Bibi harusi atoroka saloon na kwenda kumuaga mpenziwe wa zamani kwa mahaba

pilu

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2011
Posts
488
Reaction score
43
Jamani wana jamvi kuna hili limetokea ,bibi harusi amefumaniwa gest ndani ya room tena akiwa amevua shela{gauni la harusi} baada ya kutoroka saloon akiwa anarembwa kwa ajili ya harusi na kwenda kumuaga mpenziwe wa zamani kwa mahaba,
kwa bahati mbaya au nzuri mmoja wahudumu wa gest husika alikua anamjua bi harusi huyo kwani na yeye alitarajia kuhudhuria hio harusi ndipo akatoa taarifa kwa ndugu wa bi harusi kwa kua hakufurahishwa na hilo, kwa hio watu wachache upande wa bi harusi na mmewe mtarajiwa ndo wamejua hilo tukio,mme yuko njia panda kwani maandalizi yote yalishakamilika na hata ndugu wa mbali washafika kwajili ya harusi.

Tumshauri bwana harusi afanyeje au achukue uamuzi gani kuhusu harusi?
 
Tumshauri nini sasa?
Kama anataka kunyoa anyoe na kama anataka kusuka asuke.
 
Mwacheni aamue mwenyewe. Si ameona mlicho ona? Au kuna data zingine nyinyi mnazo yeye hana?

yanahitajika maamuzi ya haraka na bwana harusi yuko katika hali ya mshtuko,mchango wako tafadhali.
 
Kama kashindwa kujiheshimu siku hii ya muhimu kwake hataweza kujiheshimu huko mbeleni, bora jamaa aamue moja au aishi kwa maumivu siku zote za maisha yake na hiyo ndoa

Note
Siwanawake wote wanahadhi ya kuolewa, wengine wanapaswa wabaki kitaa kwa ajili ya mapozeo ya makapera
 
sasa tunamshauri bi harusi ama bwana harusi?
unahitaji kumuuliza bwana harusi nae kama aliaga leo ama jana?
 
too fictional hii....
hebu sema harusi ilikuwa ifungwe kanisa lipi?
na mchungaji yupi?
ukumbi upi mmekodi kwa sherehe???????
 
Ni hivi alienda kumuaga mpenziwe wa zamani!!!!! maana yake sasa ataanza maisha mapya sasa tatizo nini? ukweli utabaki kuwa yule hakumkuta bi........na ile kitu haina makombo aache wivu yeye achukue mzigo wake la muhimu amkanye asirudie tena baada ya kuolewa.
 
too fictional hii....
hebu sema harusi ilikuwa ifungwe kanisa lipi?
na mchungaji yupi?
ukumbi upi mmekodi kwa sherehe???????

si vizuri kwa sasa kuyaweka wazi sana kabla mume hajafanya maamuzi kwani taarifa ulizouliza zikisambaa sana mapema na bwana harusi akijua hilo litampa shida kisaikolojia.
 

@kirumonjeta
ahsante kwa ushauri wako ntaufikisha mahala husika.
 
sasa wifi, anataka kusuka na rasta hakuna
anataka kunyoa ila sura hailipi
hapatoshi sasa,lol:eyebrows:
Tumshauri nini sasa?
Kama anataka kunyoa anyoe na kama anataka kusuka asuke.
 

Umeimaliza kesi mkuu! Huyo mwanamke ni typical malaya, na malaya huwa hawaolewi au kuoa.
 
Pilu nisamehe kwam nitakukwaza BUT siamini hii habari kwa sababu zifuatazo....


  1. Bibi harusi kaenda na shela guest.... Jamani hivi waelewa karaha ya kuvaa shela let alone kuanza kuzunguka nalo? Kwamba yee ni mjinga kiasi gani aende ku cheat na nguo ambayo kila mmoja lazima amtazame apitapo.
  2. Mwanaume ambae ana cheat na mwanamke wa mtu hasa wa ndoa/anatarajia kufunga ndoa yupo soo makini. Sidhani kama alikua amebanwa saaana kutaka fanya hilo tendo to the extent ya kumpokea bi dada na shela tena guest.
  3. Ni kweli Uchumba/ndoa nyiingi zimekua za kisanii.... but siamini kua watu wahusika huagana karibu na eneo la tukio (in the sense kua vijimtaa vya karibiana saana).
  4. Kwamba bwana harusi anataka ushauri? Huyo mwanaume wa wapi? Bi harusi mtarajiwa afumaniwe ndani ya shela na woote mwajua alafu atake ushauri zaidi ya kubwaga manyanga? Dah! Enways.... Labda utakuja na wapi yameishia...
 
yanahitajika maamuzi ya haraka na bwana harusi yuko katika hali ya mshtuko,mchango wako tafadhali.

Hii mimi naogopa sana. Kweli tumefikia hatua ya kushindwa kufanya maamuzi mpaka tuwe loaded? Kwamba una maana usipopata ushauri hapa kwenye mablanda hii issue itabaki muted? Aisee hatari!@
 
Kwanza siamini hilo la kwenda na shela guest na pili huyo bwana achukue maamuzi magumu kama ya lowasa
 


@AshaDii
yani upo sahihi kabisa ila nkuhakikishie tu hi nikweli imetokea,
hayo maswali ulouliza ndo nasi twajiuliza pia mpaka tunahisi kuchanganyikiwa kua ujasiri huo bi.harusi katoa wapi wa kufanya yote hayo na vazi hilo, ndomana unahitajika msaada wa jf great thinkers dia.
 

Kwa hzo three premises nilizoweka red nashawishika kuamini kwamba mleta mada ametunga hii kitu.....ni kweli mtu hawez kwenda gesti na shela, na kama ilitokea basi ni crazy na hakustahili kuwa mke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…