Biashara yangu inaniingizia faida ya Tsh. 200,000 kila mwezi; Je, Niiache niende chuo?

Dogo acha upumbavu. .iyo pesa ya kulipa ada ni bora ukazungusha kwenye biashara ili kukuza mtaji. Achana na mawazo ya kurudi chuo sasa hivi. Uko utawanufaisha watu wengine tu kwa kulipa ada ..elimu ni ya kukariri sana ili ufaulu mtihani, wengine tunajuta ata kwann tulisoma...kazana na biashara futa kabisa wazo la kusoma kama ulivyofuta mwanzo ..

Shukuru hata ulikosa mkopo, leo usingekuwa na hiyo biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm ni mwanachuo mpaka mda huu ila ndoto zang zte n napigana juu chini nifike angalau hapo ulipo,
Uku akuna dili n lebo 2
 
biashara gan mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
Nakushauri tafuta kozi usome lakini kozi ambayo itakusaidia kujiajiri baada ya shule somea kitu unachotaka kufanya ikiwezekana. Kwa mtu anae angalia mbali faida ya laki 2 kwa mwezi ni ndogo sana kukufanya kuachana na elimu. Kumbuka pia kuna umri wa kusoma kirahisi japo chuo kipo tu ukikaa miaka 5/6 mtaani kusoma tena itakuwia ngumu sana maana utajiona nje ya mazingira (hauto fit in). Muda ni sasa fuata moyo wako, never give up on your dream.

Ukienda shule tayari ukiwa na malengo yakujiajiri utafanikiwa sana utaacha kuwaza biashara ya kutembeza maji (no disrespect ni mfano tu) na utawaza kufungua kampuni ya kuingizia mil 15 kwa mwezi (mfano). Utaona laki 2 kwa mwezi ni pesa ndogo sana ukiwa unaangalia bigger picture.

Walio wengi wanasoma kwa kufuata ajira na kwa kozi ipi ina mkopo ndio maana wanapata taabu baada ya kumaliza.
 

aha ha habha habha duuu
 
Ni biashara gani mkuu?


Okay, ASANTE kwa ushauri ngoja tusubiri mawazo ya wengine pia tuamue kwa pamoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Depend na wewe una malengo gani na chuo unataka ukasomee nini na ni biashara gani unaifanya so far.
Niliacha kazi ya sales kwenye kampuni kubwa tu yenye salary nzuri na commission kubwa tu nikaenda kusoma kitu ambacho kitanifanya niajiliwe na nijiajiri. Mpaka muda huu nashukuru kwenda kusoma maana ninachoingiza kwa mwezi ni zaidi ya mara tatu ya kabla sijaenda kusoma na bado sijaridhika soon kabla huu mwaka haujaisha nitaanza kuingiza mara sita ya nilichokua nalipwa.
Fuata moyo wako soma ambacho kwako unaona kina faida wengi wanaolia walisomea vitu kufuata mkumbo bila kusoma hata ramani ya ajira au kujiajiri akimaliza chuo itakuaje (samahani kwa nitakaowakwaza ila ukweli ndio umuweka mtu huru).
Ukienda kusoma ikiwa unajua unataka kufanya nini baada ya kuhitimu basi utafanya vizuri sana chuoni na utafaulu vyema sana huenda leo unapata hiyo laki mbili faida baada ya kusumbuka sana ila ukaenda chuo ukapata milioni faida ya bila kuumiza kichwa sana.
Jiandae tu chuoni kuna mateso na kuna kuvumilia kunahitajika sana maana kuna muda unaweza jisikia kuacha chuo but komaa mpaka lengo litimie
 
kijana tuambie basi biashara gani wafanya weye?
Labda ungeuliza ufanye biashara gani,(kama hufanyi lakini) inayoendana na mazingira unayoishi na kiwango chako cha mtaji pesa.
 
true say,ila watanzania tulio wengi ubongo wetu unachelewa kukua,hivi haya uliyoyaandika mtu anayetaka kwenda kusoma sasahivi hayaelewi kabisa,ila baada ya miaka 4-10 ndo atayaelewa!
 
true say,ila watanzania tulio wengi ubongo wetu unachelewa kukua,hivi haya uliyoyaandika mtu anayetaka kwenda kusoma sasahivi hayaelewi kabisa,ila baada ya miaka 4-10 ndo atayaelewa!

Hakika mimi nilipomaliza form six kwakweli sikua na hamu ya kusoma nikatafuta kwanza ajira nikafanya kwa miaka kama mitano,nikajifunza mengi nilipokwenda chuoni nikajua nafuata nini na kipi kipo mtaani.
Nimefundisha,nimeongoza taasisi binafsi na nikafanya sales zote zikanijenga na nikaenda kusomea kilimo. So kutazama unataka kufanya nini ukitoka chuo ni muhimu zaidi,kama uko A level muda wa likizo tafiti sana kuliko kujiona uko juu sababu u mwanafunzi na wengine wa mtaani hawana akili.
 
Reactions: 365
Uko vizuri sana,

Ila wazazi walio wengi ni mazwazwa lazima tukubali hili.

Juzi kuna dogo kamaliza form four,nikawashauri wazazi kwamba hii ada ya milioni 2.5 ambayo mnataka mkalipie advance,mlipien chuo cha compyuta akasomee coding na programing maana uchumi na kizazi cha leo kinategemea technology! Halafu dogo ni balaa kwenye hesabu.wazazi wake wakaniona eti nina nia mbaya na mtoto wao...sasa nimewaacha ameenda kusoma st nini,ila nina uhakika baada miaka 5,lazima watapiga kelele sana
 
200,000 ni net profit after all expenses.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pamoja na gharama Za manunuzi Au siyo ? Je biashara hiyo inamuda gani ianze? Na hicho kiwango cha faida Kwa mwezi umekuwa ukikipata Kwa miezi mingapi mfululizo? What is the nature of your business ? Je unalipa kodi stahiki Kwa kila mamlaka husika Kwa wakati ? Je mtaji wa biashara yako ni kiasi gani ? (Net wealth) , Je una mkopo wowote? Je unajaribu kuona uwezekano wa biashara yako kuwa endelevu? Je hakuna viashiria / dalili ambazo zaweza Shaka uwezekano wa biashara yako kuendelea? (Going concern symptoms ) , Je Kwenye hiyo faida umejilipa Mshahara Kwa ku assume kuwa Kama ungeajiri Mtu ungepaswa kulipa? Naomba ujibu hayo machache kwanza Kisha ndo nitakushauri uende Chuo Au usiende Kwa sasa Au ufanye vyote viwili.
 
Labda ungeuliza ufanye biashara gani,(kama hufanyi lakini) inayoendana na mazingira unayoishi na kiwango chako cha mtaji pesa.

we nambie tu hiyo yako. hata pm niambie huko.
 
....great great thinking!
..na mjadala ungeanzia hapa!
 
Ningekuwa mimi hiyo Chuo kikuu tupa mbali kabisa. Elimu uliyo nayo inatosha kabisa kufanya biashara yako. Maana wengi wetu tulio soma tuliosoma huko tumeishia kupoteza muda tu na kuwa waoga zaidi wa maisha. Kuza biashara yako tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…