Bibi anapoteza kumbukumbu, anaongea mwenyewe, tumpe dawa ghani?

Bibi anapoteza kumbukumbu, anaongea mwenyewe, tumpe dawa ghani?

Habari za usiku wanajf, bibi yangu miaka 87 anapoteza kumbukumbu, anaongea mwenyewe, pia vitu vimetokea zamani anasema vimetokea jana. Atumie dawa ghani
Hayo ni matatizo ya uzee mana hata bibi yangu mm nae ananibishiaga mambo ambayo kaongea mwenyewe. Geriatrics sijajua kama ni tasnia kubwa kibongo bongo, mpeleke psychiatry
 
Habari za usiku wanajf, bibi yangu miaka 87 anapoteza kumbukumbu, anaongea mwenyewe, pia vitu vimetokea zamani anasema vimetokea jana. Atumie dawa ghani
Hakuna dawa ya moja kwa moja ambayo mtu anaweza kutumia bila ushauri wa daktari, lakini baadhi ya dawa zinazoweza kusaidia kudhibiti dalili za kupoteza kumbukumbu (kama vile donepezil, rivastigmine, au memantine).

Pia, ni muhimu kumuona mtaalamu wa magonjwa ya wazee (geriatrician) au mtaalamu wa akili (psychiatrist) kwa uchunguzi wa kina na mpango wa matibabu unaofaa.

Wanaweza kupendekeza pia msaada wa kifamilia na matunzo maalum kulingana na hali ya bibi yako.
 
Si kuna maradhi ya Dementia na Alzheimers nayaonaga kwa wazungu walioenda age kimtindo ama? Huyo ni umri tu, madawa mkimpa mtakua mnamjazia sumu tu ila kama mnapendelea mumpeleke huko sipitali mkajue shida ni nini.
 
Hawezi tena poteza bikra,,,kwa hiyo ni vyema mkamwacha apoteze kumbukumbu,,,Subiri na wewe uwe babu
 
Msimsumbue na kumuuwa kwa madawa
Huu ni ugonjwa unaowapata wazee na hakuna dawa ila kumuangalia asipotee tu
Dementia ni kupoteza kumbukumbu sasa itarudi vipi?
Hata wazee wakizungu wanalelewa tu na wanapewa dawa kama wakiumwa
Ila msimshangae ni kawaida kwa binadamu tukizeeka ingawa sio wote
Wengi hufa na fahamu zao kabisa
Msaidieni sana
 
Hata wazee wakizungu wanalelewa tu na wanapewa dawa kama wakiumwa
Ila msimshangae ni kawaida kwa binadamu tukizeeka ingawa sio wote
Wengi hufa na fahamu zao kabisa
Msaidieni sana
Unamaanisha hata mimi nitakufa?
 
Si kuna maradhi ya Dementia na Alzheimers nayaonaga kwa wazungu walioenda age kimtindo ama? Huyo ni umri tu, madawa mkimpa mtakua mnamjazia sumu tu ila kama mnapendelea mumpeleke huko sipitali mkajue shida ni nini.
Hospitali ni muhimu watampima
 
Back
Top Bottom