Biashara za mitandao (kuunganishana) zinavyowaliza first year vyuoni

Biashara za mitandao (kuunganishana) zinavyowaliza first year vyuoni

Saa 11 jioni niliskia watu wanasemaw GOOD MORNING uchochoro mmoja hv baada ya HESLB
Hao jamaa ni hatari.
Ni kikosi kazi kamili.
Huwa wanamsoma kwanza mtu anayeletwa kuja kupigwa somo la kujiunga. Wakijua wewe ni mtu wa kidini, basi watajipanga hadi angle za kidini, wakijua wewe ni mtu kisayansi wataweka kikosi cha watu wanaojua sayansi, kama wewe ni mtu wa kiheshima basi utashaanga unakutana na kikosi kazi za waheshimiwa siku hiyo.

Hapo ni mwendo wa Good morning!!!!!
 
Mkuu unaweza kuelezea zaidi kuhusu Qnet? Kuna mtoto wa sister anawasumbua sana wazazi wake wajiunge na entrance fee ni 5m.

Baba ya mtoto(shemeji yangu) kaniuliza kama naijua na wanapataje pesa bahati mbaya sina ninalolijua kuhusu hiyo biashara. Wasiwasi wa shemeji yangu ni kwamba huo ni utapeli na mwanaye anashauriwa vibaya na kutumiwa na hao wenye biashara

Ajabu ni kwamba my sister anaelekea kuingia king maana ameanza ku side na mtoto kumshawishi baba yake wajaribu kum support binti aingie labda ni kweli kuna faida

Nilichokiona na kuwashauri ni kwamba hata wao wazazi hawajaelewa hiyo biashara inaendaje na watapataje faida? Kwahiyo wakikishe wanaelewa kwanza kabda ya kuingiza pesa yoyote huko
Mkuu, wake up! Hao ni matapeli, watakupa maelezo ambayo kama huna ufahamu mkubwa utawaamini, tapeli anachotafuta ni wewe kumuamini.

Mwambie shemeji asithubutu kwa namna yoyote ile kuweka pesa zake humo.
 
Mkuu daah wambie wakae mbali, tatizo linakuja kwenye kumuunga mtu, Kwanza kumpata wa kumuunga ni kimbembe , wengine mpak wanaroga ili kuwaingiza kingi watu , mfano huyo bint amelipa m5, anatakiwa na yeye aingize watu wawili Kwanza ambao watatoa m5 kila mtu in total inakuwa m10, Kwa kazi hyo huyo bint atalipwa only us dollars 200, hapo ndo atatakiwa kutengeneza chain kila atayekuwa anaingia kwenye chain yake atakuwa anakula commission, hapo ili faida ionekane inabidi watu uliowaunga na wao waunge watu wa kutosha ili kutengeneza chain ndefu hapo ndo utamake money, kutengeneza chain ndo pagumu ndo mana 90% ya wanaojiunga wanaangukia pua, wanaowin ni Wale waliotangulia kujiuga mwanzo kabisa wakati kampuni inaingia nchini, .......
Hiyo 200USD unaipata kwa wiki au mwezi?
 
Hizi mambo zilinikosanisha na watu..
Mimi niliungwa nikatoa pesa yangu. Na mimi nikatafuta wanyonge wangu watano nikawaunga wakanipa pesa.
Sasa tatizo likaja pale kwa wale watano niliowaunga wao wakakosa watu..

Baada ya muda wakaona mimi ndo tapeli nimewapiga wakaanza kunidai..
Mimi mwenyewe siwezi kuwapa pesa yao sababu na mimi niliungwa nikatoa pesa
Inamaana ningelipa mimi ndio ningekula loss.

Basi nikawa mbuzi tu sikuwalipa.. waliniandama kinoma lakini mwisho wa siku wakabaki kununa tu na hela nikaitafuna.

Baada ya hapo nikisikiaga mambo ya biashara za hivyo huwa hata siwasikilizi na wakikomaa nawatukana kabisa
 
Wewe kwa sbb ushapata ABC hawatakuweza! Utakuwa unawaenjoy tu! Mf unaweza kuwaambia wakukopeshe hiyo 5m afu utakuwa unawalipa kidogo kidogo kutoka ktk bonus zako! So msmamo wako unabaki hapo hapo!
Hivi unaweza kujua kabisa kua ni wapigaji na ukaingia kwenye ofisi zao usichomoe.
Kwa mfano kwa tahadhari hii tuliyopewa hapa halafu nikaamua kwenda kujionea mwenyew kwenye hizo ofisi zao huku nikiwa najua kabisa sina nia ya kujiunga,inawezekana humo ndani mm kubadili maamuzi kweli?
 
