"Bibi Nisamehe...Najuta"

"Bibi Nisamehe...Najuta"

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Hayo ni maneno ya msaidizi wangu wa nyumbani aka hg.

Nikamuuliza kwanini?

"Aaah bibi si nilimchagua Lowassa".

Kwanini?

"Niliona kama kaonewa na CCM".

Sasa nikusameh kwanini na hiyo ni haki yako kumchagua unaemuona anafaa?

"Bibi sasa nimejionea kwa macho yangu kuwa Magufuli ni bora sana zaidi ya Lowassa na sasa nimeamini CCM hawajamuonea".

Kwanini?

"Bibi wewe wacha tu, nilivyomuona anaongea kwa uchungu Muhimbili nikajuwa huyu kweli anatujali, babu Lowassa hata alivyokuwa akiongea haoneshi kama anajali au hajali.

"Bibi naweza kwenda kufuta kura yangu nimpe Magufuli?"

Mie nikaangua kicheko nikaanza kumuimbia; "CCM mbele kwa mbele".

Hayo ni kwa uchache yaliyojiri leo jioni nyumbani kwangu.
 
Jamani naomba tumuhurumie huyu mzee inasema hasara alioingia katika kuusaka uraisi tangu 2005 hadi 2015 ni takriban Bil 200, ameuza ng`ombe zaidi ya 2000 na baadhi ya Vijanja vyake, ni hasara kubwa mno! anaugulia mengi mwenzenu
 
Hata katika yote ujanja wa mwisho wa binadamu ni pumzi ya mwisho. Mungu atijalie wema katika dunia hii
 
Jamani naomba tumuhurumie huyu mzee inasema hasara alioingia katika kuusaka uraisi tangu 2005 hadi 2015 ni takriban Bil 200, ameuza ng`ombe zaidi ya 2000 na baadhi ya Vijanja vyake, ni hasara kubwa mno! anaugulia mengi mwenzenu

Mimi nnamuonea huruma mkewe, anaonesha kuwa anaumia ndani ya moyo lakini afanye nini. Babu haambiliki.
 
Jamani naomba tumuhurumie huyu mzee inasema hasara alioingia katika kuusaka uraisi tangu 2005 hadi 2015 ni takriban Bil 200, ameuza ng`ombe zaidi ya 2000 na baadhi ya Vijanja vyake, ni hasara kubwa mno! anaugulia mengi mwenzenu

Hata akikaa bila kazi analipwa 80% ya mshahara, gawio la maana voda, hafilisiki hata kwa dawa
 
Back
Top Bottom