Biashara zinazolipa mipakani Tanzania na Zambia

Nashukuru mkuu soon nitaanza process kwa huu mwangaza wako kuna mzee mmoja yeye alikuwa anazipeleka pale Dodoma cjui kama soko lake ni zuri,,
Daah unaambiwa peleka Arusha au Nairobi unazungumzia Dodoma hautaki hela wewe au hauna njaa ya hela Mkuu..mwenye njaa ya pesa akiambiwa kazi vifungo vya shati anafungia kwenye Bus vizuri la Mbeya vizuri na ukifanya uje na mrejesho hapa..
 
Tanzania mazao ni mengi hauwezi kutoa Zambia ukayaleta Tanzania
Ukiishi mipakani utajifunza kitu ipo hivi kama sasa hivi Zambia wana ukame mahindi yatatoka huku kwenda Zambia na kipindi mahindi yakiwa hapa bei kubwa mahindi yatatoka Zambia na kuja kuuzwa kwenye mikoa ya mipakani huu ni mzunguko wa kawaida tu..
 
Daah unaambiwa peleka Arusha au Nairobi unazungumzia Dodoma hautaki hela wewe au hauna njaa ya hela Mkuu..mwenye njaa ya pesa akiambiwa kazi vifungo vya shati anafungia kwenye Bus vizuri la Mbeya vizuri na ukifanya uje na mrejesho hapa..

Sawa mkuu lazima nilete mrejesho
 
Ukiishi mipakani utajifunza kitu ipo hivi kama sasa hivi Zambia wana ukame mahindi yatatoka huku kwenda Zambia na kipindi mahindi yakiwa hapa bei kubwa mahindi yatatoka Zambia na kuja kuuzwa kwenye mikoa ya mipakani huu ni mzunguko wa kawaida tu..
Lini mara ya mwisho mahindi yalitoka Zambia yakaingia Tanzania?
 
Lini mara ya mwisho mahindi yalitoka Zambia yakaingia Tanzania?
Sio lini mahindi mapana yanatoka Zambia na ndio yanauzwa Nairobi mimi kipindi cha Corona nishapakia mahindi ya wafanyabiashara wakitoa Chinsali /Zambia na kupeleka transit Nairobi kwa kupitia mpaka wa Holili..
 
Kumbe yalivuka Tanzania na kwenda Kenya
Unachobisha ni nini mazee nenda hapo Isongole uone Truck za Tanzania zikitoa mahindi Malawi pamoja na Karanga mwezi uliopita Malawi wamepiga marufuku uuzaji wa Maharage kuyatoa nje...Kasungu,Malawi pana soko kubwa la Mazao yanayokuja Tanzania sisi wengine tumezurula sana aisee...
 
Una maneno mengi sana. Hoja yangu ilikuwa mahindi ya Zambia kuuzwa kwa watumiaji wa Tanzania wakati watu wana mahindi yamejaa kwenye stoo

Mimi kama kutembea hizo nchi zotenimetembea sijaishia tu border hadi interior nazifahamu sana

Mwaka jana Desemba na mwaka huu January nimeuza sana mahindi Malawi nafahamu A-Z hali ya Malawi
 
Pia katavi pako vzr kama anataka ku deal na karanga
 
Uliuza kwa sababu ya rate biashara ya Malawi na Tanzania inategemeana na Exchange rate pia kama chenji wenyewe wanavyosema ikiwa sio nzuri huwezi kwenda kuuza biadhaa iwe Malawi au Zambia...sasa hivi hela ya Malawi ipo juu ukipeleka bidhaa kwa chenji iliyopo utapata kitu mwaka juzi iliwahi kufika 1.4 Malawian Kwatcha kwa 1 Tsh shilings...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…