Biashara za mitandao (kuunganishana) zinavyowaliza first year vyuoni

Biashara za mitandao (kuunganishana) zinavyowaliza first year vyuoni

Habari, karibu ndugu msomaji Leo tutaangazia kwa uchache namna biashara za kuunganishana ( biashara za mitandaoni kama wanavyoziita wao)
Hizi sio zile zakuuza bidhaa online kama wafanyavyo Al-Baba, Amazon, E-bay au jumia Bali hizi nizamifumo ya kuunganishana na zitakuwa pyramid in shape yani nikijiunga Mimi nakushawishi na wewe unajiunga chini yangu.

Kwa baadhi ya nchi ni haziruhusiwi na niharamu, kama ilivyo kwa michezo ya kubahatisha, na hata matangazo yake hayaruhusiwi kutangazwa katika vitengo vya matangazo ya mitandao mikubwa kama Facebook ads na google AdWords.

Unachotakiwa kufanya nikujiunga na kisha kutafuta watu wakujiunga chini yako na Mara nyingi kiasi cha kujiunga huwa nikikubwa hadi kufikia 600,000+

Ukishajiunga unaanza kuhangaika kutafuta watu wakuwaunganisha na kuwadanganya kama ulivyo danganganywa. Simaanishi kuwa ni utapeli Bali ni mfumo mgumu na unaoumiza na unaendeshwa kwa uongo yani nilazima udanganye ili upate wafuasi mfano " nimejiunga Nina wiki mbili maisha yangu yamebadilika kabisa na hapo umevaa suti yakuazima na hujui Utakuta nini maana siwashachomoka na na Laki zako haha!

Sasa hawa jamaa wamejikita sana vyuoni na kuwasubiri wale mwaka wakwanza ili kuwaingiza mkenge na kuwaacha wakilia.
Ushawishi mkubwa hutumika kuwadanganya Bila kueleza wazi ugumu wa mfumo.

Watakwambia baada ya mwezi utanunua gari. Haha!

Na mengineyo mengi kukutamanisha. Ukisha jiunga sasa ndio utaanza kuonja joto yajiwe.

Wito kwa watanzania
Anayekushawishi kujiunga na kitu chochote mwambie akwambie madhara yake tuu faida utazipata kwa kutafuta taarifa zingine wewe mwenyewe.

Namshukuru sana padri simplis wa france, maana Mimi nilishawishiwa kidogo niingie mkenge lakini Huyu father alinieleza hii ni black market na anayefanikiwa ni yule wa mwanzo( jaribu kuchora pyramid utaelewa nachoeleza)

Wito kwa serikali.

Hizi biashara zinapaswa kuundiwa bodi ya udhibiti kama ilivyo betting Tena pengine yenye nguvu zaidi

Onyo Kwako usisikie maneno kuwa " Nina project nahitaji watu 20 wanafanya nao kazi hahaha! Au kuna project sijui ikishirikiana na nmb

Fanya real business utafanikiwa
Kwaheri
Share ujumbe kwa watu wako wanguvu.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120] Somo zuri na ubalikiwe kwa kweli.
 
Hiyo ni kama chen hapo mtoto kakosa wa kumuunga ili nayeye aneemeke, hivyo anawatumia wazazi kama chambo wakijiunga tu yeye nae ataanza kupata kifuta jasho kupitia wazazi, shughuli inabaki kwa wazazi nao watafute watu wajiunge ili na wao waweze kupata kifuta jasho....
Inamaana mtoto atafaidika? Kwamba itamlipa zaidi ya pesa aliyopewa na wazazi kuwekeza
 
Hawa forever living mpaka leo sijawapatia kundi la kuwaweka, walimrubuni dada mmoja akajiunga nao na katika kutapatapa akataka aniweke na mimi ila inashindikana.

Akampata kijana mmoja akamlaghai kisha akamuunganisha kwa bahati mbaya zaidi huyo dada aliacha chuo akiwa mwaka wa pili na huyo kijana aliacha akiwa mwaka wa kwanza kwa lengo la kupanua wigo wa biashara nchi nzima wakati walikuwa wakijinasibu kuwa ni online business.

Ngoja nisiseme mengi ila Mungu awasaidie sana!
Ila kuna watu wana dhambi jamani vip sasa maisha yaliendaje baada ya kuacha chuo.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120] Somo zuri na ubalikiwe kwa kweli.
Hii kitu ni wengi wanakutana nayo na unakutwa hawana Elimu vizuri kuhusu hizi biashara. Mimi ilinichukua takribani mwezi kuielewa Alliance, maana alie taka kuniingiza kingi kuna baadhi ya mambo hakutaka kuwa wazi hadi niwe nimejiunga.