Hii ni point mkuu mafanikio yao yapo kina nadharia zaidi, utawaona wamevaa suti uchwara. Wameshika pesa na kupiga nazo picha lakini ukija katika maisha yao halisi wapo kawaida tu.
Mfano huyo jamaa wa Qnet ambayo kiingilio ni zaidi ya milioni nne. Ilifika hatua anatuma screenshot ya balance yake iliyo bank alikuwa na around milioni 3.7. Sikutaka kuwa mwepesi kuamini kuwa ile pesa imetokana na hiyo biashara, nikataka athibitishe kwa kunitumia bank statement ili nione vyanzo vya hiyo pesa. Ili nijiunge alishindwa kufanya hivyo.
Daaah, kuna jamaa yangu akinusurika na hii ishu, nikipata muda mzuri nitaeleza hapa.
 
Mkuu, wake up! Hao ni matapeli, watakupa maelezo ambayo kama huna ufahamu mkubwa utawaamini, tapeli anachotafuta ni wewe kumuamini.

Mwambie shemeji asithubutu kwa namna yoyote ile kuweka pesa zake humo.
Asante sana mkuu kwa ushauri. Actually baada ya mjadala wa jana hapa JF na kusoma maoni kutoka kwa watu tofauti nimeshampigia simu shemeji yangu nikamwambia astop kwanza then nitaongea nae kwa kirefu baadae
 
Hayo makitu wanapatikana sana wanachuo washamba washamba ambao wameingia mjini mara ya kwanza baada ya kujiunga chuo kikuu

Na wanafocus kwa wanachuo lwasabab wanajua wanahela za boom laki tano tano kila baada ya miezi miwil na wengi huwa ni washamba wa mji na ni washamba wa kupata hela kwa mkupuo

Kuna jamaa mmoja tulisoma nae chup ametokea Tandahimba ndani ndani huko, sijui ilikuwaje akaingia king kwa hao Alliance In Motion Global, yani yule jamaa ilikuwa kila boom likiingia tu moja kwa moja analitoa lote analipeleka Alliance, ilifikia kipindi hadi anakosa hela ya kula anakuja kugongea msosi magetoni kwa washikaji

Ilifikia kipindi ikawa anatoa boom lake lote na anakopa nyingine kwa washkaj kwa kuwaahidi malipo kede kede, ilifikia mda had UE alikuwa anashindwa kufanya kutokana na kutokulipa outstanding dues, alikuaa anafanya special exams na alikuwa hashikiki hata kidogo, ukitaka mgombane mwambie kwamba izo ishu hazifai

Yan hadi tunamaliza chuo yule jamaa alikuwa na madeni yakutosha na sijui kama alifanya hata UE ya mwisho,
 
Binafsi hii biashara ipigwe marufuku..... Ni ya hovyo kabisa..... Inafanya watu wawe wavivu wa kufikiri kwa kujengwa na ndoto zisizotekelezeka. Kuna jamaa yangu alibandika sebuleni kwake Picha ya jumba kama hekalu na magari ya maana Bentley Ferrari VX V8 kuwa atakuwa nayo ndani ya miezi Sita na kazi Ata acha. Hadi Sasa Ana baiskeli tu..... Nayo ni ya mtumba.....
 
Asante sana mkuu nitafanya hivyo. Dakika chache zilizopita sister katoka kunipigia, kumbe kuna pesa 4.5m walishalipa kwa ajili ya degree course(undergraduate) ya online inayoendeshwa na na University moja inaitwa Quest University ipo Malaysia( ambayo ni Education Institution ya iliyo chini ya hao Qnet). Mtoto wa sister yupo UD mwaka wa kwanza sasa anataka kusoma online degree nyingine through hao Qnet

Kanitumia risiti ya hela waliyolipa bank naona kama ni malipo ya manunuzi ya commodities yaani hata haieleweki. Sasa mtoto ndio anawashinikiza wazazi wajiunge kununua products ili eti watengeneze pesa!

Kuna mdogo wangu anasoma SUA (mwaka wa kwanza) na mwingine Muhimbili (mwaka wa kwanza pia) nao wamelipia hizo online degree kwenye hicho chuo cha Malaysia, kuna siku walinipeleka huko kwenye QNet yao. Looh ni balaa tupu, sijui watu wanawezaje kudanganyika kirahisi vile na kuziingiza familia katika mizigo mizito ya kulipia gharama kubwa za masomo.

Nakumbuka mistari michache ya Fid Q isemayo:, ni mbaya kuhifadhi fuvu la kichwa cha mtu kwenye kabati, ni mbaya zaidi kuwa na ndugu halafu ni kichwa maji.
 
