Biashara yangu inaniingizia faida ya Tsh. 200,000 kila mwezi; Je, Niiache niende chuo?

Biashara yangu inaniingizia faida ya Tsh. 200,000 kila mwezi; Je, Niiache niende chuo?

Biashara inayokuingizia faida ya laki 2 ni ndogo sana
 
University ni hiyo biashara yako dont get twisted,hiyo ada ulinayo igeuze mtaji kisha fungua project nyingine...chuoni hamna kitu kule...kama ni kupata elimu utakua unasoma online ukiwa kwenye mambo yako,vitabu vyote vinavyotumika vyuoni viko kwenye mtandao tena bure.
Aniulize mimi ni shahidi, mwaka wa nne huu naiskia ajira kwenye bomba, afadhali yake aliyewaza mapema, maana si wengine nataman zile ada na pocket money ziwe mtaji kwa sasa... Lakin ndio ivo haiwezekan, imebaki degree jina tuu nothing special.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama still biashara inakulipa fanya kwanza biashara zen jiimalishe mwenyewe kwa kila kitu kinachokuzunguka zen kabla hujaanza kusona mtafute mtu ukae nae kwny biashara umuone km anifit , akiifit biashara sasa hapo unaweza kumuachia biashara zen ukaendelea na masomo kama kawaida bila wasi wasi coz kuna maisha baada ya kumaliza chuo tena ya msoto coz ajila adimu xana mtaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chuo unafuata nini? Mademu,modules,birthday party,bash au unawaza itakuwa rahisi kuajiriwa? Mi nadhani kiasi ulichonacho ndio PHD ya kukufanya uwe na maisha mazuri! Kuza mtaji wako na ongeza thamani katika biashara yako mkuu! Chuo kipo tu! utasoma kwa amani pale maisha yako yatakapokuwa stable! Huko chuo kwenyewe kila siku wanatoa seminars kuhusu kujiajiri! Fanya biashara! Nimepita chuo na nimeona chuo ni kupoteza muda tu! Sababu elimu yetu haipo katika misingi ya kutufanya tujitegemee baada ya kuhitimu!
Umeongea point mkuu sometm ukikaa ukitafakar mdaa uliotumia kusoma mpka chuo umemaliza na bado pengine ujapat kaz unaona ni bora huo mdaa ulio utumia chuo ungekua umejiajir au unapamban ungekua mbali sana ijapokuwa elimu ni muhimu ila kwa tz ytu bado sanaa
Na ambaye ajafika uko anatamani sana na pengine anaweza kuona kama unampigia propagand ila ni true hakuna jipyaa tena wenyew ndo wanatupa elimu ya ujasiriamali
Mm naona angepambna biashara yake iwe zaidi ya hapo kusoma hata online ama open universty
 
Wakuu habari zenu,. Mwaka 2014 nilihitimu kidato ya sita shule mojawapo nchini, nikafanya application kuingia chuo kikuu nikachaguliwa kwenda kusoma course ya uchumi pale udsm.

Kwa bahati mbaya sikupata mkopo kutoka HESLB kwa ajili ya kuniwezesha kupata elimu hiyo ya juu,

Nikatazama nyuma na mbele nikagundua sina support kutokana na umasikini uliokithili ndani ya familia yangu,

Baada ya hapo nikachukua maamzi magum, nikasafiri kutoka mkoani mpaka jijini na nikafuta na kufuta kabisa mawazo ya hiyo elimu ya chuo kikuu kwanza kwenye ubongo wangu.

Mawazo yangu na bongo langu nikahamishia kwenye neno "ajira" nikaanza kutembeza bahasha la vyeti vyangu ya secondary kutafuta ajira hapa mjini, hata hivyo sikuweze kupata ajira baada ya kuzunguka sana na bahasha hapa jijini,. Baada ya changamoto hiyo ikanifundisha tena kubadili mawazo kutoka kutafuta ajira mpaka kutafuta "mtaji" ili nijiajiri, nikiwaza ni jinsi gani niachane na suala la kutembeza bahasha kila ofisi naonekana kama bango,

nikaamua kukusanya kamtaji kwa kuanzia na kale kale ambako nilikuwa nazunguka nako kutafuta ajira nikapiga vibarua vya hapa na pale, nikasaidia sana mafundi site mbalimbali, nikapata kamtaji, nikaachana kwanza na vibarua nikaanzisha biashara fulani.

kwa sasa biashara yangu hiyo inanilipa faida tasilimu ya shilingi laki mbili kila mwezi, na mpaka dakika hii nimeweza kukusanya ada ya kuweza kujilipia university nchini.,

Je niende chuo au niendelee na biashara yangu hii.

NB nikimuachia mtu kuisimamia hii business lazima ife ndani ya muda mfupi sana maana inahitaji kujitoa sana. Japo kulingana na hela niliyonayo cash lazima chuo nimalize bila wasiwasi kabisa..

Naombeni ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
Stori kibaaaao hujaandika hata ni biashara gani!
 
517c750015709ec44941c9922bb9230c.jpg

Dogo komaa kitaa na biashara Mzee Bahkresa na utajiri wake ni std 4 !
 
SHAMAC Hebu shauri mdau hapa. Mimi Niko sorted na bado nakusanya formal and informal education. Sasa maana yangu YA kusema atafute shule ni kuwa itamuongezea uwezo wa kukabiliana na changamoto (confidence pia).

Mshawishi kwa Nini asiende chuo? Hizi matambo zetu za ku-define elimu zitamkonfyuzi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
UKO SAHIHI SANA
 
Back
Top Bottom