Hapo ndipo nilipo pata alama ya kuuliza.
Nakuanza kuifuatilia kwa kina.

Hizi biashara si zakuingia kichwa kichwa.
 
Inamaana mtoto atafaidika? Kwamba itamlipa zaidi ya pesa aliyopewa na wazazi kuwekeza
Hapana hatopata pesa zaidi ya ile aliyo peleka kama kiingilio bali kuna asilimia flan ataipata kupitia hao wateja alio waleta so ili iwe endelevu itamlazimu yeye aendelee kuongeza watu na wale wanao ongezwa nao waongeze watu hapo huyo dogo ndio atanufaika, hii ni experience ya alliance ila kampuni zote hizo ni kama zinafanana mifumo.
 
Hii kitu ni wengi wanakutana nayo na unakutwa hawana Elimu vizuri kuhusu hizi biashara. Mimi ilinichukua takribani mwezi kuielewa Alliance, maana alie taka kujiingiza kingi kuna baadhi ya mambo hakutaka kuwa wazi hadi niwe nimejiunga.

Hapo ndipo nilipo pata alama ya kuuliza.
Nakuanza kuifuatilia kwa kina.

Hizi biashara si zakuingia kichwa kichwa.
Funguka zaidi mkuu kwa faida ya jamii pana zaidi
 
Hapana hatopata pesa zaidi ya ile aliyo peleka kama kiingilio bali kuna asilimia flan ataipata kupitia hao wateja alio waleta so ili iwe endelevu itamlazimu yeye aendelee kuongeza watu na wale wanao ongezwa nao waongeze watu hapo huyo dogo ndio atanufaika, hii ni experience ya alliance ila kampuni zote hizo ni kama zinafanana mifumo.
Kwamaana hiyo kama wazazi wamelipa 5m. mtoto atazipata zote kwa kulipwa kidogokidogo?
 
Mbona serikali inawasajili na wana operate kisheria? Mi wale jamaa wa mikocheni opposite na KFC walitaka kuniingiza cha kike thro my friend from Asia huwa najiuliza govt haijui?
Wanalipa hela ndefu Sana serikali, Maghufuli anavyopenda hela asingewaacha salama...wanampa huge amount so cash
 
Kwamaana hiyo kama wazazi wamelipa 5m. mtoto atazipata zote kwa kulipwa kidogokidogo?
Kwa qnet kidogo napata kigugumizi, sababu aliyetaka kuni unganisha hakuwa muwazi sana. Ila alliance nilielezwa kwa kina.

Kama utahitaji maelezo labda nikuunganishe na huyo jamaa ambae yeye tayari ni member wa qnet labda waweza ng'amua jinsi inavyo fanya kazi ukimdadisi vizuri.

Kwa hapa jukwaani sina hakika kama yupo atakae funguka vizuri kuhusu hizi biashara. Maana wengi wao huwa sio wawazi sana. Sentensi yao kuu ni kwamba uende ofisi zao zilipo ili kupata maelezo zaidi. Na ukifika narudia ukiwa na tamaa basi waweza jitosa maana jamaa wanaushawishi mkubwa.

Hata mtoa mada ameeleza hapo kuwa sio utapeli ila ukishatoa pesa,ili wewe upate pesa basi utahitaji kufanya juhudi kubwa, yani kila mtu kwako utamuona ni fursa.

Experience niliipata kwa hawa Alliance in motion.
 
Mkuu unaweza kuelezea zaidi kuhusu Qnet? Kuna mtoto wa sister anawasumbua sana wazazi wake wajiunge na entrance fee ni 5m.

Baba ya mtoto(shemeji yangu) kaniuliza kama naijua na wanapataje pesa bahati mbaya sina ninalolijua kuhusu hiyo biashara. Wasiwasi wa shemeji yangu ni kwamba huo ni utapeli na mwanaye anashauriwa vibaya na kutumiwa na hao wenye biashara

Ajabu ni kwamba my sister anaelekea kuingia king maana ameanza ku side na mtoto kumshawishi baba yake wajaribu kum support binti aingie labda ni kweli kuna faida

Nilichokiona na kuwashauri ni kwamba hata wao wazazi hawajaelewa hiyo biashara inaendaje na watapataje faida? Kwahiyo wakikishe wanaelewa kwanza kabda ya kuingiza pesa yoyote huko
Mkuu daah wambie wakae mbali, tatizo linakuja kwenye kumuunga mtu, Kwanza kumpata wa kumuunga ni kimbembe , wengine mpak wanaroga ili kuwaingiza kingi watu , mfano huyo bint amelipa m5, anatakiwa na yeye aingize watu wawili Kwanza ambao watatoa m5 kila mtu in total inakuwa m10, Kwa kazi hyo huyo bint atalipwa only us dollars 200, hapo ndo atatakiwa kutengeneza chain kila atayekuwa anaingia kwenye chain yake atakuwa anakula commission, hapo ili faida ionekane inabidi watu uliowaunga na wao waunge watu wa kutosha ili kutengeneza chain ndefu hapo ndo utamake money, kutengeneza chain ndo pagumu ndo mana 90% ya wanaojiunga wanaangukia pua, wanaowin ni Wale waliotangulia kujiuga mwanzo kabisa wakati kampuni inaingia nchini, .......
 
