Biashara zangu zimegeuzwa kuwa za ukoo

Biashara zangu zimegeuzwa kuwa za ukoo

Hii hali nakumbuka iltokea kwenye frem yetu....baba alifungua duka....ikawa mahitaji yote tnabeba humo....!!ndugu wa4 wote wakawa wanaingia....mimi kipind hko nipo chuo

Niliporudi sina ajira nkcheki duka wamelifirisi....nikawaita woote mbele ya baba....nkawapa ukweli kuwa ntaingiza mtaji....ntaweka vitu ila sitaki mtu asogeze pua yake

Wakajua utani....tangu nmefungua kwa mtaji hafifu mpk sasa mtaji umekuwa hawajawah kugusa chchte....!!mchango wa chakula nachangia lkn mazoea ya dukan nlishawakataliaga

Weka msimamo kisha usimamie
2020 co mwaka wa hurum ht kdg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wadau naombeni ushauri...

Mimi ni kijana ila Mungu alinijalia ajira ya muda mfupi nikapata pesa nyingi. Sasa nimefungua biashara 2 hapa Dar na zinanilipa, ila tatizo kubwa ni kwamba familia na wanandugu wamekuwa wakifanya kama mali za ukoo.

Kutwa kucha wana matatizo na wamekuwa wakienda hata kama sipo wanachukua pesa kwa waajiri kwa kigezo cha kaka, dada au mjomba n.k

Nifanyaje?
Tafuta Kijana mmoja mnoko muweke hapo uankuwa umemaliza shida pamoja na mlinzi
 
Nasimamia mimi na mzazi wangu wa kike ikitokea pesa zimetoka unakuta kachukua dada sina la kufanya ndio maana naomba ushauri
Unafanya biashara na mama !!?? ... Mpumzishe huyo kaa mwenyewe au ajiri ...hivi aje dada ako na shida na mama amuache !!?? Aje kaka yake amuache tu !!??
 
Uliwaruhusu kuwa karibu yako, usipokuwa makini Kaburi linakuhusu. Ndugu sio watu wa kuwaentertain sana, ila pambana uwe msiri wasijue mambo yako, utakuwa salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wa
Habari wadau naombeni ushauri...

Mimi ni kijana ila Mungu alinijalia ajira ya muda mfupi nikapata pesa nyingi. Sasa nimefungua biashara 2 hapa Dar na zinanilipa, ila tatizo kubwa ni kwamba familia na wanandugu wamekuwa wakifanya kama mali za ukoo.

Kutwa kucha wana matatizo na wamekuwa wakienda hata kama sipo wanachukua pesa kwa waajiri kwa kigezo cha kaka, dada au mjomba n.k

Nifanyaje?
Hongera kwa mafanikio.

Watu wanachuma matunda kwenye mti wenye matunda. Kwa hiyo watu kuja kuhitaji msaada kwako si jambo baya. Kikubwa hapa ni kuwa na utaratibu, kuwa na kiasi.

Kwa ushauri, waambie wakiwa na shida wakuone moja kwa moja wewe. Hii itakupa nafasi ya kufanya maamuzi ya kusaidia ndugu zako. Watu wengi wanapata taabu wakiombwa msaada kujizuia kutoa hata kama bajeti zao haziruhusu. Mwombe Mungu akupe roho ya kiasi ili ikiwa unasaidia, usaidie huku mambo yako mengine yaende sawa sawa.
 
niweke mtu baki km mimi hapo, hata akija mama yako namrudisha kwa tabasamu la bashasha. kuna namna ya kumyima mtu kitu bila ya kuonekana mbaya.
 
Kuna bro wangu wakati nipo dogo alipitia changamoto hiyo ila alivyoniweka mimi kauzu zaidi ya dagaa walijuta kwanza sinaga kabisa desturi ya kucheka wala uoga wa kujibu rafu,heshima ilirudi na mtaji ulikuwa maradufu,ilikuwa hata akija yeye boss mwenyewe kuchukua kitu namchenjia


Sent using IPhone X
 
Back
Top Bottom