Biashara za kufanya kwa mtaji mdogo wa elfu 10 mpaka 50

[emoji109]
 
nimeiona kwa jamaa yangu haishiwi elfu kumi hata siku moja anauza maji ya kufunga
 
ILA KWELI AISEE...NGOJA NIFIKIRISHE AKILI ZAIDI 10-50K HUWA NAZIPOTEZAGA KIZEMBE SANA KUMBE NAWEZA KUFANYIA BIASHARA
 
Ila huu ni ukweli vijana wengi tunawaonea aibu watu naam hapa umeongelea mpka sisi vijana masharo duh hili liuzi limenigusa --- asante dada naamini hata mm nitaleta uzi lkn mwisho wa mwaka .... ..
 
[emoji23][emoji23][emoji23] nimeona huu uzi nimekumbuka mbali..nakumbuka mimi na mdogo wangu tulikua tunapiga mishe za icecream..yeye kazi yake ilikua kwenda kununua ubuyu..analeta home natengeneza icecream zikishaganda akirudi shule anapeleka kuna sehemu ilikua ya pooltable..aisee tulikua tunauza mno..na enzi zile icecream sh 10 na 20 dah..ila pesa zenyewe zilikua zinaishia kwenye chips tu..tukiwa na hamu na chps tunachukua mwsho mtaji ukafa.
 
Chuo nliwekaga usistaduu pembeni..mimi na rafiki yangu tulikua tunauza kachori..tunatengeneza na pilipili tam hatari..tunatembezea majirani na hostel tulipiga sana pesa..biashara ndondogo mwanzo wa mafanikio
 
Hivi machine za kukamulia juice ya miwa zinapatikana wapi ?, mimi nipo mbeya wilaya ya kyela.
 
Asante sana
 
Wakuu habari za Leo

Nimekuwa nikihangaika kuwainua kiuchumi wanawake katika jamii yangu inayonizunguka.
Baada ya kufanya utafiti Wangu usio rasmi, niliona bora nianze na vicoba. Hii itawasaidia kupata mtaji kwa kiasi Fulani.

Nashukuru Mungu hili limefanikiwa. Tumeweza kuazisha vocoba, ambapo tunanunua hisa moja kwa sh. 2,000 .

Tumeanza kukopeshana hadi 40,000 kwa wenye Biashara ndogo wapo wauza barafu, ice cream, samaki na maandazi.

Tatizo ni kwamba kuna baadhi hawana Biashara, lakini wana hamu ya kufanya Biashara. Nifanyeje kiwasaidia?

Jana nilisoma Uzi mmoja Wa idea za Biashara, nikauelewa vizuri tuu, kwamba tuangalie bidhaa zenye uraibu. Hii ni sawa.

Sasa naomba mnisaidie idea za Biashara ndogo, zenye mtaji chini ya 50,000 plss nahitaji kuwasaidia wanawake wenzangu plsss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…