Wala usipate shida, hapa hapa nitatoa maelezo ya QNET wanavyofanya kazi zao, maana wapo jamaa kadhaa waliingia mkenge kujiunga huko wakalizwa hatari.
-Kifupi kabisa, msingi wao mkuu ni ule ule kama Forever Living, Alliance in motion nk, zote ni PYRAMID SCHEME (Yaani wachache wanaotangulia kujiunga wanavuna zaidi kupitia migongo ya wengine wengi wanaofuata nyuma yao katika mnyororo) Katika hilo hakuna tofauti.
-Kuna gharama(mtaji) wa chini wa kujiunga, ambazo kwa sasa ni zaidi ya shilingi 4.5milioni. Bila hicho kiasi kukilipa kwa mara moja huwezi kujiunga na QNET. Wao watakwambia sio gharama za kujiunga bali ni pesa yako unayotumia kununua bidhaa au huduma za Qnet! (Hapo utaambiwa bidhaa zenyewe ni Saa ya mkononi, Pafyumu, kulala kwenye hoteli kali ya kitalii huko Asia nk.)
-Kamwe hawatakwambia kinagaubaga biashara yao kirahisi mtaani, lazima watakuita uje kwenye ofisi zao(ndani ya chumba maalum!), hapo watajipanga watu kadhaa kukufanyia 'brain washout' na kukupa maelezo marefu mazuri na matamu ya kukufanya uwe milionea kupitia Qnet kwa muda mfupi na bila kuhangaika kabisa, na hicho kitu watakifanya kwa ustadi mkubwa sana, kwa hatua au siku kadhaa kabla ya kukwambia utoe pesa kujiunga. (Wakati wote huo watakwambia hiyo ni secret opportunity, usiulize mtu mwingine yoyote wala kusema sema kwa watu ovyovyo!).
-Sasa ukishajiunga tu na Qnet kwa kutoa zaidi ya 4.5milion ndio akili inafunguka na kujua kuwa umelizwa au kugundua kuwa umelionea siyo kitu kirahisi kabisa, sasa mtu ndio anahangaika kutafuta 'wajinga' wengine kadhaa ili wajiunge kwenye mnyororo wake ili kuanza kufidia kile ulicholizwa, na hapo inakuwa ni suala la kufa na kupona.
Kwa leo niishie hapa......