Sono...
Waliokuwa hawaijui historia hii waijue.
Ulikuwa unayajua haya?
Kaniandikia msomaji wangu mmoja:
BAADA YA KUSOMA KITABU CHA ABDUL SYKES MSOMAJI ANASEMA:
Kwanza sikujua waasisi wa uhuru wa Tanganyika.
Kabla nilijua ni Julius Nyerere ndio mwanzilishi, kumbe walikuwepo kina Plantan, Kleist Sykes, Abduwahid na wadogo zake Ally na Abbas na wengine wengi na vuguvugu la uhuru tangu African Association.
2. Nimemfahamu Bibi Titi Mohamed vizuri.
3. Nimefahamu mchango wa Kambona kwa TANU.
4. Nimefahamu historia ya Kura Tatu na kujiondoa kwa Zuberi Mtemvu TANU na kuanzisha chama chake cha Congress.
5. Sikujua kama kuna mtu anaitwa Suleiman Takadir na kuondolewa kwake TANU na hatimae kufariki.
6. Sikujua kama kina Mtwa Mkwawa, Nduna Songea walikuwa Waislam.
7. Nimejua sababu ya kufa kwa EAMWS na kuanzishwa Bakwata na kisa cha Rehani Waikela.