Mkuu daah wambie wakae mbali, tatizo linakuja kwenye kumuunga mtu, Kwanza kumpata wa kumuunga ni kimbembe , wengine mpak wanaroga ili kuwaingiza kingi watu , mfano huyo bint amelipa m5, anatakiwa na yeye aingize watu wawili Kwanza ambao watatoa m5 kila mtu in total inakuwa m10, Kwa kazi hyo huyo bint atalipwa only us dollars 200, hapo ndo atatakiwa kutengeneza chain kila atayekuwa anaingia kwenye chain yake atakuwa anakula commission, hapo ili faida ionekane inabidi watu uliowaunga na wao waunge watu wa kutosha ili kutengeneza chain ndefu hapo ndo utamake money, kutengeneza chain ndo pagumu ndo mana 90% ya wanaojiunga wanaangukia pua, wanaowin ni Wale waliotangulia kujiuga mwanzo kabisa wakati kampuni inaingia nchini, .......