King Kong III
Platinum Member
- Oct 15, 2010
- 64,227
- 98,761
Mpo sawa wote, miezi michache nyuma King Kong III alisema tutaokota pesa barabarani, lakin hali imekuwa tofauti
Kuna unafuu Bushmamy ,mimi nipo kwenye udalali , ujenzi na mkaa ,kwahiyo napiga miguu yote yote ,ujenzi ukikata napiga mkaa ,watu washaanza kujenga na kutafuta viwanja ,cha kushauri badili gear upige issue nyingine ,mama kashamleta dangote , ajira elf 9 zishatangazwa ,accounts za wafanyabiashara zimefunguliwa ,kesi feki 147 zimefutwa ,issue hizo zote zitaleta impact kwenye mzunguko wa pesa ,ngoja tuendelee kunywa mtori nyama zipo chini.
Nilivyomaliza form iv nikawa nakamtafuta mshikaji anibrush somo la economics ,alinifundisha kitu kimoja kwamba "you can not make someone well off without making someone else worse off" ,kwenye resources allocation ukiona wewe umekosa basi jua kuna mwingine amepata na vile vile ukipata wewe basi jua mwingine amekosa.
Katika awamu zote kuanzia ya nyerere hadi ya samia kuna watu watakuwa na pesa na wengine watakuwa wanawasindikiza wenzao ,ndio maana enzi za nyerere kina mbowe waliweza kununua mabenzi lakini wazazi wetu walikuwa wanafulia nguo kwa majani ya mpapai.
Tumpe muda mama ,jiwe aligalagaza uchumi angeendelea tena miaka mi5 ingekuwa balaa,mambo yatakaa sawa tu.