Biashara ya viazi mviringo

Biashara ya viazi mviringo

Morogoro sehemu gani wanalima viazi..?
Wilaya ya mnvomero hasa maeneo ya mgeta ni maarufu kwa kilimo vikiwemo viazi mviringo,unaweza ukaenda huko au unaweza kwenda pale soko la morogoro mjini stendi ya SUA huwa kuna wafanya biashara wa viazi mviringo huleta pale ila huenda ukapata bei kidogo endapo wamevitoa mbeya au njombe.
 
Habari.
Natafuta soko la viazi mviringo kwa mkoa dar,morogor na singida tafadhali kama kuna mnunuzi naomba nitafute no:0743185408
 
Mimi nimefanya hii biashara, naijua vizur sana ni biashara nzuri sana, nilisimama kwa muda kutokana na kubanwa na masomo nategemea kurudi kwenye hii biashara mwezi wa kumi mwaka huu, kwa laki 8 kweli ni ndogo mkuu atleast uwe na kama 3milion ndoo utaona faida ya hii biashara

Kwani gari ya chini huwa n fuso yenye uwezo wa kubeba magunia 75 kujaza mzigo siyo pungufu ya 2.4m ni bora ufanye ivo kuchukua gari yako kuliko kushare maana itakugharimu sana kwenye usafirishaji

Nakaribisha tuungane mkuu kama kuna swali waitaji kujua waweza kuuliza apa apa ntakujibi
Kwani usafiri kutoka njombe mpaka dar kwa gunia moja nauli shilling ngapi kwa fuso
 
Jamani mliofanya hii biashara tunaomba mtupe mrejesho....nyinyi ndo mabalozi wetu
 
Bro! Naweza kuonana nawe ili tuongee zaidi! Pls ni PM. Nimekuwa natafuta data za hii biashara na nijue mahala pa kuanzia!
Sijui kwanini nimehisi utaibiwa na huyu mtu ila let me ignore my intuition
 
Soko lipo vizuri, kama unavyoona watu kila siku wanazidi kupenda chips na matumizi ya viazi yanaongezeka cha muhimu ni uchaguzi mzuri wa viaz kule shamban, hakikisha unachagua kiaz kizuri na kiwe kikubwa soko zuri ni buguruni na mabibo ilala siyo wazuri sana
Kuhusu usafiri kama unachukua mzigo njombe kulee kuna shida kidogo ya usafiri lakini tofauti na mbeya usafiri hausumbui sana maana semi tyler nyinyi zinatoka zambia kuja dar zingine zinakuwa tupu soo deal kaa izo hawawez kuacha
Mimi nipo ndagha apa vinaplimwa viaz Na nna Lima kidogo ila hua nataman kuuzia dar kwa kununua vingne tatzo sjui bei Na soko la huko zao lingne ni ndizi Toka tukuyu nazo znalipa
 
Mimi nipo ndagha apa vinaplimwa viaz Na nna Lima kidogo ila hua nataman kuuzia dar kwa kununua vingne tatzo sjui bei Na soko la huko zao lingne ni ndizi Toka tukuyu nazo znalipa
Dagha iko wapi?,usafiri huko ukoje?
 
Salamu kwenu wadau,

Naomba kujulishwa kiundani juu ya biashara ya Viazi mviringo/ulaya kutoka Tarime kupeleka Mwanza. Moja ya Mambo muhimu ninayoomba kueleweshwa ni haya:-
-Misimu ya Viazi hivi ni miezi ipi?
-Gunia shambani ni sh. Ngapi?
-kusafirisha ni sh ngapi?
-ushuru tra ni sh ngapi?
-usafirishaji ni Wa namna gani?
-zipi changamoto hasa?
-kwa kila gunia ukiondoa kila gharama kuanzia kutoa shambani hadi Mwanza sokoni likiuzwa unaweza pata faida kiasi gani?
-mzigo unaweza isha baada ya muda gani ukishafika sokoni? Niishie hapa kwanza

Natumai nitapewa msaada na wazoefu Wa biashara hii,mana maisha magumu nataka nitumbukie na kwenye biashara hii kama ikiwezekana. Natanguliza shukurani ndugu zangu!
 
Back
Top Bottom