Bibi Titi Mohammed: Historia, harakati na wasifu wake

BIBI TITI MOHAMMED; MWANAMKE SHUJAA WA HARAKATI ZA UHURU WA TANGANYIKA ALIYEONJA JELA.

Na. Comred Mbwana Allyamtu

Kila binadamu hupitia magumu tena mara nyingine magumu hayo ambayo mimi huyaita ‘kipimo cha uimara wa mtu’ hupelekea kutoka kwa roho.
Leo nimeona si vibaya kuwakumbusha juu ya mwanamke aliyepata kujitoa kwa moyo wote ili nchi yetu ya Tanzania iwe huru lakini inaelezwa kuwa maisha yake ya mwisho hapa duniani yalijawa na huzuni, upweke, kubaguliwa na ufukara mkubwa.
Huyu ni Bibi Titi Mohammed, bila shaka vijana wengi wa sasa hawamjui kabisa mama huyu shupavu na wamekuwa wakisikia au kuiona tu barabara ya Bibi Titi. Kati ya miaka ya 1970 mwanamke mwenye wajihi wa ushupavu Bibi Titi Mohammed alihusishwa katika tukio la kujaribu kutaka kuipindua serikali ya wakati huo, Alihukumiwa kifungo cha maisha jela. Haikuwa rahisi kulipokea hilo kwani baadae alitolewa lakini ameendelea kukana kabisa mpaka umauti ulipomfika mwaka 2000.
Bibi Titi Mohammed aliingia TANU kwa kushawishiwa Schneider Plantan(Wanahistoria wengi huandika Nyerere-Baba wa Taifa ndo alimuingiza kwenye Chama si jambo la kweli) akapata kadi namba 16 na mumewe ndugu Boi Selemani alipewa kadi 15. Bibi Titi alikuwa mwasisi wa Umoja wa Wanawake Tanganyika (UWT) uliokuja kuundwa rasmi mwaka 1962.

Wakati wa harakati za kupigania uhuru alisimamia vikundi vya muziki kama vile lelemama’ na mara zote alitangulia kuongea na umati mkubwa kabla hata Nyerere hajaongea na watanganyika. Alikuwa na maneno makali dhidi ya ukoloni na alikuwa ana nguvu kubwa ya ushawishi. Akiwa na miaka 26 tu alikuwa ni mmoja kati ya wanawake wachache walioaminiwa katika kuongoza mapambano dhidi ya udhalimu waliokuwa wakifanyiwa Watanganyika.

Mwaka 1955, Nyerere na Bibi Titi Mohammed walifanya mkutano mkubwa huko Tabora. Hii ni kutokana na mualiko walioupata toka kwa watu wa huko, Ikumbukwe kuwa Tabora ya wakati huo ilikuwa na hamasa kubwa katika kudai uhuru. Hivyo mualiko ulitoka kwenye kamati ya wazee kama Hassan Mohamed Ikunji, Hamis Khalfan, Swedi Mambosasa, Germano Pacha, Juma Mrisho, Shaaban Mohamed Silabu, Bilali Rehani Waikela, Mohamed Mataka wakati ule akiwa muadhin wa Masjid Nur - msikiti wa Wamanyema pale Tabora.

Kuna mikutano mingi tu ya harakati za uhuru aliyoongoza Bibi Titi mfano ule wa Mombasa akishirikiana na Tom Mboya katika Ukumbi wa Tononoka. Kiujumala mkutano mkuu wa kwanza tabora ulifungua njia kukubalika kwa TanU baadaye kulifanyika Azimio La Tabora’. Azimio hilo liliongozwa na Nyerere na wengine kama Sheikh Suleiman Takadir,Mzee Jumbe Tambaza, Juma Selemani na Bibi Titi.
Baada ya uhuru 1961 alichaguliwa kuwa mbunge na waziri pia. Halikuwa jambo la kushtua kwani alistahili. Mwaka 1963 inaelezwa kulitokea kutokuelewana kati ya Bibi Titi na Mwalimu Nyerere wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya TANU uliofanyika Ukumbi wa Karimjee.

Hapo walitupiana maneno makali kabisa. Inaelezwa kuwa kati ya mambo mengine mengi sababu zilikuwa ni Halmashauri Kuu ya TANU kulivunja Baraza la Wazee wa TANU ambao kwa hakika walisaidia wakati wa harakati za uhuru, Hilo lilipingwa na Bibi Titi.

Jambo jingine linaelezwa na mwandishi Said Mohammed katika maandishi yake kuwa ni uamuzi wa Bibi Titi kuitetea jumuia ya EAMWS ambapo Mwalimu Nyerere alipinga hilo kwani aliona ni hatari kuchanganya ‘Dini na Siasa’. Bado kumekuwa na ugumu kupata taarifa hasa chanza cha mtifuano huo kwani wengi wanaelezea mkutano huo ulikuwa ni nafasi ya kuonesha tofauti zao wazi wazi.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1965 Bibi Titi na Tewa(Tewa Said Tewa alikuwa rais wa jumuia ya EAMWS) wakapoteza viti vyao ndani ya TANU na serikalini. Mwaka 1968, Bibi Titi alikamatwa na kuhusishwa na tukio la uhaini’ Mahakama ilimkuta na hatia ,alihukumiwa kwenda jela maisha. Mwaka 1972 aliachiwa huru kwa msamaha wa rais. Bado aliendelea kukana kuhusika kabisa na tukio hilo. Alirudi na kuendelea na maisha yake ya kawaida huko maeneo ya Temeke.

