Bibi harusi atoroka saloon na kwenda kumuaga mpenziwe wa zamani kwa mahaba

Bibi harusi atoroka saloon na kwenda kumuaga mpenziwe wa zamani kwa mahaba

si vizuri kwa sasa kuyaweka wazi sana kabla mume hajafanya maamuzi kwani taarifa ulizouliza zikisambaa sana mapema na bwana harusi akijua hilo litampa shida kisaikolojia.

Ndio maana unaambiwa hii ni hadithi zaidi. Ina maana hadi sasa ndoa haijafungwa na bibi harusi bado kavaa shela?
Lazima kuna uamizi ambao hadi sasa umeshafanyika.
Kingine, ina maana hadi bibi harusi anavaa shela kuna watu wengi sana hapo, walimwachaje akaondoka?
JF is the home of great Thinkers and not Global publishers.
 
Jamani wana jamvi kuna hili limetokea ,bibi harusi amefumaniwa gest ndani ya room tena akiwa amevua shela{gauni la harusi} baada ya kutoroka saloon akiwa anarembwa kwa ajili ya harusi na kwenda kumuaga mpenziwe wa zamani kwa mahaba,
kwa bahati mbaya au nzuri mmoja wahudumu wa gest husika alikua anamjua bi harusi huyo kwani na yeye alitarajia kuhudhuria hio harusi ndipo akatoa taarifa kwa ndugu wa bi harusi kwa kua hakufurahishwa na hilo, kwa hio watu wachache upande wa bi harusi na mmewe mtarajiwa ndo wamejua hilo tukio,mme yuko njia panda kwani maandalizi yote yalishakamilika na hata ndugu wa mbali washafika kwajili ya harusi.

Tumshauri bwana harusi afanyeje au achukue uamuzi gani kuhusu harusi?


Kuna kitu kinanishawishi kuona kwamba hii ni story na hakuna uhalisia hapa....
kwenye blue inaonyesha kwamba bibi harusi alitenda tukio siku ya harusi... ukilink na hapo kwa red unatuchanganya best....
 
kama ni kweli huyo bi. harusi alienda gest kufanya mapenzi na mpenziwe wa zamani na imethibitika, mimi namshauri jamaa kwa kuwa hawajafunga ndoa amuache huyo bi harusi ili amruhusu aende akaendelee na mambo yake. Usijaribu kuoa mtu amabye hakupendi, utajuta ndugu yangu,. Nadhani kama haya ni kweli ajue Mungu anampenda na ameamua kumuonesha? Je jamaa atajuaje kama hata ujauzito kama anao ni wake na sio wa mpenzi wake wa zamani?

mm napita
 
haya ndio matatizo ya watu kufanya uasherati na watu wengi hata kabla ya kuoana, inamfany kuona akiolewa atapoteza,m hataweza kufanya uovu,

Ndugu kuja kwa ajili ya harusi sio tatizo hata kama ndo ingekuwa siku yenyewe ya harusi au wako kanisani anaruhusiwa kumwacha mara moja

gd day
 
Pilu nisamehe kwam nitakukwaza BUT siamini hii habari kwa sababu zifuatazo....

  1. Bibi harusi kaenda na shela guest.... Jamani hivi waelewa karaha ya kuvaa shela let alone kuanza kuzunguka nalo? Kwamba yee ni mjinga kiasi gani aende ku cheat na nguo ambayo kila mmoja lazima amtazame apitapo.
  2. Mwanaume ambae ana cheat na mwanamke wa mtu hasa wa ndoa/anatarajia kufunga ndoa yupo soo makini. Sidhani kama alikua amebanwa saaana kutaka fanya hilo tendo to the extent ya kumpokea bi dada na shela tena guest.
  3. Ni kweli Uchumba/ndoa nyiingi zimekua za kisanii.... but siamini kua watu wahusika huagana karibu na eneo la tukio (in the sense kua vijimtaa vya karibiana saana).
  4. Kwamba bwana harusi anataka ushauri? Huyo mwanaume wa wapi? Bi harusi mtarajiwa afumaniwe ndani ya shela na woote mwajua alafu atake ushauri zaidi ya kubwaga manyanga? Dah! Enways.... Labda utakuja na wapi yameishia...

Nakubaliana na maoni yako dadangu. Haiwezekani na haiingii akilini bii harusi atoke saloon na shela lake aende gesti mchana kweupe bila wonga akafanye ufusika. Mleta mada kaleta habari yenye mwelekeo wa kubuni zaidi kuliko uhalisia, yaani ni ya uongo mtupu
 
Back
Top Bottom