Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 887
BIBI TITI MOHAMMED; MWANAMKE SHUJAA WA HARAKATI ZA UHURU WA TANGANYIKA ALIYEONJA JELA.
Na. Comred Mbwana Allyamtu
Kila binadamu hupitia magumu tena mara nyingine magumu hayo ambayo mimi huyaita ‘kipimo cha uimara wa mtu’ hupelekea kutoka kwa roho.
Leo nimeona si vibaya kuwakumbusha juu ya mwanamke aliyepata kujitoa kwa moyo wote ili nchi yetu ya Tanzania iwe huru lakini inaelezwa kuwa maisha yake ya mwisho hapa duniani yalijawa na huzuni, upweke, kubaguliwa na ufukara mkubwa.
Huyu ni Bibi Titi Mohammed, bila shaka vijana wengi wa sasa hawamjui kabisa mama huyu shupavu na wamekuwa wakisikia au kuiona tu barabara ya Bibi Titi. Kati ya miaka ya 1970 mwanamke mwenye wajihi wa ushupavu Bibi Titi Mohammed alihusishwa katika tukio la kujaribu kutaka kuipindua serikali ya wakati huo, Alihukumiwa kifungo cha maisha jela. Haikuwa rahisi kulipokea hilo kwani baadae alitolewa lakini ameendelea kukana kabisa mpaka umauti ulipomfika mwaka 2000.
Bibi Titi Mohammed aliingia TANU kwa kushawishiwa Schneider Plantan(Wanahistoria wengi huandika Nyerere-Baba wa Taifa ndo alimuingiza kwenye Chama si jambo la kweli) akapata kadi namba 16 na mumewe ndugu Boi Selemani alipewa kadi 15. Bibi Titi alikuwa mwasisi wa Umoja wa Wanawake Tanganyika (UWT) uliokuja kuundwa rasmi mwaka 1962.
Wakati wa harakati za kupigania uhuru alisimamia vikundi vya muziki kama vile lelemama’ na mara zote alitangulia kuongea na umati mkubwa kabla hata Nyerere hajaongea na watanganyika. Alikuwa na maneno makali dhidi ya ukoloni na alikuwa ana nguvu kubwa ya ushawishi. Akiwa na miaka 26 tu alikuwa ni mmoja kati ya wanawake wachache walioaminiwa katika kuongoza mapambano dhidi ya udhalimu waliokuwa wakifanyiwa Watanganyika.
Mwaka 1955, Nyerere na Bibi Titi Mohammed walifanya mkutano mkubwa huko Tabora. Hii ni kutokana na mualiko walioupata toka kwa watu wa huko, Ikumbukwe kuwa Tabora ya wakati huo ilikuwa na hamasa kubwa katika kudai uhuru. Hivyo mualiko ulitoka kwenye kamati ya wazee kama Hassan Mohamed Ikunji, Hamis Khalfan, Swedi Mambosasa, Germano Pacha, Juma Mrisho, Shaaban Mohamed Silabu, Bilali Rehani Waikela, Mohamed Mataka wakati ule akiwa muadhin wa Masjid Nur - msikiti wa Wamanyema pale Tabora.
Kuna mikutano mingi tu ya harakati za uhuru aliyoongoza Bibi Titi mfano ule wa Mombasa akishirikiana na Tom Mboya katika Ukumbi wa Tononoka. Kiujumala mkutano mkuu wa kwanza tabora ulifungua njia kukubalika kwa TanU baadaye kulifanyika Azimio La Tabora’. Azimio hilo liliongozwa na Nyerere na wengine kama Sheikh Suleiman Takadir,Mzee Jumbe Tambaza, Juma Selemani na Bibi Titi.
Baada ya uhuru 1961 alichaguliwa kuwa mbunge na waziri pia. Halikuwa jambo la kushtua kwani alistahili. Mwaka 1963 inaelezwa kulitokea kutokuelewana kati ya Bibi Titi na Mwalimu Nyerere wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya TANU uliofanyika Ukumbi wa Karimjee.
Hapo walitupiana maneno makali kabisa. Inaelezwa kuwa kati ya mambo mengine mengi sababu zilikuwa ni Halmashauri Kuu ya TANU kulivunja Baraza la Wazee wa TANU ambao kwa hakika walisaidia wakati wa harakati za uhuru, Hilo lilipingwa na Bibi Titi.
Jambo jingine linaelezwa na mwandishi Said Mohammed katika maandishi yake kuwa ni uamuzi wa Bibi Titi kuitetea jumuia ya EAMWS ambapo Mwalimu Nyerere alipinga hilo kwani aliona ni hatari kuchanganya ‘Dini na Siasa’. Bado kumekuwa na ugumu kupata taarifa hasa chanza cha mtifuano huo kwani wengi wanaelezea mkutano huo ulikuwa ni nafasi ya kuonesha tofauti zao wazi wazi.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1965 Bibi Titi na Tewa(Tewa Said Tewa alikuwa rais wa jumuia ya EAMWS) wakapoteza viti vyao ndani ya TANU na serikalini. Mwaka 1968, Bibi Titi alikamatwa na kuhusishwa na tukio la uhaini’ Mahakama ilimkuta na hatia ,alihukumiwa kwenda jela maisha. Mwaka 1972 aliachiwa huru kwa msamaha wa rais. Bado aliendelea kukana kuhusika kabisa na tukio hilo. Alirudi na kuendelea na maisha yake ya kawaida huko maeneo ya Temeke.
Inaelezwa kuwa kuwa alipoteza kumbukumbu za harakati za uhuru kama vile picha na taarifa nyingi za vikao.
Aliporudi walikuwa na urafiki kama zamani na Mwalimu Nyerere kama zamani, Aliumwa na kupelekwa na serikali ya Tanzania katika hospitali ya Net Care huko Afrika ya Kusini. Alifariki dunia akiwa hapo hospitalini akipata matibabu tarehe 5 Novemba 2000. Hakika ni ‘mama wa nguvu’ na shujaa mwanamke wa Tanzania yetu.
Ndimi
Comred Mbwana Allyamtu
+255679555526
+255765026057
Mbwanaallyamtu990@gmail. Com