Inaelezwa kuwa kuwa alipoteza kumbukumbu za harakati za uhuru kama vile picha na taarifa nyingi za vikao.
Aliporudi walikuwa na urafiki kama zamani na Mwalimu Nyerere kama zamani, Aliumwa na kupelekwa na serikali ya Tanzania katika hospitali ya Net Care huko Afrika ya Kusini. Alifariki dunia akiwa hapo hospitalini akipata matibabu tarehe 5 Novemba 2000. Hakika ni ‘mama wa nguvu’ na shujaa mwanamke wa Tanzania yetu.

Ndimi

Comred Mbwana Allyamtu

+255679555526
+255765026057
Mbwanaallyamtu990@gmail. Com
 
roho imeniuma sana napo mkumbuka nyamadwanga marufu kama bibi titi shujaa Wa kindengereko
 
Mndengereko One,
Allah amweke mahali pema peponi mama yetu huyu Bi. Titi biti Mohamed.

Nakuwekea picha yake ya mwaka 1955 wakati anaijenga TANU bega kwa bega
na Mwalimu Nyerere.

Hapo ni Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu mahali Ali Msham alipofungua tawi
la TANU:

Bi. Titi Mohamed wa tatu kushoto waliokaa
 
mm huyu nyamadwanga naudugu nae wa damu
 
Bikra,
Nikikupa link haitoshi wewe kumjua Bi. Titi Mohamed.
Nakushauri soma kitabu cha Abdul Sykes.

Kila alipoweka mguu Mwalimu Nyerere nyayo iliyofuata
ilikuwa ya Bi. Titi.

Bi. Titi kahutubia mkutano wa TANU Mnazi Mmoja 1954
hajaona sura ya Mwalimu Nyerere.

Kaletwa kwenye chama na Schneider Abdullah Plantan.

Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Media Centre Bookshop Msikiti
wa Mtoro na Manyema, Elite Bookshop Mbezi Samaki,
Soma Bookshop Mikocheni na Rubawa Investment Amana.

Nakuwekea hapo chini picha ya Bi. Titi na Nyerere siku ya
kusheherekea uhuru wa Tanganyika katiba ''Ball,'' iliyotumbuizwa
na band Royal Marine Band, Diamond Jubilee Hall:

Kama sitakosea niliwahi simuliwa na mzee wangu kuwa bibi huyo aliwekwa kizuizini ktk kijiji cha gumbiro barazani songea vijijini karibu na madaba akiwa kama bibi maendeleo.watu wa gumbiro ya zamani wanamfahamu sana bibi huyo
 
Naomba kitabu chako
 
cc; Elli BAK MANI tpaul zumbemkuu
Sina hakika kama historia hii mumewahi kuisoma maana thread hii ni ya zamani ila leo mie ndio nimeiona. Nimewashirikisha ili muwaze kama niwazavyo mimi hapa nilipo. Tufanye habari hii ni ya kweli, halafu tuchukulie maisha ya wakati huo (almost 60 years ago) na ya wakati huu tulionao. Kumbe duniani hakuna jipya kabisa! Haya mambo yetu haya kumbe yalikuwepo sana na hayata tuzuia kufikiriwa utakatifu hapo baadae kama tutayaenzi. Ni mtizamo tuu
 
Mie Mkuu nilipata bahati ya kuhadithiwa na watu waliomfahamu Bibi Titi kwa karibu kabisa. Walifahamiana naye hata kuweza kualikana majumbani mwao. Waliniambia kuhusu umaarufu mkubwa aliokuwa na Bibi Titi ndani ya TANU na pia ukaribu wake na Baba wa Taifa. Baba wa Taifa inasemekana alimpenda huyu kwa kujituma kwake katika kuhamasisha Watanganyika kujiunga na TANU na pia kwenye harakati za kutaka uhuru toka kwa Mkoloni. Hili la kuwa mpenzi wa Mwalimu sikuwahi kulisikia, labda hawakuona umuhimu wa mimi kulijua (kama ni kweli)

Bi Titi ni miongoni mwa watu ambao hawakutendewa haki na Nyerere,walijitolea maisha yao kudai uhuru lakini wakaishia jela
 
Jaman cc wengine tunafurahia kuongeza maarifa ktk ubongo wetu maana tulikua hatujui hii hustoria ya bibi titi na mwalimu
 
Sheikh Mohamed Said tupe kidogo juu ya Kambona na Bibi Titi ukaribu wao ulikuweje
 
Kiatu...
Katika TANU kulikuwa na wasemaji kwa maana ya wahutubuaji wakubwa
wawili nao walikuwa ni Nyerere na Bi. Titi Mohamed.

Hawa wawili ndiyo walikuwa vinara wa harakati.

Kambona alikuja baadae katika TANU na yeye alikuwa na uwezo mkubwa
pia lakini hakumzidi Bi. Titi katika kukibeba chama.

Kwa kipindi kile cha kudai uhuru Bi. Titi alikuwa juu zaidi aking'ara zaidi ya
Kambona.

Kambona
alikuja kuwa juu baada ya uhuru kwani haukupita muda Bi. Titi
na Nyerere wakakuruzana mwaka wa 1963 Nyerere alipoonysha dalili za
kutaka kuifungia East African Muslim Welfare Society (EAMWS).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…