Bibi Titi Mohamed na akina Mama wa Bukoba 1950s

Bibi Titi Mohamed na akina Mama wa Bukoba 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Picha hiyo hapo chini ya Bi. Titi na akina mama wa Bukoba wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika nimeletewa kutoka Bukoba na mmoja wa watu ambao nawaheshimu sana katika kuhifadhi kumbukumbu.

Kaniletea picha nyingi na In Shaa Allah nitaziweka hapa JF kwa faida yetu sote.

1628706902374.png

Waliosimama kutoka kushòto Bìti Kaijage, Biti Sheikh, Biti Mwanandege walioketi kushoto Mama Boi, Bibi Titi na Biti Farahani. Hawa walikuwa viongozi wa Umoja wa akina mama wa TANU Bukoba.
 
Peleka msikitini
Makafiri wanapata taabu wanapoona majina ya kiislamu. Lakini huu ni ukweli usiyopingika, waislamu wana mchango mkubwa sana katika ukombozi wa nchi hii kutoka ktk mikono dhalimu ya wakoloni. Wengi wetu tumeathiriwa na historia aliyoiandika mzungu. Bila kutambua kwmb kuna uwongo mwingi ktk hiyo historia. Mfano mmoja wapo wa uwongo wa mzungu ktk historia, ni pale anapotufundisha kwmb "binaadamu hapo kabla alikuwa sokwe"
 
Mohamed Said, salaam.

Ama baada ya salamu Mimi ni buheri wa siha muruwa kabisa.

Dhumuni ya waraka huu ni kuomba kupata wasaa wa kuivinjari maktaba yako adhimu iliyojaa makablasha yenye makala, picha, maandiko, na kumbukumbu za namna kwa namna.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Wako mtiifu, Bujibuji
 
Tupe historia.

Yani katika watu walitakiwa kuchangia hostoria ya tanzania basi mzee hupo na wewe.

Sema historia nyingi za Tanzania ni ngumu kuzijuwa
 
Siwezi kumsahau Bibi Titi alikuwa anatuuzia togwa mtaa wa Ngarambe. Alikuwa mtengenezaji mzuri sana wa togwa la mtama kwenye chupa za soda na Bwimbi.

Baadae akaanza kutuuzia mafuta ya taa, enzi hizo yaliadimika.

RIP.
 
Mkuu..togwa,bwimbwi Ni vyakula asilia,siku hizi havionekani.

Bibi yetu huyu ilipaswa jina na heshima yake katika mapambano vitunzwe. Na vizazi vya Wanawake wa Sasa wasome habari zake badala ya kuwasoma mafeminist wa Ulaya. Historia yetu bado nyembamba na vitu vingi bado havijaandikwa nafurahishwa na Mzee wetu Mohamed Said kwa kuweka bayana yaliyo nyuma ya Pazia. Ningeshauri ayaweke kwenye vitabu na hifadhi nyingine za maandishi naamini siku moja tutarudi kufanys marejeo katika mfumo wetu waelimu na historia ya Tanzania
 
Ungetaja na miaka ingependeza zaidi tujue ni kabla au baada ya kuanza harakati..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Kuna mtu atasema sio Bibi Titi bali ni Masister wa kanisa Katoliki.
 
Mkuu..togwa,bwimbwi Ni vyakula asilia,siku hizi havionekani.

Bibi yetu huyu ilipaswa jina na heshima yake katika mapambano vitunzwe. Na vizazi vya Wanawake wa Sasa wasome habari zake badala ya kuwasoma mafeminist wa Ulaya. Historia yetu bado nyembamba na vitu vingi bado havijaandikwa nafurahishwa na Mzee wetu Mohamed Said kwa kuweka bayana yaliyo nyuma ya Pazia. Ningeshauri ayaweke kwenye vitabu na hifadhi nyingine za maandishi naamini siku moja tutarudi kufanys marejeo katika mfumo wetu waelimu na historia ya Tanzania
Dar...
Nime-document historia takriban yote ya kupigania uhuru wa Tanganyika kuanzia 1929 African Association ilipoundwa hadi 1961 uhuru ulipopatikana.

Ingia: mohamedsaidsalum.blogspot.com

Nitakueleza moja la Bi. Titi.

Abbas Sykes anasema wakati wa kupigania uhuru ilikuwa inafika mahali Mwalimu Nyerere akili imechoka hawezi kuhutubia.

Hapo wako chini ya jukwaa na uwanja umefurika watu.

Basi Nyerere akamwambia Bi. Titi apande jukwaani kuhutubia.

Bi. Titi atafanya hivyo.

Abbas Sykes anasema kutokana na hotuba ya Bi. Titi Mwalimu atapata "cue," na atazumgumza kutokana na yale aliyosema Bi. Titi.

Bi. Titi aliombwa na KANU aende Kenya kusaidia Kenyatta afunguliwe kutoka Kapenguria.

Alifanya mkutano mkubwa sana Tononoka, Mombasa akishirikiana na TANU Club iliyokuwa ikiongozwa na Ismail Bayuni kijana kutoka Moshi.

Kenyatta alipofunguliwa alikuja Tanganyika kumshukuru Bi. Titi na TANU kwa msaada wao.
 
Back
Top Bottom