Ninapenda kumrecommend huyu mtaalamu wa kutengeneza website kwa moyo wote. Nilimpa kazi ya kutengeneza website yetu, na kwa kweli amefanya kazi ya kiwango cha juu na kuzidi matarajio yangu.
Kabla ya kuanza kazi sikuwa na wasiwasi hata kidogo wa kulipa advance, kwa sababu nilithibitisha kuwa tayari alikuwa amefanya kazi na taasisi mbili ninazozifahamu, na nilipata ushuhuda mzuri kuhusu uaminifu na ubora wa kazi yake.
Kitu kingine kilichonivutia ni mawasiliano yake. Anafanya kazi kwa wakati, anajibu simu na ujumbe kwa haraka, na akiona umempigia simu hajapata nafasi ya kupokea, anakurudia kwa nidhamu na weledi wa hali ya juu. Hilo ni jambo ambalo si rahisi kulipata siku hizi.
Ingawa yupo mbali ushirikiano wetu ulikuwa mzuri sana kana kwamba tulikuwa sehemu moja. Kila alichoahidi alikitekeleza, na website ilikamilika ndani ya muda tuliokubaliana bila usumbufu wowote.
Kwa yeyote anayehitaji website ya biashara, kampuni, taasisi au shirika, ninamrecommend kwa asilimia 100. Utapata huduma ya kitaalamu, mawasiliano bora, uaminifu, na kazi yenye ubora wa hali ya juu.
Asante sana kwa huduma yako bora, na Mungu azidi kubariki kazi ya mikono yako.