Biashara za mitandao (kuunganishana) zinavyowaliza first year vyuoni

[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120] Somo zuri na ubalikiwe kwa kweli.
 
Inamaana mtoto atafaidika? Kwamba itamlipa zaidi ya pesa aliyopewa na wazazi kuwekeza
 
Ila kuna watu wana dhambi jamani vip sasa maisha yaliendaje baada ya kuacha chuo.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120] Somo zuri na ubalikiwe kwa kweli.
Hii kitu ni wengi wanakutana nayo na unakutwa hawana Elimu vizuri kuhusu hizi biashara. Mimi ilinichukua takribani mwezi kuielewa Alliance, maana alie taka kuniingiza kingi kuna baadhi ya mambo hakutaka kuwa wazi hadi niwe nimejiunga.

Hapo ndipo nilipo pata alama ya kuuliza.
Nakuanza kuifuatilia kwa kina.

Hizi biashara si zakuingia kichwa kichwa.
 
Inamaana mtoto atafaidika? Kwamba itamlipa zaidi ya pesa aliyopewa na wazazi kuwekeza
Hapana hatopata pesa zaidi ya ile aliyo peleka kama kiingilio bali kuna asilimia flan ataipata kupitia hao wateja alio waleta so ili iwe endelevu itamlazimu yeye aendelee kuongeza watu na wale wanao ongezwa nao waongeze watu hapo huyo dogo ndio atanufaika, hii ni experience ya alliance ila kampuni zote hizo ni kama zinafanana mifumo.
 
Funguka zaidi mkuu kwa faida ya jamii pana zaidi
 
Kwamaana hiyo kama wazazi wamelipa 5m. mtoto atazipata zote kwa kulipwa kidogokidogo?
 
Mbona serikali inawasajili na wana operate kisheria? Mi wale jamaa wa mikocheni opposite na KFC walitaka kuniingiza cha kike thro my friend from Asia huwa najiuliza govt haijui?
Wanalipa hela ndefu Sana serikali, Maghufuli anavyopenda hela asingewaacha salama...wanampa huge amount so cash
 
Kwamaana hiyo kama wazazi wamelipa 5m. mtoto atazipata zote kwa kulipwa kidogokidogo?
Kwa qnet kidogo napata kigugumizi, sababu aliyetaka kuni unganisha hakuwa muwazi sana. Ila alliance nilielezwa kwa kina.

Kama utahitaji maelezo labda nikuunganishe na huyo jamaa ambae yeye tayari ni member wa qnet labda waweza ng'amua jinsi inavyo fanya kazi ukimdadisi vizuri.

Kwa hapa jukwaani sina hakika kama yupo atakae funguka vizuri kuhusu hizi biashara. Maana wengi wao huwa sio wawazi sana. Sentensi yao kuu ni kwamba uende ofisi zao zilipo ili kupata maelezo zaidi. Na ukifika narudia ukiwa na tamaa basi waweza jitosa maana jamaa wanaushawishi mkubwa.

Hata mtoa mada ameeleza hapo kuwa sio utapeli ila ukishatoa pesa,ili wewe upate pesa basi utahitaji kufanya juhudi kubwa, yani kila mtu kwako utamuona ni fursa.

Experience niliipata kwa hawa Alliance in motion.
 
Mkuu daah wambie wakae mbali, tatizo linakuja kwenye kumuunga mtu, Kwanza kumpata wa kumuunga ni kimbembe , wengine mpak wanaroga ili kuwaingiza kingi watu , mfano huyo bint amelipa m5, anatakiwa na yeye aingize watu wawili Kwanza ambao watatoa m5 kila mtu in total inakuwa m10, Kwa kazi hyo huyo bint atalipwa only us dollars 200, hapo ndo atatakiwa kutengeneza chain kila atayekuwa anaingia kwenye chain yake atakuwa anakula commission, hapo ili faida ionekane inabidi watu uliowaunga na wao waunge watu wa kutosha ili kutengeneza chain ndefu hapo ndo utamake money, kutengeneza chain ndo pagumu ndo mana 90% ya wanaojiunga wanaangukia pua, wanaowin ni Wale waliotangulia kujiuga mwanzo kabisa wakati kampuni inaingia nchini, .......
 
Kwa ujumla ni biashara zisizo eleweka. Yaani zinataka uamini na uingie kwanza ndio utaelewa na sio uelewe kwanza ndio uamini na kuingia

Jambo jingine hata kama wanaodai kufaidika hawafunguki sana mwanzo lakini maendeleo yao si yanaweza kuonekana waziwazi angalau ikawa ndio ushuhuda wenyewe?
 
Wanavaa vizuri Sana.
Wanatembelea sehemu za gharama kubwa hasa migahawa ya bei mbaya
Wanaongea habari kubwa Kama magari ya thamani kubwa, Kuwa na apartment, kusafiri nje na kulala Kwenye 5 Star hotel n.k
Lakini mfukoni hawana hata mia
 
Wanavaa vizuri Sana.
Wanatembelea sehemu za gharama kubwa hasa migahawa ya bei mbaya
Wanaongea habari kubwa Kama kumiliki vitu vya thamani Kama magari ya thamani kubwa, Kuwa na apartment, kusafiri nje na kulala Kwenye 5 Star hotel n.k
Lakini mfukoni hawana hata mia
 
Hii ni point mkuu mafanikio yao yapo kina nadharia zaidi, utawaona wamevaa suti uchwara. Wameshika pesa na kupiga nazo picha lakini ukija katika maisha yao halisi wapo kawaida tu.
Mfano huyo jamaa wa Qnet ambayo kiingilio ni zaidi ya milioni nne. Ilifika hatua anatuma screenshot ya balance yake iliyo bank alikuwa na around milioni 3.7. Sikutaka kuwa mwepesi kuamini kuwa ile pesa imetokana na hiyo biashara, nikataka athibitishe kwa kunitumia bank statement ili nione vyanzo vya hiyo pesa. Ili nijiunge alishindwa kufanya hivyo.
 
MKUU,NAKUOMBA KWA NGUVU ZUIA HILI JAMBO AISEE,

NAKUOMBA TENA MKUU,MUAMBIE HUYO BINTI ASIFANYE HILO JAMBO,SIO JAMBO JEMA KABISA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…