Biashara yangu imedoda, nimekosea wapi na nini kifanyike kuiimarisha?

Biashara yangu imedoda, nimekosea wapi na nini kifanyike kuiimarisha?

Habari wakuu!

Nimefungua biashara ndogo ya mtaji wa kama 7.5m hivi. Biashara nimeifungua rasmi Jumatatu ya week hii.

Biashara yangu inadeal na uuzaji wa vitu kama battery za magari, oil na matairi ya magari.

Location ya biashara iko eneo zuri tu la barabarani na uzuri zaidi eneo limechangamka sana tu.

Lakini cha kusikitisha toka niifungue hii biashara yapata siku tano zilizopita nimeuza only 3 items, mfano jana sijauza kitu kabisa.

So niko dilemma, Je nimepotea njia au tatizo ni nini wakuu au ni hali ya kawaida kwa biashara mpya?
Nitakuuliza swali taff kdg... Wakat unafkiria kuanzisha biashara ni njia gan ambayo ni 'game changer' uliifikiria ilikuongeza / kufanya mauzo, I mean kuna kitu gani cha kitofauti ktk utoaji wako wa huduma ambacho knakutofautisha na wengine sokoni. Sabab ukumbuke km alivyosema mdau hapo kuna wenzako nao wapo kwny laini hyo hyo pia ya biashara tena wapo kwny game kabla yako!.
 
Mkuu mm nina biashara ina mwaka na miezi 7 sasa, lkn nimeanza kuona faida baada ya mwaka mzima, na kila mwezi faida inaongezeka. Kitu cha kwanza vuta wateja, usijar sana kuhusu hasara, maana unaweza anza biashara ukapata hasara mwezi wa kwanza usikate tamaa. Endelea baada ya miaka miwili utafurahia show.
 
Jaribu pia kucheza na mafundi garage , ili ujipatie wateja kupitia wao

Pili Weka punguzo la bei kwa bidhaa zako ili uvute wateja mpka utakapohakikisha sasa inatosha then pandisha bei iwe kama wenzako

Tatu,vumilia mkuu bado biashara haijachanganya kwa maana mauzo ya siku ,huwez fungua biashara wiki hyohyo then uuze sanaa kama ingekuwa hvyo watu wasinge ajiriwa . kumbuka wakat COCA- COLA wanaanza bongo waliuza soda 3 mwezi mzima

Kama nimekosea watanirekebisha ila yangu ni hayo
Sio coca cola ya Tanzania ni coca-cola ya huko ulaya ilipoanzia hiyo kampuni.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mwenzio sijaona sehemu ambayo jamaa kasema anaitegemea kwa kila kitu. Labda unisaidie
Bado mapema sana Kaka Wacha pressure
Tatizo hiyo biashara unaitegemea Kwa mahitaji yako ya Kila siku ndio maana unaumiza kichwa kitu ambacho ni hatari
Jaribu kurelax.
 
Habari wakuu!

Nimefungua biashara ndogo ya mtaji wa kama 7.5m hivi. Biashara nimeifungua rasmi Jumatatu ya week hii.

Biashara yangu inadeal na uuzaji wa vitu kama battery za magari, oil na matairi ya magari.

Location ya biashara iko eneo zuri tu la barabarani na uzuri zaidi eneo limechangamka sana tu.

Lakini cha kusikitisha toka niifungue hii biashara yapata siku tano zilizopita nimeuza only 3 items, mfano jana sijauza kitu kabisa.

So niko dilemma, Je nimepotea njia au tatizo ni nini wakuu au ni hali ya kawaida kwa biashara mpya?

kaka biashara wiki tu ushaanza kupiga kelele.. utatoboa mwez wewe.. anaeruhusiwa kuwa na wasiwasi kwenye biashara kwa kila dakika inayopita ni muuza vyakula tu ambapo kila dakika inayopita bila mteja kuja kula ndo risk ya chakula kubaki na kuharibika ni kubwa

lakin kama bidhaa zako hata zikae mwaka haziharibik ww unaanza kulalamika tena ndo kwanza una wiki ambapo watu hawajazoe kuwa umefungua duka la bidhaa za aina hiyo ..

au ndo unategemea kula yako na familia itoke hapo?.. kama ni hivyo nakushaur tafuta njia mbadala haraka la sivyo utafunga biashara sababu utakopa sana na hakutakuwa na uwiano kati ya mikopo na kipato

kawaida kama una plan ya kufungua biashara ya 5m hakikisha walau una 8m to 10m.. biashara ni kama Engine za gari au jenerera za zaman hadi uzungushe kile chuma injini ipate mwendo ndo iweze kujiendesha so unatakiwa uwe na nguvu za kutosha kuzungusha injin had ishike kas la sivyo Engine haiamki
 
Back
Top Bottom