Hiyo 200USD unaipata kwa wiki au mwezi?
Sio Kwa mwez, ukiingiza hao watu ukapewa hyo ndo imetoka hvyo, cha msingi hao unaowaingiza wanatakiwa wapige kazi ya kuleta watu , na Wale wanaowaingiza na wenyewe wapige kazi kuleta watu, wakileta na wao watapata commission Yao na wewe utapata commission Kwa kila member anayeongezeka kupitia chain yako, wakat wanaingiza na we unapambana kuingiza kingi wengine ili chain iwe kubwa, Ila mara ya Kwanza sharti uingize watu wawili Kwanza do upate us dollar 200 na chain yako iwe activated, yaan kiufupi ili chain yako iwe activated zinatakiwa million 15 , ya kwako M5, na za maboya wengine wawili M 10, in return unapewa Dollar 200, na kazi inabaki kwako sasa kutengeneza chain sio kazi rahsi hata kidogo, labda uwe umezungukwa na middle-class people, kuna Mwamba wangu mmoja anaitwa Eliya Mroso tulipiga naye school Galanos Tanga, kampuni ya Qnet ilipoingia Tu nchini akajiunga fasta akaacha na chuo IFM, sa hv ni millionare mkubwa Sana and he is only 26yrs, advantage yake member karbia wote wa Qnet nchi nzima amekula commission zao , Ila wanaojiunga sa hv ni kimbembe kutoboa
 
Mimi nilikoswakoswa, jamaa yangu aliniambia ukiweka M10 utapata faida kubwa na kwenye maisha yako hutonisahau. Lakn hadi leo yeye ni bodaboda. Huwa najiuluza nisingemsahau kwa hasara aliyonipa. Juz juz anakuja nimuazime kilo 1.
 
Kuna mdogo wangu anasoma SUA (mwaka wa kwanza) na mwingine Muhimbili (mwaka wa kwanza pia) nao wamelipia hizo online degree kwenye hicho chuo cha Malaysia, kuna siku walinipeleka huko kwenye QNet yao. Looh ni balaa tupu, sijui watu wanawezaje kudanganyika kirahisi vile na kuziingiza familia katika mizigo mizito ya kulipia gharama kubwa za masomo.

Nakumbuka mistari michache ya Fid Q isemayo:, ni mbaya kuhifadhi fuvu la kichwa cha mtu kwenye kabati, ni mbaya zaidi kuwa na ndugu halafu ni kichwa maji.
Hahahaaa shemeji yangua alienda pia hapo kwenye ofisi yao Sinza. Anasema ni nyumba ipo ndani kidogo na hakuna hata fenicha sasa sijui wanasomaje

Anasema wale watoto kama wamelishwa imani flani hivi ya kimaigizo na hawajielewi. Ukiingia wanakuja wote wanazunguka mduara qanakusalimia Good morning hata kama ni saa nane mchana, kisha wanaanza kukueleza ABC za hayo mambo yao lakini hadi mwisho huelewi kitu

Wanakuingiza kwenye chumba kingine na wanakuja wanafunzi wengine eti wanakupa darasa tena ya hizo products. Kifupi yeye wameshamliza 4.5 za hiyo ada ya mwanae lakini baada ya mimi kuongea nae na kumueleza wasiwasi wangu, hawezi tena kupeleka hata shilingi huko,kwanza anahisi itampotezea concentration mtoto wake kule UD
 
Mimi nilikoswakoswa, jamaa yangu aliniambia ukiweka M10 utapata faida kubwa na kwenye maisha yako hutonisahau. Lakn hadi leo yeye ni bodaboda. Huwa najiuluza nisingemsahau kwa hasara aliyonipa. Juz juz anakuja nimuazime kilo 1.
Inamaana kuna mtu mahali flani anafaidika ja hizo pesa hao wengine wanabaki kupiga debe tu
 
😂😂😂 Hapa unanikumbusha jamaa alipotaka nijiunge DECI wakati huo maana ingekuwa sio imani yangu kunikataza nami ningekuwa miongoni mwa walioliwa noti zao
 
Asante sana mkuu nitafanya hivyo. Dakika chache zilizopita sister katoka kunipigia, kumbe kuna pesa 4.5m walishalipa kwa ajili ya degree course(undergraduate) ya online inayoendeshwa na na University moja inaitwa Quest University ipo Malaysia( ambayo ni Education Institution ya iliyo chini ya hao Qnet). Mtoto wa sister yupo UD mwaka wa kwanza sasa anataka kusoma online degree nyingine through hao Qnet

Kanitumia risiti ya hela waliyolipa bank naona kama ni malipo ya manunuzi ya commodities yaani hata haieleweki. Sasa mtoto ndio anawashinikiza wazazi wajiunge kununua products ili eti watengeneze pesa!
Screenshot_20190822-200548~2.jpeg
 
Back
Top Bottom