Kwa qnet kidogo napata kigugumizi, sababu aliyetaka kuni unganisha hakuwa muwazi sana. Ila alliance nilielezwa kwa kina.

Kama utahitaji maelezo labda nikuunganishe na huyo jamaa ambae yeye tayari ni member wa qnet labda waweza ng'amua jinsi inavyo fanya kazi ukimdadisi vizuri.

Kwa hapa jukwaani sina hakika kama yupo atakae funguka vizuri kuhusu hizi biashara. Maana wengi wao huwa sio wawazi sana. Sentensi yao kuu ni kwamba uende ofisi zao zilipo ili kupata maelezo zaidi. Na ukifika narudia ukiwa na tamaa basi waweza jitosa maana jamaa wanaushawishi mkubwa.

Hata mtoa mada ameeleza hapo kuwa sio utapeli ila ukishatoa pesa,ili wewe upate pesa basi utahitaji kufanya juhudi kubwa, yani kila mtu kwako utamuona ni fursa.

Experience niliipata kwa hawa Alliance in motion.
Kwa ujumla ni biashara zisizo eleweka. Yaani zinataka uamini na uingie kwanza ndio utaelewa na sio uelewe kwanza ndio uamini na kuingia

Jambo jingine hata kama wanaodai kufaidika hawafunguki sana mwanzo lakini maendeleo yao si yanaweza kuonekana waziwazi angalau ikawa ndio ushuhuda wenyewe?
 
Wanavaa vizuri Sana.
Wanatembelea sehemu za gharama kubwa hasa migahawa ya bei mbaya
Wanaongea habari kubwa Kama kumiliki vitu vya thamani Kama magari ya thamani kubwa, Kuwa na apartment, kusafiri nje na kulala Kwenye 5 Star hotel n.k
Lakini mfukoni hawana hata mia
 
Kwa ujumla ni biashara zisizo eleweka. Yaani zinataka uamini na uingie kwanza ndio utaelewa na sio uelewe kwanza ndio uamini na kuingia

Jambo jingine hata kama wanaodai kufaidika hawafunguki sana mwanzo lakini maendeleo yao si yanaweza kuonekana waziwazi angalau ikawa ndio ushuhuda wenyewe?
Hii ni point mkuu mafanikio yao yapo kina nadharia zaidi, utawaona wamevaa suti uchwara. Wameshika pesa na kupiga nazo picha lakini ukija katika maisha yao halisi wapo kawaida tu.
Mfano huyo jamaa wa Qnet ambayo kiingilio ni zaidi ya milioni nne. Ilifika hatua anatuma screenshot ya balance yake iliyo bank alikuwa na around milioni 3.7. Sikutaka kuwa mwepesi kuamini kuwa ile pesa imetokana na hiyo biashara, nikataka athibitishe kwa kunitumia bank statement ili nione vyanzo vya hiyo pesa. Ili nijiunge alishindwa kufanya hivyo.
 
Mkuu unaweza kuelezea zaidi kuhusu Qnet? Kuna mtoto wa sister anawasumbua sana wazazi wake wajiunge na entrance fee ni 5m.

Baba ya mtoto(shemeji yangu) kaniuliza kama naijua na wanapataje pesa bahati mbaya sina ninalolijua kuhusu hiyo biashara. Wasiwasi wa shemeji yangu ni kwamba huo ni utapeli na mwanaye anashauriwa vibaya na kutumiwa na hao wenye biashara

Ajabu ni kwamba my sister anaelekea kuingia king maana ameanza ku side na mtoto kumshawishi baba yake wajaribu kum support binti aingie labda ni kweli kuna faida

Nilichokiona na kuwashauri ni kwamba hata wao wazazi hawajaelewa hiyo biashara inaendaje na watapataje faida? Kwahiyo wakikishe wanaelewa kwanza kabda ya kuingiza pesa yoyote huko
MKUU,NAKUOMBA KWA NGUVU ZUIA HILI JAMBO AISEE,

NAKUOMBA TENA MKUU,MUAMBIE HUYO BINTI ASIFANYE HILO JAMBO,SIO JAMBO JEMA KABISA
 
Back
Top Bottom