cbf5bf7265f7a966b5c9a7b449d5f04e.0.jpg
dd13ed58b51e2202374f8a7748ffec7c.0.jpg
 
Viazi safi kwa chakula kutoka Tukuyu vinauzwa, pia tunasafirisha Tanzania nzima.
Bei ya kiazi bila usafiri ni elfu arobaini kwa kipeto, safari inaanzia Mbeya wewe utalipia usafiri kutoka Mbeya jijini.
Bei ya usafirishaji inaanzia elfu 10 kipeto kwa safari za dar es Salaam.
Bei 40000 bila usafiri.
Karibuni PM na 0756254925
View attachment 1240011View attachment 1240012
Hizo bei za wapi? Na ni aina gani ya viazi, kwani bei za viazi zilizopo sokoni kwa sasa dar ni kuanzia 37,000-40,000 kwa bei ya jumla!!! Hapo mtu ameshavinunua, na kuvisafirisha hadi dar na ndio anauza kwa bei hiyo, sass hiyo bei yako hata siielewi, au ni aina gani labda ya viazi tofauti na tigoni, obama?
 
Hiyo bei ya Mwezi wa 8 mpaka 9 mwanzoni, sasa hivi Obama haipo ndomana tumepandisha bei. Mwaka jana bei ilikua sh ngapi muda huu? Tunauza Obama ya stock.
 
Kwa mwaka jana kipindi kama hiki viazi kwa dar bei ilikuwa 58,000 ikaja kupanda hadi 70,000!!hiyo bei ninayokuambia hadi leo hii kwa soko la mbagala ndio iliyopo mkuu, obama ni 40,000-42000, kwa sasa bei hiyo kwa dar haipo, Juzi kuna jamaa aliweka uzi humu yupo huko mbeya obama anauza 20,000 akatoa mchanganuo hadi kufika dar ni kama 33,000!!huyo yupo sawa mtu akiuza 40,000 anapata. Ndio maana hiyo bei yako imenishutua au unaposema kipeto una manisha nini?? Nijuavyo mimi kipeto ni kile kigunia kimoja kama kinavyoonekana kwenye gari hapo!! Au una manisha vikiwa viwili ndio bei hiyo?!!
 
Hizo bei za wapi? Na ni aina gani ya viazi, kwani bei za viazi zilizopo sokoni kwa sasa dar ni kuanzia 37,000-40,000 kwa bei ya jumla!!! Hapo mtu ameshavinunua, na kuvisafirisha hadi dar na ndio anauza kwa bei hiyo, sass hiyo bei yako hata siielewi, au ni aina gani labda ya viazi tofauti na tigoni, obama?

Kwa mwaka jana kipindi kama hiki viazi kwa dar bei ilikuwa 58,000 ikaja kupanda hadi 70,000!!hiyo bei ninayokuambia hadi leo hii kwa soko la mbagala ndio iliyopo mkuu, obama ni 40,000-42000, kwa sasa bei hiyo kwa dar haipo, Juzi kuna jamaa aliweka uzi humu yupo huko mbeya obama anauza 20,000 akatoa mchanganuo hadi kufika dar ni kama 33,000!!huyo yupo sawa mtu akiuza 40,000 anapata. Ndio maana hiyo bei yako imenishutua au unaposema kipeto una manisha nini?? Nijuavyo mimi kipeto ni kile kigunia kimoja kama kinavyoonekana kwenye gari hapo!! Au una manisha vikiwa viwili ndio bei hiyo?!!
Ungemuuliza anauza kiazi gani, kipeto hicho hicho kimoja! Obama haipo mkuu, nilionayo mimi ni hazina ilikua inasubiria soko. Sasa hivi kiding'a inaisha isha na tigo nayo inaelekea kuisha so obama ina bei, kuna jamaa hapa bila 42 hauzi Obama nae ana hazina.
 
Kwa mwaka jana kipindi kama hiki viazi kwa dar bei ilikuwa 58,000 ikaja kupanda hadi 70,000!!hiyo bei ninayokuambia hadi leo hii kwa soko la mbagala ndio iliyopo mkuu, obama ni 40,000-42000, kwa sasa bei hiyo kwa dar haipo, Juzi kuna jamaa aliweka uzi humu yupo huko mbeya obama anauza 20,000 akatoa mchanganuo hadi kufika dar ni kama 33,000!!huyo yupo sawa mtu akiuza 40,000 anapata. Ndio maana hiyo bei yako imenishutua au unaposema kipeto una manisha nini?? Nijuavyo mimi kipeto ni kile kigunia kimoja kama kinavyoonekana kwenye gari hapo!! Au una manisha vikiwa viwili ndio bei hiyo?!!
Dar kipeto moja usafiri ni 10000 tu
 
nimetoka kununua hapo soko la mabibo muda huu..Obama kipeto moja ni elfu 9 tu mkuu.
 
Dar kipeto moja usafiri ni 10000 tu
Huyo amechangana hiyo ni bei ya ndoo!! Mimi ninapokuambia hadi leo soko la viazi(obama) hapo mbagala hadi 40,000(kipeto)wanauza,tigoni ni 37,000!!!!any hapo sijui inakuwaje na kwa sasa viazi sokoni ni vingi, KILA RAHELI MKUU KWENYE BIASHARA YAKO.
 
Shukrani, karibu nawewe ulime nna plot nauza ya vipeto 12 guaranteed au zaidi kutokana na wingi wa mbolea mil 2 na laki 2
 
Back
Top Bottom