Bibi anasema "Tusiilaumu serikali kwa tozo mpya, bali tubadili mfumo wa kuhifadhi na kutumiana pesa"

Bibi anasema "Tusiilaumu serikali kwa tozo mpya, bali tubadili mfumo wa kuhifadhi na kutumiana pesa"

Kanal Hilal

Member
Joined
Feb 4, 2017
Posts
62
Reaction score
121
Nimefuatilia mijadala mbali mbali kuhusu ongezeko la gharama na tozo mpya za miamala ya kifedha kwa upande huduma wa mitandao ya simu za mkononi. Mjadala umekuwa mkubwa sana kwenye mitandao mbalimbali.

Wananchi wanalalamikia ongezeko la tozo hizi huku kiasi kikubwa cha makato (tozo) hizo kikienda kwa serikali, ambapo gharama za miamala kwa upande wa mitandao ya simu zikibaki vile vile.

Bibi yangu anasema hivi, "hili si swala la kuilalamikia au kuilaumu serikali. Ni swala la kufanya maamuzi tu ya pamoja kama wananchi, kwa sababu kuna njia mbadala za kutatua. Ikiwa gharama ni kubwa na hatuwezi kumudu tunapaswa kubadili mfumo. Badala ya kutumia huduma za kifedha za simu, tutumie huduma za kifedha za benki ambazo zimebaki vile vile na ni nafuu zaidi."

Maneno ya bibi yana uhalisia zaidi. Nadhani ndio muda muafaka wa mabenki kutimia hili kama fursa ya kujiimarisha kwa kusambaza mawakala wao maeneo kwenye maeneo mbali mbali nchini, mjini na vijijini. Hilo litatuhakikishia wateja kupata huduma mahali popote pale tutakapokuwa.

Tazama, kutoa pesa shilingi 200,000 hadi 299,000 kupitia Akaunti ya CRDB tozo yake ni shilingi 4,900 tu wakati TigoPesa, Airtel Money, M-Pesa na wengine tozo ni shilingi 8,240. Maana yake ni kuwa, kutoa pesa benki ni nafuu mara mbili zaidi ya kutoa pesa kwenye mitandao ya simu.

Nikiitafakari vema kauli ya bibi, nadhani sasa ndio wakati sahihi kwa wananchi kuanza kumiliki akaunti za benki na kuzitumia akaunti zao kama MUARUBAINI tatizo hili la kupanda kwa tozo za miamala.

Ingawa kuna dhana kuwa huduma za benki ni kwaajili ya wenye pesa (matajiri) tu-: hii si kweli. Hata mimi ni wewe tunaweza kutumiana pesa kupitia benki. Upatikanaji wa huduma ukiboreshwa ni rahisi na salama zaidi.

Wapo wanaosema eti bibi na babu zetu kule vijijini hawawezi kumudu huduma za kibenki kama ilivyokuwa kwenye simu. Katika hili nadhani hatujafanya utafiti (research) wa kutosha. Nenda vijijini ambako wazee wetu wanajishughulisha na kilimo, utagundua kuwa pesa zao zote za mauzo ya mazao wanaziweka kwenye AKAUNTI ZAO ZA BENKI.

Bibi yangu ana akaunti kwenye mabenki matatu tofauti na kote katunza pesa. Na yeye ndiye aliyeniambia nimtumie shilingi 10,000 ya sikuu ya Iddi el Hajji kwenye akaunti yake ya benki ili kuepuka makato mapya.

Ndugu zangu, tubadilike. Tunapaswa kubadili mfumo wa kutumiana fedha. Akaunti za benki kwa sasa zinalipa zaidi ya akaunti za simu za mkononi.

Na Hilal Kanal.
July 17, 2020.
 
Cha ajab hii tozo ikifutwa watu watasema SERIKALI yetu imetusaidia kufuta!
(Soma unielewe)
 
Hii tozo itaondoka tu, huu mwaka hauishi, najua ninachozungumza
Kuondoka inawezekana lakini sio rahisi, ni lazima kuwe na mtazamo tofauti kutoka kila upande. Makampuni ya simu yatakapopata hasara na kulalamika pengine inaweza kuleta ahueni
 
Cha ajab hii tozo ikifutwa watu watasema SERIKALI yetu imetusaidia kufuta!
(Soma unielewe)
Nakuelewa, uelewa wa mambo ambayo ni haki yetu ndio tatizo kuu. Always mzazi hasifiwi kwa kuihudumia vema familia yake kwani ni wajibu wake kuipatia huduma bora.
 
Kuondoka inawezekana lakini sio rahisi, ni lazima kuwe na mtazamo tofauti kutoka kila upande. Makampuni ya simu yatakapopata hasara na kulalamika pengine inaweza kuleta ahueni
Hayo yote yanafahamika, huwezi kubadilisha muelekeo wa maji ya mto kurudi nyuma, haiwezekani, hii tozo inaondoka, period
 
Wewe unafikiri kila mtu yupo mjini? Kuna mtu yupo Maisome hakuna benki wala wakala lakini kuna mpesa, kutoka hapo kwenda benki kiometa 130 itawezekana kweli? Think big.
 
Tozo za kwenye bank muda si mrefu na zenyewe zitapandishwa, subirini muongozo kutoka BOT muda wowote ule. Jambazi lina mahesabu makali sana, msifikiri halikuwaza kwamba mtakimbilia kwenye mabank...
Mabenki yenyewe yalishakuwa wafu kitambo sana. Kuyaongezea gharama ni kuyafanya ndio yanuke kabisa. Watumiaji wa benki kwa makadirio tu haraka haraka hawakufika hata 30m kati ya watanzania 60m. Na ukitazama kodi wanazolipa, nadhani hii inaweza kuwa ndio mbinu ya kuyanyanyua tena (mabenki).
 
Wewe unafikiri kila mtu yupo mjini? Kuna mtu yupo Maisome hakuna benki wala wakala lakini kuna mpesa, kutoka hapo kwenda benki kiometa 130 itawezekana kweli? Think big.
Sasa hivi ni tofauti kabisa mkuu. Mm nimetembea karibu Tanzania nzima. Naona idadi ya mawakala inayofanana kwenye mitandao na mabenki.

Sehemu nyingi ambazo kuna wakala wa TigoPesa, Aurtel Money na MPesa basi hapo pia kuna huduma za NMB, CRDB (Fahari Huduma) nk. Pia nimesema hapo, ndio wakati wa benki kuboresha zaidi upatikanaji wa huduma hasa maeneo ya ndani ndani sana (vijijini).
 
Back
Top Bottom